Vifijo na Nderemo vyatawala Nairobi Kwenye mapokezi ya Rais Uhuru Kenyatta

Vifijo na Nderemo vyatawala Nairobi Kwenye mapokezi ya Rais Uhuru Kenyatta

Mapengo 17

R I P
Joined
Mar 28, 2014
Posts
1,229
Reaction score
610
Makundi ya watu wanaoshangilia, yamempokea Rais Uhuru Kenyatta ambaye amerejea Nairobi nchini Kenya baada ya kuhudhuria katika Mahakama ya Kimataifa ICC, iliyopo The Hague.

Kenyatta alihudhuria shauri Mahakamani siku ya Jumatano, Octoba 8, 2014 na kuwa rais wa kwanza aliyepo madarakani kufika katika mahakama ya ICC.

attachment.php


Anakanusha mashtaka dhidi yake ya uhalifu dhidi ya ubinaadam kuhusiana na ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007, zilizosababisha vifo vya watu 1,200 na wengine 600,000 kupoteza makazi.


Rais Kenyatta alipokelewa Nairobi kwa gwaride la heshima na ngoma tangu saa 6:30 asubuhi ya leo Octoba 9, 2014.

Source: Citizen TV
 

Attachments

  • kenyatta.jpg
    kenyatta.jpg
    54 KB · Views: 1,036
Hahaha uko sahihi siasa, ni sawa na kuwa na uhuru wa kupata habari unaamua mwenyewe kuwa unapenda zipi na kutoka sehemu gani.

Naipenda katiba ya Kenya lakini simpendi uhuru kenyatta.
 
10505478_862816620403671_2447015658794777821_n.jpg


10678548_862816627070337_1296384297565378832_n.jpg


10516827_862816613737005_5843430159510626764_n.jpg



10690352_862816593737007_1231364202587452668_n.jpg




141008065250_kenyatta_512x288_afp.jpg

Kenyatta alikwenda Hague kwa kikao maalum na mahakama ya ICC

Mamia ya watu kwa shangwe na vigelegele wamemkaribisha Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta baada ya kurejea kutoka kikao chake katika mahakama ya kimataifa ya ICC mjini the Hague.

Kenyatta alihudhuria kikao maalum katika mahakama hiyo Jumatano, na kuwa Rais wa kwanza aliye mamlakani kufika katika mahakama hiyo.
Mahakama hiyo ilimtaka afike mbele yake kutokana na malalalmsihi kutoak kwa kiongozi w amashitkaka kuwa serikali ya Kenya inaficha ushahihidi kuhusiana na kesi inayomkabili.

141009105906_kenyatta_ruto_512x288_bbc_nocredit.jpg

Rais Kenyatta akipokelewa na naibu wake William Ruto

Alikanusha madai ya uhalifu dhidi ya binadamu wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi nchini Kenya mwaka 2007 ambayo yalisababisha vifo vya watu 1,200 na kuwaacha wengine zaidi ya laki sita bila makao.

Kenyatta alipokelewa na idadi kubwa ya watu waliokuwa wanacheza densi pamoja na gwaridde la heshima.
Asubuhi na mapema, wafuasi wake walipanga foleni kwenye barabara ya kutoka uwanja wa kimataifa wa ndege mjini Nairobi.

141009094713_rais_kenyatta_512x288_bbc_nocredit.jpg

Rais Kenyatta katika mahakama ya kimataifa ya ICC

Walipeperusha bendera na kusikika wakiimbia kwa shangwe na kumsifgu Kenyatta wakisema kuwa Rais wao hana hatia.

Rais aliwahutubia kwa mda mfupi umati huo wa watu ambao waliombwa kufika kumpokea rais na waziri wa usalama.
Mwandishi wa BBC aliyefika kushuhudia Rais huyo akiwasili nchini alisema kuwa Kenyatta ana wafasui wengi. chanzo.http://www.bbc.co.uk/swahili/…/2014/10/141009_kenyatta_kenya
 
watu wengi wako wapi??
mbona ni wanausalama ndo wapp wengi??
acha mahaba kijana ,,au we ni wa mombasa??
 
Hata katiba inayopendekezwa ilikabidhiwa kwa rais uwanja wa jamuhuri dodoma na walionekana watu wengi wakicheza na kuimba,je ni kweli inapendwa na watu wote? au ni viongozi wenye maslahi nayo.
Mimi ni mtanzania sizijui vizuri siasa za Kenya na au usafi au ufisadi wa rais wao lkn si sawa kusema kwa kuwa umati ulienda kumpokea ndo anakubalika,kwani ukiwa na lako jambo unaandaa mazingira ya kuvutia watu,k.v ngoma na mziki na unaleta watu kwa usafiri wa bure ilimradi ionekane watu walikuwa wengi.
 
Nampongeza Kenyatta kwa kuitikia wito,na viongozi wengine wa afrika wafuate nyayo zake
naiombea ICC idumu milele kwani viongozi waliowengi afrika bila kilanja wa kuwasimamia ni majanga.
 
Hata katiba inayopendekezwa ilikabidhiwa kwa rais uwanja wa jamuhuri dodoma na walionekana watu wengi wakicheza na kuimba,je ni kweli inapendwa na watu wote? au ni viongozi wenye maslahi nayo.
Mimi ni mtanzania sizijui vizuri siasa za Kenya na au usafi au ufisadi wa rais wao lkn si sawa kusema kwa kuwa umati ulienda kumpokea ndo anakubalika,kwani ukiwa na lako jambo unaandaa mazingira ya kuvutia watu,k.v ngoma na mziki na unaleta watu kwa usafiri wa bure ilimradi ionekane watu walikuwa wengi.

Sijaelewa kinachokuuma ni nini. maana hamna mtu ametaja masuala ya kukubalika.
 
watu wengi wako wapi??
mbona ni wanausalama ndo wapp wengi??
acha mahaba kijana ,,au we ni wa mombasa??
Mitula alichofanya MziziMkavu ni ku copy habari na kuiweka hapa pamoja na kukupatieni chanzo chake kuwa ni bbcswahili.
Sasa unapomshutumu na kumtukana kuwa ana mahaba na labda ni wa "mombasa" utakua mzima kichwani kweli wewe?
 
Last edited by a moderator:
@lawmaina78 embu tupia kidogo alikua anasema nini huyu kiongozi kisiki!
He has beaten them at their own game! Damn!
 
Mitula alichofanya MziziMkavu ni ku copy habari na kuiweka hapa pamoja na kukupatieni chanzo chake kuwa ni bbcswahili.
Sasa unapomshutumu na kumtukana kuwa ana mahaba na labda ni wa "mombasa" utakua mzima kichwani kweli wewe?
Mkuu Nyamgluu Umemwambia Ukweli mtupu huyu mkuu.@Mitula inaonyesha hata huko shule alikwenda kufuta ujinga ili mradi aonekane kuwa amekwenda shule kumbe hajasoma kitu. Huyu Mkuu Mtula anapenda kulaumu pasipo na kuisoma habari yenyewe imetoka wapi? na nini chanzo chake analaumu kipumba pumba ahhhhhh ukiwa umesoma na kupasi ni kitu muhimu kuliko kusoma shule huku umefeli na unaonekane umesoma kumbe ulikuwa unakwenda na kurudi pasipo kusoma kitu ahhh jamani kazi kweli ipo.
 
Nimeona habari citizen, watu ni wengi hatari.
Museven kasema Africa inaendelea na mchakato wa kujitoa ICC.
 
Aisee Kenyatta anapendwa sana maana kapokelewa na umati mkubwa
 
Embu sikilizeni kichwa hicho! Kudaaadeki! Dah! Sisi lini tutapat kichwa hivi Mungu?
Sisi tuna suluhu ya matatizo yetu, sio kuruka nje kila siku kulamba ------ ya wazungu waje kutusaidia hapa!
 
ICC ni muhimu sana kwa Afrika. isingekuwa ICC Kenya uchaguzi uliopita ungekuwa ni damu pia - lakini wote wagombeaji walipata message kuwa kuna kubeba masuulia kwa uchochezi wa kuwagawa wananchi na kuleta machafuko na mauwaji ili mradi upate kiti. Hili ni fundisho hata kwa nchi zote za jirani kwa wale ambao wana tabia ya kutojali maisha ya wananchi wao.
 
Back
Top Bottom