Vifo Kariakoo vyafikia 29, zoezi la uokoaji lafikia tamati

Vifo Kariakoo vyafikia 29, zoezi la uokoaji lafikia tamati

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Idadi ya vifo vilivyotokana na kuporomoka kwa jengo la ghorofa, Kariakoo jijini Dar es Salaam vimefikia 29, baada ya miili mingine tisa kupatikana.

Jengo hilo liliporomoka asubuhi ya Jumamosi Novemba 16, 2024 na kusababisha vifo, majeruhi zaidi ya 80 na uharibifu wa mali za mamilioni ya fedha.

Soma, Pia: Live Updates Kuporomoka kwa Ghorofa Kariakoo Nov 16: Waziri Mkuu aunda Tume ya watu maalumu 21 leo Nov 22, 2024

Leo Jumanne, Novemba 26, 2024, Msemaji Mkuu wa Serikali, Thobias Makoba akizungumza na waandishi wa habari akiwa eneo hilo la jengo lilipoporomoka amesema miili hiyo tisa imepatikana wakati shughuli ya kuondoa kifusi ikiendelea.

Makoba ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari- Maelezo amesema shughuli ya uokozi imefikia tamati leo Jumanne Novemba 26.

 

Miili mingine tisa yapatikana Kariakoo, vifo vyafikia 29

Idadi ya vifo vilivyotokana na kuporomoka kwa jengo la ghorofa, Kariakoo jijini Dar es Salaam vimefikia 29, baada ya miili mingine tisa kupatikana.

Jengo hilo liliporomoka asubuhi ya Jumamosi Novemba 16, 2024 na kusababisha vifo, majeruhi zaidi ya 80 na uharibifu wa mali za mamilioni ya fedha.

Leo Jumanne, Novemba 26, 2024, Msemaji Mkuu wa Serikali, Thobias Makoba akizungumza na waandishi wa habari akiwa eneo hilo la jengo lilipoporomoka amesema miili hiyo tisa imepatikana wakati shughuli ya kuondoa kifusi ikiendelea.

Makoba ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari-Maelezo amesema shughuli ya uokozi imefikia tamati leo Jumanne Novemba 26.

Majengo mawili yachunguzwa

Majengo mawili yaliyopo pembezoni mwa ghorofa lililoporomoka Mtaa wa Mchikichi, yanaendelea kuchunguzwa, imeelezwa.

Wakati uchunguzi ukiendelea kwa majengo hayo, mengine yameruhusiwa kufunguliwa kuanzia saa nane mchana wa leo Novemba 26, 2024.

Jengo hilo la ghorofa nne lililoporomoka Novemba 16, 2024 limesababisha vifo vya watu 29 na wengine 88 kuokolewa.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Thobias Makoba akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 26 amesema baada ya kuhitimisha shughuli ya uokozi maduka yaliyokuwa yamefungwa yanaruhusiwa kuendelea na biashara.

Kuhusu usalama wa majengo mawili ya ghorofa yaliyo pembezoni mwa lililoporomoka, ambalo moja lilitumika kama njia ya kuwafikia watu walionasa, Makoba amesema yote yatachunguzwa na wataalamu na kujiridhisha kuhusu usalama wake.

Credits: Mwananchi Digital
 
Pole sana kwa wafiwa wote na majeruhi wapone haraka na kurudi kazini
Pongezi ziende kwa wote waliojitoa kwa hali na Mali kuwasaidia wahanga kuokoa na kutibu
Naamini uchunguzi utafanyika wa kina kujua kama Kuna jengo lingine lenye shida ili wateja na wauzaji wawe huru kuuza na kununua
Tanzania Moja lugha Moja daima mbele
 
Poleni sana wafiwa wote. Kupoteza ndugu na mali ni kitu kigumu sana kuelezea. But shit happens.

Kwani sisi ni watu wa kujifunza kitu? Vinginevyo ni kukaa kimya tu na kusubiri yajayo, Yakiwa heri basi na iwe heri. Yakiwa shari, hata kama ni ya kujitakia, pia tutapena pole maisha yaendelee
 
Tuwaone sasa wahusika wote waliosababisha hiyo ajali kutokea, wakifikishwa mahakamani ili haki ipatikane kwa marehemu na majeruhi.

Sijui sana, ila uzoefu unaonyesha imeenda hiyo 😂 😂 😂 😂 . Na kama kuna mengine yana shida, pia nayo imeenda hiyo😂😂😂😂
 
DAR ES SALAAM - Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Thobias Makoba, amesema serikali imekamilisha zoezi la uokozi katika jengo lililoporomoka Kariakoo Novemba 16.

Akitoa taarifa rasmi leo Novemba 26, Makoba amesema eneo la ajali sasa limekabidhiwa chini ya uangalizi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wakati taratibu za uchunguzi wa eneo hilo na maeneo mengine ya Kariakoo likiendelea
1732637067344.jpg
.
 
Dar es salaam

Zaidi ya watu 80 walipatikana wakiwa hai
Idadi ya waliokufa kutokana na kuporomoka kwa jengo la ghorofa katika soko kubwa la kibiashara Kariakoo, Dar es Salaam, imefikia watu 29 baada ya miili tisa kupatikana.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Thobias Makoba akizungumza na vyombo vya habari leo, amesema miili hiyo tisa imepatikana wakati wa shughuli za kuondoa kifusi.

Vilevile Makoba ametoa taarifa kuwa shughuli za uokozi zimefikia tamati leo Jumanne Novemba 26.

Jengo hilo liliporomoka asubuhi ya Jumanne Novemba 16, 2024 huku zaidi ya watu 80 wakiokolewa wakiwa hai.
 
Back
Top Bottom