🌐Utangulizi, Mafanikio katika sekta ya Afya katika kukabiliana na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi, mama na mtoto kumepelekea baadhi ya mataifa mengine ya Afrika kuja kujifunza nchini.
Hayo yalisemwa na katibu mkuu wizara ya Afya Dkt.John Jingu tarehe 22 Februari, 2024 jijini Dodoma
"Takwimu zinaonesha mwaka 2015 vifo vya watoto wachanga vilikuwa ni 556 kati ya vizazi hai laki 100,000 namba hizi zimeshuka kufikia vifo 104 kwa vizazi hai laki 100, 000." Alisema Dkt. Jingu
🌐Duniani kote
Takimwu za WHO kwa mwaka 2020 zinaonesha mwaka 2020 kilasiku zaidi ya wanawake 800 walikufa kutokana na changamoto zinazo epukika kipindi cha ujauzito na kujifungua.
Kifo cha mama kilitokea kila baada ya dakika mbili mwaka 2020.
🌐Kwa kutambua jitihada za Serikali kupitia wizara ya afya iliopelekea kupungua vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua, serikali bado inawajibu wa kuboresha huduma za Afya kwa wajawazito na watoto wachanga( siku 0-7), Ili kuweza kufikia malengo ya maendeleo endelevu ya millennia kuhusu afya ifikapo mwaka 2030 ya kuwa na raia wenye Afya Bora. kwa kufanya yafuatayo;
🌐kuboresha vituo vya afya na zahanati kwa kuhakisha upatikanaji wa huduma zote muhimu za Mama na mtoto, ikiwa zahanati na vituo vya afya ni sehemu ya msingi kwa huduma ya Mama na mtoto.
🌐kuongeza idadi ya wataalam wa afya wenye uwezo wa kutoa huduma stahiki kwa Mama na mtoto kwenye zahanati, vituo vya Afya na hospitali .Ili kuepukana na makosa madogo madogo ya uzembe ambayo madhara yake nikifo kwa mama na mtoto.
🌐kuandaa mkakati maalumu wa kutoa elimu kwa jamiii nzima ya umuhimu wa Mama mjamzito kuanza kliniki mapema na kuhudhuria kliniki kipindi chote cha ujauzito kama inavyo shauriwa na wataalam wa Afya.
🌐kuboresha maslahi ya wataalamu wa afya kuwa kama hamasa na kutambua umuhimu wa kazi na jitihada za kutoa huduma bora za afya.
🌐Kuboresha miundombinu kama barabara, Umeme na gari za kubebea wagonjwa (ambulance) ili kuhakikisha upatikanaji wa huduma muhimu kwa Mama na mtoto muda wote.
🌐Huduma zinazotolewa na wataalamu wa Afya kabla ya kujifungua, kipindi cha kujifungua na baada ya kujifungua husaidi kuokoa maisha ya Mama na mtoto.
Niwazi sasa kilammoja wetu anamchango wa kuhamasisha akina Mama kuhudhuria kliniki katika kipindi chote cha ujauzito na chakujifungua.
Upvote
6