Vifo vingi vinavyotokana na ajali nchini Tanzania ni kwa sababu ya ujinga na uzembe wa kutowakimbiza majeruhi hospitalini kwa haraka

Vifo vingi vinavyotokana na ajali nchini Tanzania ni kwa sababu ya ujinga na uzembe wa kutowakimbiza majeruhi hospitalini kwa haraka

Lord denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
15,819
Reaction score
33,255
Kati ya sehemu ambayo kusema kweli ni rahisi sana kufa baada ya kupata ajali basi tuseme ni nchini Tanzania.

Kwa uzoefu wangu mara nyingi ajali inapotokea nchini Tanzania ni mara chache sana watu wanashughulikia kuwakimbiza majeruhi hospitali kwa haraka. Watu huwa wanawatoa majeruhi na kuwalaza pembeni tu ya eneo la ajali na majeruhi hawa wamekuwa wanakaa muda mrefu bila kupata huduma ya kwanza hivyo kufariki!

Kituko zaidi ni ni polisi ambao hata wao wanapofikaga katika maeneo ya ajali hawahangaiki kuanza kusimamisha magari na kuomba kuwakimbiza majeruhi hospitali. Wanahangaikaga kuanza kupima na kupoteza muda tu!

Kuna haja ya mafunzo makubwa kufanywa kwa polisi na raia kuhusu huduma za uokozi na namna ya kuwahudumia kwa haraka au kuwapa msaada wa haraka majeruhi wa ajali ikiwemo kuwafikisha hospitalini.
 
Ni mambo ya kusikitisha sana lakini ndio ukweli wenyewe.

Kwanza ikitokea ajali, wenye magari binafsi huwa hawasimami kutoa msaada. Waokiaji wakuu ni bodaboda na bajaji. Hao watakuibia pia, lakini angalau wanasogea kukusaidia.

Baada ya hapo kama haujaumia sana basi utapakiwa kwenye bajaji akukimbize hospitali.

Kama umeumia sana basi watakulaza pembeni kisha utangojea kufariki. Yaani unakufa watu wamekuzunguka wanashika vichwa na kusikitika tu kwa kauli kama "mweee jamani, masikini.... "

Hatuna jeshi la uokoaji nchi hii; hatuna mafunzo ya huduma ya kwanza, yaani madereva wengi wa magari hawajui hata wafanye nini wakikuta sehemu kuna ajali!

Mbaya zaidi ni polisi, hawa ndio matatizo matupu, muda mwingine huwaletea usumbufu wa kipumbavu watu wanaojitolea kuokoa maisha. Yaani unampekeka majeruhi hospitali kisha mtu anakwambia sasa twende kituoni ili tukachukue maelezo. What the f*uck??
 
P3 imeshaniulia wanangu wa2. Kuna dokta nilinuwia kumoasua sema nikamuachia mungu tu. Kama angeweka huruma mbele, basi dogo angekuwa hai hadi leo
 
Mkuu Wakati mwingine ni ngumu! Fikiria Ajali imetokea porini mbali na vituo vya afya! Na hata ajali zinazotokea karibu na vituo afya inakuwa vigumu kuhudumia majeruhi kwa kukosa gari la ambulence.
Lakini kama ni gari limepata ajali na abiria wote wameumia kiasi cha kushindwa hata mmoja kushika simu na kupiga,majeruhi wanaweza kukaa masaa hawajapata huduma.
Kwa kweli ni changamoto.
 
..barabara zetu pia sio rafiki ktk masuala ya uokoaji. Zimejengwa kwa mbanano hali ambayo inaleta msongamano wakati wa ajali, na kufanya zoezi la uokoaji kuwa gumu.
 
Siyo kwamba ni mapenzi ya Mungu?
Hakuna mapenzi ya Mungu. Ni uzembe na ujinga. Kuna clip ilikuwa inasambaa Weekend hii ya ajali eneo la Mbande Dodoma itazame utaona mwenyewe.

Kuna uzembe mkubwa sana na kutojali sana kwenye suala la uokoaji hapa Tanzania
 
Kupima na maswali ni baadae, majeruhi wachukuliwe chap chap.
Kwa Tanzania uzoefu wangu nimeona majeruhi wanakaaga bila kukimbizwa hospitali kuanzia dk 40 hadi saa moja na nusu.

Muda huu ni wa kutosha sana kuokoa uhai wa mtu endapo wangekuwa wanachukuliwa haraka na kukimbizwa hospitali
 
Leo katika uokoaji wa majeruhi wa kuanguka kwa jengo la Kariakoo vifaa vya uokoaji vimefika mchana wakati majeruhi walikwama kwenye vifusi tangu asubuhi
 
Back
Top Bottom