Luqman mohamedy
JF-Expert Member
- Jul 24, 2016
- 899
- 1,231
Ukiongelea haya mambo utajua ni utani,ila ukosefu wa hivi vitu ndio sababu namba 1 ya vifo vingi kwenye mkanyagano katika mikusanyiko na vifo kupitia magonjwa ya ghafla majumbani
[emoji117]Kwa bahati mbaya watu wanadhani hivi vitu anapaswa kujua muhudumu wa afya tu,watu wa huduma ya kwanza au kikosi cha zima moto,la hasha basic life support anapaswa kujua kila mtu kabla ya kumaliza elimu ya msingi,haihitaji degree ya udaktari.
Basic life support ni zipi??
(1)Kufika kwenye tukio na kuangalia madhara aliyoyapata majeruhi kisha kuangalia kama majeruhi ana muitikio.
(2)Cardiopulmonary resuscitation (CPR).
[emoji117]Punde baada ya kusikia tukio lenye kuweza kusababisha madhara kama ajali , kukanyaganana mtu kudondoka ghafla watu waliokaribu na tukio wanapaswa kusogea karibu na tukio na kuangalia madhara waliyopata wahanga kama kuvunjika,kuungua na ikiwa wamevunjika sehemu zisizowazuia kubebwa (ie majeruhi wa kuvunjika uti wa mgongo anapaswa kubwa na wataalamu) basi unawasogeza mbali na tukio na kuanza step ya 2.
[emoji117]Kama majeruhi hana muitikio wowote pigia ambulance ije.
[emoji117]CPR-Kabla ya kuanza kufanya CPR yakupasa ukague njia ya hewa kujua kama mhanga anapumua,
Utajuaje mtu anapumua?
•Njia za kujua mtu anapumua ni kuweza kutoa sauti/kulia kwa kuugulia maumivu,sababu huwezi kulia kama njia ya hewa imeziba.
•Sogeza sikio karibu na pua uone kama kuna hewa yeyote inatoka na kuingia.
•Angalia kama kifua kinapanda na kushuka.
[emoji3516]Kama hivyo vyote havijatokea,haraka sana funua kinywa cha majeruhi kisha angalia kama ulimi umeziba njia ya hewa uutoe au kama kuna kitu chochote kimekwama jaribu kukitoa kwa kumpiga mkongoni huku umemuinamisha na kutingisha kichwa.
[emoji117]Step ya 2 weka mikono yako katikati ya kifua ukiweka mmoja juu ya mwingine kisha anza kukandamiza kifua mara 30,huku kila mara moja ikipishana sekunde mbili
[emoji117]Kwa kila mikandamizo mitano,mpulizie majeruhi hewa mara 2
Ikiwa hatarespond basi piga simu haraka kwa watu wa huduma ya kwanza.
[emoji1690]Kuhusu paramedics au wahudumu wa huduma ya kwanza linapotokea janga lolote majumbani au mtaani kwa Tanzania hichi kitu hakijatiliwa mkazo.
Ukiuliza ni watanzania wangapi wanajua namba za kupiga ikiwa kutatokea janga au mtu kadondoka ghafla basi ni 2 kati ya 100.
[emoji117]Kitu chaajabu mtu akidondoka mtaani ni kumshangaa na kuhisi mlevi hakuna anayejua namna ya kuokoa maisha yake.
Elimu juu ya kutumia fire extinguisher moto unapitokea pia asilimia 90% ya wananchi hawajui,wanajua ni kazi ya watu wa kikosi cha zima moto tu,hali inayopelekea kushindwa kudhibiti moto mdogo mpaka unasababisha madhara makubwa.
[emoji117]Huduma ya kwanza kwa majeruhi wa majanga mbalimbali;
Lazima kuwepo na taasisi za kiserikali zinazozunguka mtaani kutoa elimu juu ya huduma ya kwanza kama zilivyo taasisi nyingone za kiserikali na zisizo za kiserikali zinavyotoa elimu nyingine za afya.

Upvote
0