Vifo vya watoto hawa 2 vichunguzwe!


Ngabu....dont worry coz monkeys do the fluting ...... and that speaks louder than big boxer.
 

YOU MADE IT VERY CLEAR:
Man, I've had it up to here. We are a joke, beyond a joke when it comes to the rule of law. Hivi wakati wa mkoloni yalikuwepo kweli haya? Nyie vidingi humu ndani hebu tuambieni?

I really don't care what y'all think of me. None of you know me like that anyway. To hell with political correctness. Miafrika Ndivyo Tulivyo. Deal with it
 

This shows only how far we are joining the Animal Kingdom! versus Human Kingdom
 
Bongolander, kimantiki si sahihi kujichukulia sheria mkononi.Mbaya zaidi kama walivyochangia wengine hapo juu watanzania ndivyo tulivyo kwani mtaani watu huchoma wezi moto kwa kuwavisha matairi bila ya huruma yoyote badala ya kuacha sheria ichukue mkondo wake.Wakati umefika wananchi tuachane na upotovu huu.Nakubaliana na Nyani Ngabu ya kwamba "Miafrika Ndivyo Tulivyo"
 

Huu ndiyo uandishi ambao Kuhani anaulani kila siku. Inaelekea kuna utata kuhusu kifo cha hao watoto. Polisi wanadai ni mob justice wakati wazazi/walezi wanasema hapana, haikuwa hivyo. Mmoja wao anadai kuwa mtoto wake aliuawa na askari. Polisi wanadaiwa kuwashurutisha wazazi hao waandike uongo maana wao ( wanavyodai) hawakushuhudia vifo vya wanao. Hizi ni shutuma nzito sana hasa ukizangatia yaliyowapati wale wachimbaji wa madini. Lakini badala ya kutafuta ukweli wa ishu yenyewe, wengi wetu (hata wale wanaowatetea hao watoto) tumeisha wahukumu marehemu kuwa walikuwa vibaka!

Juhudi za mwandishi kutafuta ukweli wa mambo inaelekea zilikoma pale alipompigia simu Kova na kuambiwa kuwa yuko likizo. Kwa nini hakuenda ofisini kwake ambako bila shaka angemkuta anayekaimu hiyo nafasi wakati mheshimiwa yuko likizo? Je alienda sehemu ambapo panadaiwa hilo tukio lilitokea na kjihakikisha kuwa kuna ukweli ndani yake? Alienda maeneo ( si kupiga simu) ya hoteli ya Legho kufuatilia shutuma za mjomba wa Emmanuel?

Hapana, hii habari inatakiwa ifikishwe kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani. Panatakiwa uchunguzi wa dhati ufanyike ili kuonyesha kuwa tabia za kujichukulia sheria mkononi ( kwa wananchi na wale waliopewa dhamana ya kulinda usalama wao) hazina nafasi katika jamii yetu. Uchunguzi ufanyike kujua kama ni kweli hao polisi walitaka kuwalazimisha wazazi waseme uongo! Ikionekana kuwa ni kweli, wachukuliwe hatua.

Huu ni wakati ambapo ofisi hiyo inabidi kuwahakikishia kwa vitendo wananchi wake kuwa wako makini katika kuhakikisha usalama wao. Wawakumbushe askari walio chini yake kuwa wao ndiyo wanaopaswa kuwakamata wahalifu na si kutegemea wananchi wawafanyie kazi hiyo. Inabidi wafanye jitihada za dhati kuwaelimisha wananchi kuhusu haki zao maana wengi wanaogopa kushindana na serikali kama alivyosema mzazi wa Bakari!

Yaliyompata Zion Train yamekuwa ni kawaida. Polisi wanakaa kwenye polisi posti na kutegemea wananchi wawakamatie wahalifu na kuwaletea! Na wakifanya hivyo, wao wanachangamkia dili!

Na, Chuma. Mzee Mwanakijiji hakuileta hii habari hapa kwa vile tu mmoja wa marehemu anaitwa Emmanuel. Mbona mwingine anaitwa Bakari? Mbona huyo Emmanuel mjomba wake ambae ndiye mlezi wake anaitwa Khalfan? Usitake, Mkuu, kutupeleka ambako hakustahili!

Amandla........
 
FM... unajua umeleta the right attitude:

a. Mwandishi anasema hivi kwenye kifungu cha tatu
"Tukio hilo linadaiwa kufanyika usiku wa Jumamosi katika eneo la Legho, Barabara ya Shekilango na watoto hao kupigwa na watu wenye hasira hadi kufa kwa kutumia silaha mbalimbali yakiwamo mawe na fimbo."


Kabla ya hapo hata hivyo ametangaza hivi kwa uhakika:

Watoto wawili wa Shule ya Msingi Manzese jijini Dar es Salaam wameuawa kikatili na watu wenye hasira kwa tuhuma za kuiba vioo viwili vya pembeni mwa gari.

Sasa kati ya kauli hizo mbili jambo moja mwandishi wetu halisemi: Alijuaje kuwa watoto hao wameuawa na watu wenye hasira; na anaposema "inadaiwa" ni kina nani wametoa madai hayo wakati Polisi hawajasema lolote na wazazi wanakanusha?

Cha kushangaza hapo chini ananukuu maelezo ya Mganga kuwa "waliowaleta walisema walipigwa na watu wenye hasira kali" Sasa tunajiuliza "Waliowaleta" ni kina nani? (ni lazima watakuwa watu walioshuhudia tukio hilo au walioshiriki katika tukio hilo)

Nadhani I got something to do early this morning!!! Hakuna ufisadi unaoniumiza kama haya ya vifo vya watoto!!!! grrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
 
Mzee Mwanakijiji!
Watoto, wakina mama wazee na wenye ulemavu ( wenye matatizo ya akili, albinoz n.k.) ni expendables katika jamii yetu. Wakiuawa hakuna anaetoa machozi ili mradi tuhakikishiwe kuwa wao ni vibaka au wanga. Ni hivi karibuni tumeanza kuona aibu juu ya albinoz kwa sababu tumeanikwa duniani kote! Iko kazi.

Amandla..............
 
Police hunt lynch-mob in slaying of 2 pupils




THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

IT is a tragic story, which has left many Dar es Salaam residents reeling in shock and horror. And now, police say they have launched a manhunt to find the lynch-mob behind the deaths of two primary school pupils at the weekend.

The Acting Commander of the Dar es Salaam Special Police Zone, Assistant Commissioner of Police (ACP) Evarist Mangala, told THISDAY that a formal investigation was underway into the brutal slaying of pupils from Manzese Primary School.

Emmanuel Malobya (16), a Standard Six pupil, and 14-year-old Bakari Ramadhani, a Standard Five pupil, were brutally murdered when a lynch mob dispensed its own form of justice on the pupils at the Sinza Legho suburb on Saturday.

In a bizarre case of mistaken identity, the two pupils were suspected to have stolen side mirrors from a car and ended up being lynched by a mob.

Police have not made any arrests in connection with the incident that has sent shock-waves throughout the country.

Police officials say they were getting little cooperation from possible eyewitnesses at the Dar es Salaam suburb where the grisly incident occurred.

’’You know this was a mob justice and no one has volunteered to give us any information yet ... we shall inform the public when we conclude our investigation,’’ said ACP Mangala.

The police chief warned members of the public against taking part in mob justices, saying such actions were against the law.

’’People should report any incident of crime to the police and avoid taking the law into their own hands. It is illegal to punish someone just because he or she has been suspected of committing a crime. The police should be the ones to act,’’ he insisted.

Parents, teachers and fellow students of the slain pupils have vented their anger at the lynch mob and are calling for a swift investigation.

The Manzese Primary School Head teacher, Joseph Said, told reporters that both Emmanuel and Bakari had no history of theft and were model students.

He demanded an immediate police inquiry into the brutal murders of the two primary school pupils.

’’I urge the police to investigate this matter fully and ensure those behind this heinous act are brought to to justice,’’ said the boys’ teacher.

’’Emmanuel was an orphan boy brought to Dar es Salaam by his uncle so he could have a chance at education, but his life was tragically ended,’’ a neighbour told reporters.

Eyewitnesses said the boys had cried out in vain for help while a mob unleashed their attack on them.
 
Tusilaumu watu wenye hasira, hapa wa kulaumiwa ni system nzima ya serikali. Kuna kitu tunaita confidence of the people to their governing organs. Watanzania hawana tena Imani na serikali, na vyombo vya dola. Haya mambo hayakuanzia leo ya watu kuchukua sheria mikononi, ni matokeo ya serikali corrupt na vyombo vyake vyote, yaani mimi hapa mchawi mkuu ni Rushwa, rushwa, rushwa, rushwa narudia rushwa. Nitachambua kama ifuatavyo

1. Miaka ya 19XX, wananchi wanamkamata mtu akiiba na vidhibiti vyake na kumpeleka polisi ili apelekwe mahamani na hatimaye kufungwa kwa kuwa ushahudi upo

2. Wananchi hawa wakiondoka kituoni na kumuacha mtuhumiwa na polisi, then polisi wanamwambia wewe utafungwa huna ndugu?, then ndugu wa mtuhumiwa wanakuja na kuwapatia pesa polisi then polisi wanamwachia mtuhumiwa na anarudi mtaani kwa nguvu zote

3. Wananchi hawa wanashangaa vipi huyu kaachiwa? na ushahidi upo? kafanya nini polisi? kafanya nini mahakamani? maswali haya yanakaa vichwani mwa wananchi bila majibu toka ama polisi au mahakamani.

4. Pole pole wananchi wanaanza kupoteza imani na vyombo vya dola, na kuona kuwa havipo kwa ajili ya haki. Utamaduni huu wa dili kati ya polisi na mahakama na watuhumiwa ambao ulikuwa ni kwa siri sasa unaanza kufanywa wa wazi, wananchi wanaanza kusema polisi kuingia ni bure kutoka hela, na wananchi wanaombwa pesa kwa lazima sasa na inakuwa siyo kama zamani ( wanaita chai, soda, maji ya baridi, taulo, chochote, kidogodogo etc) wanakwambia wazi leta Hela.

5. Huku wakuu wa serikali na wakubwa wa vyombo hivi wakifumbia macho mambo haya yanayofanywa na walio chini yao kwa kisingizio mishahara haiwatoshi, wananchi nao wanakuwa na mawazo mapya kabisa kuwa bila hela siwezi kupata haki yangu popote pale. Imani hii inazaa utamaduni mpya "On your own" kivyakovyako hapendwi mtu hapa.

6. Yule kibaka aliyakamatwa mwanzo na ushahidi anakamatwa tena kaiba na ushahidi upo, ila wananchi wanasema, huyu tukimpeleka polisi ataachiwa, na akiachiwa atakuja kutusumbua tena sisi na si polisi, dawa yake tumhukumu wenyewe wanampiga mawe na kwa bahati polisi wanawahi na kuja kumuokoa kabla hajauwawa na kuwalaumu wananchi kuwa mbona hawakumaliza kazi kabisa?. Wakifika polisi wanachukua hela tena na kumuachia mtu huyu anarudi uraiani na safari hii anarudi na hasira ya kulipa kisasi kwa waliompiga, anafanikiwa kuwapiga nondo wawili na kuwaua kati ya wale waliompiga mwanzo. Wananchi wanajua kuwa aliyefanya hii kazi ni mmbaya wao lakini hawana pa kumpeleka kwani ataachiwa.

7. Mara ya tatu kibaka huyu anaiba tena na wanamkamata na ushahidi ila wanasema this time tumuondoe kabisa maana akipona anaondoa wengine wanachofanya ni kumuwahisha na kumuua, polisi wanakuja kuchukua mwili na kuwapa hongera wananchi kwa kazi nzuri waliyoifanya maana mtu huyu hasikii kabisa. Kumbuka hapo hakamtwi mtu yeyote kwa kujichukulia sheria mikononi. Wananchi wanaona walilofanya ni sahihi kabisa na mchezo unakuwa ni huo

8. Mchezo huu unaendelea na kuleta madhara makubwa kwani mtu akikupigia kelele tu wewe ni mwizi hupewi muda wa kujitetea ni moja kwa moja unapata hukumu ya kifo.

Hitmisho: Haya tunayoyaona leo ni matokeo ya mbegu tulizopanda miaka mingi sana ambazi zinachochewa na rushwa ya leo, hebu tuanze kufuata sheria, mtu kaiba polisi anaitwa na mtuhumiwa anapelekwa mahakani na kama kuna ushahidi anapata adhabu, na kwa wananchi wanaojichukulia sheria tuwe tuwa identify hata kumi tu na kuwapa adhabu stahili, watu watakuwa makini. Ila je hilo linawezekana?, "Vita ya ufisadi"
 
Last edited:
Wananchi nao wanastahili kulaumiwa. Vitendo viovu tunavyovifanya dhidi ya wenzetu ( mauaji ya bibi vizee, mauaji ya Albinoz, uchomaji moto wa wale tunaodhani ni vibaka n.k.) ni dalili ya jamii yenye matatizo. Uwezo wa jamii yetu wa kuvumilia na kukubali vitendo vya kikatili (violent acts) hauelezeki. Ni mara ngapi magazeti yamechapisha picha za haya mauaji kwenye front page ( nchi nyingine zingefichwa ndani na kuambatana na onyo) na kwenye picha utaona watoto wadogo wakiwa miongoni mwa wanaoangalia hizo maiti? Angalia video na dvd tunazoangalia na watoto wetu? Nyingi zina glorify vitendo vya kinyama dhidi ya binadamu wengine lakini hatuoni tatizo kuziangalia na watoto wetu! Lakini tunachachamaa kweli tukiona tangazo la sanitary pad! Tunachachamaa tukiona watu wanaonyesha mapenzi kwa kubusiana! watu wakibusiana tuwakinga macho watoto wetu wasione. Tunapandisha munkhari kuhusu mavazi ya binti zetu n.k! Wakati vibaka wana terrorise maeneo mengi ya miji zetu, polisi wetu wanawavalia njuga makahaba!

Hapana, Mkuu. Ingawa nakubaliana nawe kuwa system yetu ina matatizo makubwa lakini hata sisi hatuwezi kukwepa lawama. Wote tumo kwenye hilo.

Amandla.........
 
Mkuu FM nakubaliana nawe kwenye hii issue ya jamii kupaswa kulaumiwa. Ninashangaa sana kama majuzi ambapo ippmedia wameweka picha ya mbuzi anayechinjwa kwenye ukurasa wa mbele. Naelewa huku majuu wanasema "sex sells"; je kwetu wanahabari wanafikiri kuwa "violence sells"?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…