Vifo vya Watuhumiwa Mikononi mwa Polisi, nini kifanyike ili mambo yakae sawa?

Vifo vya Watuhumiwa Mikononi mwa Polisi, nini kifanyike ili mambo yakae sawa?

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Hivi karibu kumetokea matukio yakihusisha watuhumiwa kupotea maisha mikononi mwa vyombo vya usalama. Mkoani Morogoro Askari wawili wanashikiliwa kwa tuhuma za mauaji ya Hamis Hassan (30) Mkazi wa Mvuha, Jeshi la Polisi limesema marehemu aliuawa kwa kufyatuliwa risasi Mei 31, 2022.

Jijini Arusha, kifo cha Kibabu Msese (26) aliyekuwa fundi magari kilichotokea Mei 31, 2022 akiwa mikononi mwa Polisi baada ya kushikiliwa Mei 24, 2022 pia kimezua hataruki, Jeshi la Polisi limesema mtuhumiwa aliugua ghafla.

Matukio yote hayo mamlaka za usalama kwa maana makamanda wa jeshi wa mikoa wamekiri kuwa uchunguzi unaendelea ili kujua zaidi kuhusu kilichopo nyuma ya pazia kama kipo.

Unadhani nini kifanyike kuboresha elimu ya usalama wa raia na mali zao?


================

Askari wawili washikiliwa kwa mauaji ya Mtuhumiwa

Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro linawashikilia askari wawili wa Kituo cha Polisi Mvuha kwa tuhuma za kusababisha mauaji ya mkazi wa Mvuha Wilaya ya Morogoro, Hamis Hassan (30) maarufu Ng’ombe, baada ya kumpiga risasi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro (RPC), Fortunatus Muslim ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tukio hilo la mauaji lilitokea Mei 31 mwaka huu katika Kijiji cha Bwila Juu Kata ya Selembala wilayani Morogoro.

==============

 
Sijui wao, mi ukiua ndugu yangu lazima nikutafute personal tumalizana hata kama itapita miaka 10 nitakuwinda tu.


Nikifanikiwa kkupata tutakaa chini tunaagiza chai ya maziwa na mihogo tunasimuliana ilikuaje basi tunatawanyika zetu.!!!
 
Back
Top Bottom