Vifurushi 21 vya msaada wa Jack Ma 'havikufika' Kenya

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mamlaka nchini Kenya imekiri kwamba mchango muhimu katika vita dhidi ya Covid-19 kutoka kwa bilionea wa China Jack Ma haikuwasili nchini.

Naibu wa waziri wa uchukuzi wa, Chris Obure amefichua kuwa vifurushi 21 vilivyokuwa na vifaa vya matibabu vilivyotolewa na wakfu wa Jack Ma mwezi Machi kama msaada wa kukabiliana na Covid 19 haikufika Kenya.

Bwana Obure alisema hayo siku ya Alhamisi mbele ya kamati ya bunge ya afya japo hakudokeza ni vifaa vya aina gani vilikuwa ndani ya vifurushi hivyo.

Aliongeza kuwa vifaa hivyo havikuwahi kuwawasili nchini kutoka Ethiopia ambako misaada ya Jack Ma katika eneo hilo ilitumwa kwa ajili ya kusambazwa katika nchi zingine.

Wizara ya uchukuzi iligundua kuwa vifurushi 21 havikuwepo baada ya kuthibitisha hilo katika stakabadhi za kuegesha kutoka China.‘’Binafsi niliongea na maafisa wakuu wa Wizara ya Afya na walinithibitishia kuwa wanafuatilia suala hilo’’ alisema bwana Obure.

Kumekuwa na madai kwamba misaada ya Covid-19, ikiwemo ile kutoka kwa Jack Ma ilitumiwa vibaya au kutoweka katika njia za kutatanisha.
 

Attachments

  • 1599225493434.gif
    42 bytes · Views: 2
Wakenya mazazwa bado wanamini mambo ya corona.

Ova
 
mara vifaa wameuzia Tanzania.. sasa wanasema vifaa vilibaki Ethiopia! Hivyo Ethiopia ndio waliwabania wakabaki navyo au? Mbona Jubilee ni washenzi hivi? Yani jubilee inataka kugombanisha wakenya wote na nchi zinazo wazunguka kisa tu sera mbovu na wizi na ufisadi wa uhuru?
 
Ila baadhi ya wa Waenya ni wapuuzi sasa kama havikufika Kenya iweje yule mwandishi wa habari akasema ktk uchunguz wake aligundua baadhi ya vifaa tiba vya kupambana na corona kuuzwa Tz?

Na nilikuwa nasikioiza BBc swahili online ile kamati mmoja kati ya mjumbe akadai eti huuenda mzigo ulipelekwa Tz. Nchi inachekeshaaaa
 
Aisee wakenya bwana nasikia eti hizo vifaa waliiuzia Tanzania na ndivyo vimesaidia kuitokomeza corona hapa Bongo.
 
Mashati hatoki anabidili katiba soon!

Ah hiyo haiwezekani, watamnywa supu mzima mzima akiona. BBI yenyewe wamemgomea ndio katiba ataweza kuigusa?

Hahah ila katiba ya kucopy na kupaste nuksi kweli, yani hata hawajamaliza kuisoma na kuielewa tayari wanataka kuibadilisha. Mashati fala sana, akiona katiba za nchi nyingine zinazomzunguka na akiangalia hiyo katiba yao anawaza tu akitoka madarakani atakuwa salama kweli? Hahaha jamaa yuko katika hali mbaya sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…