VIFURUSHI VYA MB: kwanini hivi Vifurushi vya wiki na mwezi kwenye mitandao ya simu vinakosa uhalisia wa muda?

ezekeo

Member
Joined
Aug 27, 2022
Posts
63
Reaction score
158
Hivi Vifurushi vya wiki na mwezi kwa sehemu kubwa kipindi hiki vinakosa uhalisia yaani ujazo wake hauna sifa za muda tajwa.

Haiwezekani kifurushi cha wiki kiishe kabla hata ya masaa 12 au kikijitahidi sana yaani mtumiaji akijibana basi ni ndani ya masaa 24 kinaisha na wengi wetu imekuwa ni kila siku tunajiunga vifurushi vya wiki.

Hiki cha mwezi kutoboa nacho siku tano ni bahati kwa sehemu kubwa ni siku mbili au tatu kimekata, sijajua shida huwa ipo wapi hata Kama ni matumizi ya mtu binafsi kwanini sasa hivi data ziwe zinaisha haraka kwa matumizi yaleyale ya kipindi cha nyuma(kabla ya malalamiko) ambapo data zilidumu na uhalisia wa kifurushi uhisika ulionekana?

Ushauri wangu ni kwamba hivi Vifurushi ipewe majina mengine halafu viletwe vifurushi vyenye sifa tajwa huku mamlaka ya mawasiliano ikitusaidia kuangalia uhalisia wake...

Hizi story za kuambiwa background apps kuwa ndio zinamaliza mb haraka tofauti na matumizi ya mhusika naona zimekuwa kama kichaka cha kuhalalisha wizi wa vifurushi vyetu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…