Vifurushi vyetu vinapotea shirika la posta

senzighe

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2012
Posts
2,108
Reaction score
1,666
Kuna mazingira ambayo hayaeleweki katika shirika la Posta hapa Dar es salaam.Kutokana na maendeleo yaliyopo sasa hivi ya kiteknolojia, Kuna bidhaa ambazo tunanunua kwa njia ya mitandao kutoka sehemu mbalimbali duniani.
Baada ya kukamolisha taratibu zote za kimalipo,bidhaa inatumwa huko ilipotoka na unapewa 'tracking number' ya kifurushi chako.Unafuatilia 'online' kwa mtiririko mpaka mzigo unaingia Dar es salaam.

Tatizo linaanzia hapa Dar es salaam. Unasubiri kama utapewa taarifa yoyote toka Poata kutokana na anwani uliyoweka lakini hupati taarifa yoyote.Sasa unapofuatilia pale Posta makao makuu ukiwa na nakala ya vithibitisho vyote unapewa majibu yenye utata.Mara tracking system yao mbovu mara mzigo haujafika.

Wale vijana waliopo 'Customer care' ni kama wamelazimishwa kufanya ile kazi kwani wanarushiana mpira .Mmoja anmwambia mwenzake mtizamie wewe naye anajibu ana mambo mengi labda aende kwa bosi moja kwa moja.

Inafikia hatua mtu unakata tamaa na unaachia tu kifurishi chako kinaishia hukohuko Posta na hatujui baada ya hapo kinapelekwa kwa nani.
Tunawaomba wenye dhamana wasaidie utatuzi wa hili jambo kwani tunapoteza imani na hili shirika,
 
Siku nyingine ukiagiza mzigo usitumie kampuni ya watu wasiojua customer care,wasiojitambua,wasiojua maumivu ya mtu kupoteza mzigo wake,wasiojali hasara ya mteja,wapowapo tu bora liende.
 
Shirika la posta ni shirika la serikali hivyo sie walipa kodi ndio tunawalipa wakizingua na kuleta uhuni inabidi turuke nao babu.
 
Back
Top Bottom