Vigezo gani hutumika kupanga na kuamua kiasi cha mahari ya mwanamke anayechumbiwa?

Vigezo gani hutumika kupanga na kuamua kiasi cha mahari ya mwanamke anayechumbiwa?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Vigezo gani huwa vinatumika kupanga na kuamua kiasi cha thamani ya mahari ya mwanamke ambacho mwanaume anatakiwa aitoe kwa upande wa familia ya wazazi wa mwanamke?
 
Hivi zama hizi za wanawake micharuko na wasaliti kwenye ndoa kuna umuhimu wa kutoa mahari wakati hata ukitoa ndoa haidumu?
 
Vigezo gani huwa vinatumika kupanga na kuamua kiasi cha thamani ya mahari ya mwanamke ambacho mwanaume anatakiwa aitoe kwa upande wa familia ya wazazi wa mwanamke?
Hakuna vigezo maalumu ndio maana kiwango cha mahari hakifanani
 
•Elimu - Binti mwenye elimu ya juu hupewa mahari kubwa.

•Umri - Binti mdogo chini ya 25 mahali yake huwa kubwa tofauti na binti wa zaidi ya miaka30.

•Tabia na malezi ya binti- Tabia nzuri na maadili huongeza thamani.

•Hadhi ya familia - Familia yenye hadhi ya juu inaweza kudai mahari kubwa tofauti na familia za hali ya mtu.

•Kipato cha kijana - Mahari huendana na uwezo wa kifedha wa anayeoa.

•Utamaduni wa kabila - Kila kabila lina viwango vyake.

•Makubaliano ya familia - Familia zote mbili hujadiliana na kukubaliana ili kusaidiana mara nyingine.

•Hali ya binti - Ikiwa binti ni bikira mahali itakua juu tofauti na binti aliyepitiwa tayari au binti mwenye watoto hupunguza kiwango cha mahari.

•Dini - Tamaduni za kiislamu, waisilamu waaminifu, binti zao hujipangia mahali mwenyewe.

Kuna yule jamaa Dubai alipangiwaga Followers Milioni moja Tiktok 🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom