Vigezo na masharti ya kushiriki katika Stories of Change 2023

JamiiForums

JF Official Account
Joined
Nov 9, 2006
Posts
6,229
Reaction score
5,285
  1. Mshiriki lazima awe mwanachama wa JamiiForums, ambapo anaweza kujisajili kwa kiunganishi hiki; Register
  2. Mshiriki anaweza kutumia jina la kubuni ‘pseudonym’.
  3. Mshiriki atatakiwa kutaja jina halisi endapo ataibuka mshindi.
  4. Mshiriki anatakiwa kutayarisha andiko ambalo linachochea mabadiliko kuhusu Uwajibikaji au Utawala bora katika nyanja mbalimbali. Andiko linaweza kuwa Habari, taarifa, maoni, uchambuzi au uchunguzi.
  5. Andiko liwe kwa lugha ya Kiswahili lenye maneno yasiyopungua 700 na yasiyozidi 1000.
  6. Andiko lisiwe limewahi kuchapishwa sehemu nyingine yoyote (Plagiarism). Aidha lisiwe tafsiri ya andiko lililochapishwa sehemu nyingine kwa lugha tofauti.
  7. Hakikisha unachapisha andiko lako kwenye Jukwaa la Stories of Change, ukichapisha katika majukwaa mengine halitazingatiwa.
  8. Usiweke andiko kama attachment (Word/pdf).
  9. Matumizi ya picha au video yanaruhusiwa ili kushibisha andiko. Endapo picha na video sio za mshiriki, atalazimika kutaja chanzo.
  10. Unaweza kuchapisha andiko Zaidi ya moja.
  11. Andiko lisiwe na sehemu ya mwendelezo, mathalani, Sehemu ya I, Sehemu ya II.
  12. Kichwa cha habari kisipungue maneno manne yanayoeleweka.
  13. Watendaji wa JamiiForums na ndugu zao wa karibu hawaruhusiwi kushiriki kwenye shindano hili.
Aidha

Soma SoC03 - Namna ya kuweka andiko lako ndani ya jukwaa la Stories of Change 2023

na SoC03 - Jinsi ya kujisajili kuwa mwanachama wa Jamiiforums.com
 
Upvote 90
Bahati njema kwa kila atakaye shiriki
 
habari nime register apo nimeambiwa nitapata ujumbe kwenye Email ndo nasubiri sijui saa ngapi
 
ok sawa
 
Hili shindano la awamu hii halina amsha amsha kabisa kama mwaka Jana & juzi
 
Tupieni jicho hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…