Vigezo vya kuomba chuo under NACTE kozi ya Afya ni uwe umemaliza Form Four na umefaulu masomo haya kuanzia ufaulu wa alama D, (physics, Chemistry, Biology, Mathematics, na English) .
Ukiomba chuo ambacho kipo under Nacte Cheti cha Form six kinakua kama Additional requirements. Wenyewe wanahitaji cheti cha form 4
NB: Nacte kuna ushindani mkubwa sana , namaanisha kupata nafasi katika vyuo vya serikali. Ufaulu wa juu , utakusaidia katika ushindani wa kupata nafasi . Maana wanaoomba ni wengi sana na karibia wote wana vigezo vya kuchaguliwa hiyo kozi.
Kuna ishu umesema ya ukiwa umemaliza form 6 na umefaulu kama wewe kua ,je unaweza kusoma 2yrs diploma. Kwa upande wa kozi za afya jibu ni HAPANA , hasa kwa hiyo Clinical medicine uliyoitolea mfano.
ILA kwa kozi nyengine tofauti na afya inawezekana . Mfano Diploma in Science and Laboratory Technology utasoma miaka miwili tu.
Na hapo ndipo cheti chako cha form six kitakua first priority
Nafikiri jibu langu litakua limekupa mwanga kiasi . Au pa kuanzia.