Vigezo vya kumpa mtu uprofesa wana jf!

Mpigamsuli

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2012
Posts
3,885
Reaction score
582
Swali langu wana jf ni kwamba ni vigezo hani hasa vya msingi hutumika kumpa mtu uprofesa ni kugundua vitu au ni ni ni ?
 
sifa kubwa za kuukwa U-professor haraka ni 1) kuwa mganga wa dawa za kienyeji ;2) uwe na uwezo mkubwa wa kulaghai watu ; 3) Baada ya ramli lazima uwe unaweka sharti la kuwataka wateja wakuletee majogoo na ma-beberu weusi. na mwisho 4) kwenye bango lako la matangazo neno "mganga kutoka sumbawanga au mlingotini" lisikosekane.
 
Wana jf! Mbona hamleti majibu ya hili au ni mabongolala ?
 

kama hujuwi ni bora ufunge bakuli lako watu wanauliza maswali ya msingi wewe unaleta kamasi zako zilizojaa kichwani kwako
 
kama hujuwi ni bora ufunge bakuli lako watu wanauliza maswali ya msingi wewe unaleta kamasi zako zilizojaa kichwani kwako
saafi majutomperungu bora umeliona hilo cha msingi ni kumuacha huyo bongolala bin kilaza by mpogamsuli
 
kwanza kabisa Uprofessor sio daraja la Elimu ( ninaposema sio daraja la elimu namaanisha kuwa hausomewi), ila ni ngazi ya utumishi hata kwenye academic institution, ngazi ya kwanza huwa ni Tutorial assistant, inafuatia Assistant lecturer, Lecturer, Seniior Lecturer, Associate Professor na mwisho kabisa ni Full Professor. Sasa katika vyuo vyetu vikuu kuna waraka unaitwa "UP THE LADDER", waraka huu unaeleza ni jinsi gani mtu anaweza kupanda ngazi moja kwenda nyingine, lakini kwa ufupi tu ni kuwa Kuwa Professor ( boith associate and full) ni lazima kwanza muhusika awe na degree tatu yaani Bachelor, Masters na PhD,na kupanda ngazi moja kwenda nyinge ni lazima muhusika kwanza awe ametimiza miaka mitatu katika post yake ya awali, mfano ili uwe Associate professor kigezo cha kwanza ni lazima uwe Senior lecturer kwa miaka mitatu, kigezo cha pili ni teaching points ( sina kumbukumbu ni point ngapi zinahitajika) na tatu ni pint kutokana na publication kama nakumbuka vizuri ni point kama 5.5 au 6 hivi na hizi ni kutokana na publication kutoka katika peer reviewed journal! ukitimiza vigezo hivi vyote ndipo baraza la utumishi la chuo husika hutangaza kumpandisha muhusika kutoka level moja kwenda nyingine!
 
Mikojo tupu hapa ..., mdau anauliza anataka aelimishwe nyie mnapenga mikamasy yenu hapa!?
 
nadhamini uwepo wako hapa jf unamchango mkubwa sana mpigamsuli big up
kaka ndo tunatafuta data taratibu TUNAWEZA KUTIMIZA HIVYO VIGEZO SIKU NA SISI TUKAITWA MAPROFESA MFANO.profesamajutomperungu,by mpigamsuli
 
well said
 

Pale muhumbili kuna maprofesa wana maste tu. Tena wengine ni full proffesot. Sasa unawazumgumzaje hawa ambao hawana hata PHD
 
Pale muhumbili kuna maprofesa wana maste tu. Tena wengine ni full proffesot. Sasa unawazumgumzaje hawa ambao hawana hata PHD
kwani hao majaji wasiona vigezo wamepatikanaje jibi hili suali then nitakujibu lako!!!!!!!!!
 
Pale muhumbili kuna maprofesa wana maste tu. Tena wengine ni full proffesot. Sasa unawazumgumzaje hawa ambao hawana hata PHD

Sina uhakika kama ni kweli wamekuwa ma professor bila kuwa na PhD, inawezekana umechanganya kidogo, maana ni rahisi na ni kawaida mtu kuwa na PhD bila Masters ( nina ushahidi na hili), lakini kwa ufahamu wangu haiwezekani kuwa professor bila kuwa na PhD na machapisho ya kutosha! unakumbuaka kilicho tokea Mzumbe University mwaka juzi? walimu kadhaa walikuwa disqualified kwa kukosa vigezo vya madaraja waliyokuwa wamejipa!
 
mkuu phd bila masters ? inakuajemkuu tuwekee ukweli humu jf
 
Uwezekano upo, inategemea na taratibu za chuo au nchi husika. Kuna nchi nyinge professor ni kama vile tunavyoweza kuita "mwalimu" kwa kiswahili (i.e. halina uhusiano na chuo kikuu).
 
Mtafute mtu m1 anaitwa Steven Ngonyani ni mbunge wa korogwe vijijini na yeye ni proffesor atakuelezea vizuri taratibu za kuupata!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…