Vigezo vya TRA kufanya makadirio ya juu zaidi ya gharama halisi za magari yanayoingizwa nchini

KIMOMWEMOTORS

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2018
Posts
358
Reaction score
675
Salam wana jukwaa.

Kodi ilivyokadiriwa kwenye gari aina ya Subaru Exiga ya mwaka 2008, ambapo ushuru wa garii hii unasomeka kama Tsh 21,000,000 wakati Valuation iliyotumika kwenye kupata ushuru huo ni Dola 8000+

Uhalisia wa gharama za gari hii yaani CIF ni dola kati ya 2000 mpaka 5000+ kama ambavyo ntaambatanisha kwenye picha hapa chini. Kwa kweli kodi iliyokadiriwa ni kubwa mno kwa gari hii ukilinganisha na CIF halisi tunayoishuhudia kwenye mitandao ya wauzaji wa magari huko Japan ambayo ni kati ya CIF dola 1900 mpaka CIF dola 5000.

Subaru Exiga ya 2009 imethaminishwa kwa CIF dola 11,000 na Ushuru wake ni 22,000,000+ wakati ukiingia mitandao halisi ya wauza magari huko nje unakuta CIF dola 2000 mpaka 6000 ambayo ni chini sana tofauti na wanayotumia wao kwenye hesabu zao.

Ombi kwa mamlaka husika wajaribu kulipitia upya jambo hili au kama kuna vigezo maalum wanatumia kwa baadhi ya magari basi vizuri wakaweka utaratibu wa kutoa elimu juu ya vigezo hivyo ili watanzania wapate kufahamu.

Kama ni makosa ya kibinadamu pia wafanye marekebisho maana watanzania wengi wanataka kutumia gari hizi ila Ushuru mkubwa ni kikwazo.

Karibuni wadau kwa maoni zaidi ili Mamlaka ipate kuona uzito katika jambo hili na kwa aina nyingine za magari.


 
Wametumia kigezo gani Hadi ushuru uwe juu kiasi hiki? Maana Subaru exiga inafanana na legacy au athletes.....Kwa style hii tutaendelea kununua Toyota Tu tofauti na wenzetu wakenya wanasukuma mandinga ya maana na spare parts zipo nyingi Nairobi yote
 
Wametumia kigezo gani Hadi ushuru uwe juu kiasi hiki? Maana Subaru exiga inafanana na legacy au athletes.....Kwa style hii tutaendelea kununua Toyota Tu tofauti na wenzetu wakenya wanasukuma mandinga ya maana na spare parts zipo nyingi Nairobi yote
Ni wakati sasa walaji customers kupaza sauti!! wakisikia watarekebesha
 
Wametumia kigezo gani Hadi ushuru uwe juu kiasi hiki? Maana Subaru exiga inafanana na legacy au athletes.....Kwa style hii tutaendelea kununua Toyota Tu tofauti na wenzetu wakenya wanasukuma mandinga ya maana na spare parts zipo nyingi Nairobi yote
Kweli mpo sahihi hawa TRA Motor Vehicle system hawapo sahihi kabisa hii Model ya Exiga wameiweka kundi la SUV na wanaipiga zaidi ya 20M
labda kwa vile wapo kweny viti tu hawayajui magari yote, wauzaji/ waagizaji na watumiaji wangewahabarisha wabadili hicho kipenele
 
Kufanya biashara za importation hapa Tanzania inachukuliwa kama ANASA sasa Kwa vijana ambao wamejiajiri Kwenye sekta hii wanafanya biashara Kwenye mazingira magumu
 
Nawaambia mara nyingi hapa kwamba TRA ni kikwazo Tanzania. Lakini majinga majinga yanakuja hapa oooh...! Mnakwepa kodi. Ole wako yakukute. TRA wameirudisha nyuma sana hii nchi kwa kodi zao za ajabu ajabu. Siku hizi watu wanaoenda kuagiza mizigo nje wamepungua mno,sababu ya makadirio ya ovyo ya hawa njemba. TRA ni majanga
 
Kwa kawaida mitandao ya wauza magari duniani(hasa Japan), haiaminiki. Hivyo gari ya aina moja na umri mmoja inaweza kuuzwa bei tofauti tofauti.

Pia wateja wanaweza kula njama na wauzaji ili 'CIF value' iwe ndogo. Hivyo TRA ilichofanya ni kufanya utafiti na kujiwekea 'CIF value' waliyoifanyia kazi kwa magari mbalimbali ili wasije 'kupigwa' na wafanyabiashara.

Kinachokera ni pale wanapo-'uplift' tena hizi tarakimu baada ya gari kufika Bandarini na taratibu za malipo ya ushuru kuanza.

Hii inaleta wasiwasi kuwa hata kikokotoo chao wenyewe hawakiamini..
 
TRA wanaunga juhudi za serikali ya awamu ya Tano.
Wanataka watu waishi kama mashetani.
Kuna vitu ambavyo ni basic needs kama usafiri malazi chakula na mavazi inatakiwa visiwe na ushuru.

Unajega barabara halafu hutaki watu wanunue magari mwishowe wataingiza punda barabarani kama ilivyotokea kule chato kwenye lami
 
Mkuu umesema kweli, ila umebonyeza sana.
 
Nawaza tu hapa, hivi mbishi flani ukinunua Tesla kodi wataikadiriaje mana haina Engine CC wala Fuel(Petrol/Diesel) [emoji23][emoji23][emoji23]View attachment 1267812View attachment 1267813
hiyo kali sana Mkuu, watachanganyikiwa TRA
lkn utajaza wapi hiyo GAS ? maana hapo Ubungo ni ya kilomita 200 tu, service hawajuiwatakuacha wakishajaza ya Songosongo , matengenezo ni km Ndege zetu service unaruka nayo
 
hiyo kali sana Mkuu, watachanganyikiwa TRA
lkn utajaza wapi hiyo GAS ? maana hapo Ubungo ni ya kilomita 200 tu, service hawajuiwatakuacha wakishajaza ya Songosongo , matengenezo ni km Ndege zetu service unaruka nayo
Hiyo ngoma ya umeme mkuu ina battery haina engine ya mafuta wala gesi.

Kibongo bongo itabidi uchaji kwa umeme wa Tanesco. Huu huu wa single phase 220v ila ndio inabidi uweke circuit breaker kubwa zaidi ya 32amps. Betri itajaa ndani ya masaa 12 na utaweza kutembea 500km. Inachaji kwa 7kW so ndani ya masaa 12 itakuwa imetumia 84kWh yani unit 84 za umeme ambao kwa rate tunayonunua bongo ni kama umeme wa 30,000/= hivi

Yaani Tsh 30,000 unatembea 500km, Dar Dodoma hiyo. Tesla sio gari ya mchezo.

Ukitaka gari ijae haraka unafunga umeme wa three phase 400v hiyo mzigo unakuwa unachaji kwa 11kW ndani ya masaa 8 gari imejaa. So unit zinatumika zaidi kidogo 88kWh ila unakuwa umeokoa muda.

Usiulize service. Hizi gari hazina oil mkuu hazina oil filter hazina spark plugs, ATF na madude mengine. Motor yake ni sealed hamna cha kuservice. So labda uongezee maji ya wiper mkuu[emoji1787][emoji1787]

Gari hizi zina regenerative braking ambapo ukitoa mguu kwny pedal ya "mafuta" gari inageuza direction ya motor na kutumia momentum iliyobaki kwenye gari kulipunguza spidi huku at the same time umeme unaovunwa hapo unawekwa kwny betri. Kwahyo brake pad huzitumii sana kama kwny gari za engine.

Yani ukiwa unashuka mlima au ukiachia mafuta, tairi zinageuzwa dynamo kurudisha umeme kwny betri ya gari! Na kifanya hvyo ndo inakuwq kama breki ya gari yani. Chukulia mfano vile vitaa vya baiskeli vya kwny tairi ya mbele, kama unakumbuka ilikuwa ukiiconnect kwny tairi inawaka unavyoendesha ila baiskeli inakuwa nzito zaidi.

Vitu vya kutengeneza kwny hii gari labda mabushing na mashock up

Tatizo bei za hizi ndinga SIO MCHEZO.
Ila ukiipata unasahau shida.
 

Mtu atakaeweza Kununua Tesla ata ile base model (Model 3) hawezi waza kuhusu gharama za umeme.

Tatizo kubwa litakalofanya ata uwe Billionea TZ ushindwe kununua Tesla ni Service Baaasi.

Tesla hawauzi spare zao kwa mtu. Kama gari yako mbovu wapelekee, wataikagua wewe ukiwa kwenu (watakupa loaner car), wakifix utaifuata. Utalipa utasepa.

Ila usitegemee kupata ata screw au tairi la Tesla madukani labda ebay mfano mtu lake limekufa.

Youtube kuna jamaa anaitwa Rich Rebuild naonaga ana build Tesla kwenye gereji yake ilaanapata shida sana.

Mzee unaonekana unazielewa sana hizi ngoma. Safi sana. Ila One Day wateta Tu watu. Niliona Mo Dewj kapost kunasiku kwenye Insta labda ilikua showoff.
 
Yeah hiyo issue ya spare ndiyo iko hivyo. No thrird party dealership network. Plus vipuri vyake ni gharama balaa.

Nazielewa sana hizi kitu mkuu. And yes zitakuja tu hata zikisogea Kenya tutazikamatia huko huko.
 
Barabara za bongo utaiua hii gari mapema sana.

Hili gari lipo delicate kuliko maelezo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…