Vigogo hawa wa Wizara ya Mambo ya Nje wapelekwe mahakamani

Vigogo hawa wa Wizara ya Mambo ya Nje wapelekwe mahakamani

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
maalim.jpg

Naibu Waziri,Mahadhi Juma Maalim.

Yapo baadhi ya mambo yanayotokea Tanzania ambayo hakika hayawezi kutokea mahali pengine duniani. Ebu fikiria kisanga hiki. Pamoja na kuthibitishwa wizi wa zaidi ya Sh3.5 bilioni za Kitengo cha Itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na waliohusika na wizi huo kujulikana, Serikali imesema haikuwafungulia watu hao mashtaka kutokana na kutokuwapo ushahidi wa kutosha.


Naibu Waziri katika wizara hiyo, Mahadhi Juma Maalim alisema hayo juzi mbele ya Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakati alipokuwa akijibu hoja ya Mwenyekiti wa kamati hiyo, Edward Lowassa aliyetaka kujua maendeleo ya sakata hilo na hatima ya maofisa waliodaiwa kuchota fedha hizo kwa ajili ya safari za Rais ambazo zilikuwa hewa.



Naibu waziri huyo alisema fedha hizo zilichukuliwa na maofisa hao kinyemela kutoka Hazina kwa ajili ya safari za viongozi za kufikirika tu, hivyo baada ya Wizara kubaini kwamba fedha hizo zilichotwa Hazina bila kuidhinishwa wakati Waziri, Naibu wake na makatibu wakuu wakiwa hawapo, iliomba msaada wa Takukuru ili kuchunguza zaidi tukio hilo.



Kwa mujibu wa kiongozi huyo, uchunguzi wa Takukuru ulibaini kwamba kweli fedha hizo zilichotwa Hazina kwa uzembe au kwa nia ya kuiba na ndipo wajumbe wa kamati hiyo walipohoji kwa nini maofisa hao hawakupelekwa mahakamani kama Takukuru ilikuwa tayari imebaini kwamba maofisa hao walikuwa wamechukua fedha hizo kwa nia mbaya.



Naibu waziri huyo alisema Takukuru ilishauri kuwa, licha ya wahusika wote kubainika kuhusika katika tukio hilo, ilikuwa ni vigumu kuwashtaki kwa kuwa hakukuwa na ushahidi wa moja kwa moja, hivyo ndiyo maana Wizara iliishia kuchukua hatua za kiutawala pekee. Kama ilivyotazamiwa, majibu ya Naibu waziri huyo yaliwaacha wajumbe wote wa kamati hiyo wakiwa katika mshangao mkubwa pasipo kujua nini la kufanya.



Tumeorodhesha mlolongo wa sakata zima la wizi huo kwa lengo la kuonyesha jinsi tatizo la ufisadi linavyozidi kuwa akubwa katika nchi yetu na jinsi vyombo vilivyoundwa kupambana na tatizo hilo vinavyoshindwa kutumia sheria zilizopo kwa visingizio mbalimbali. Fedha hizo zilizochotwa kutoka Hazina ni nyingi na wote waliohusika walipaswa kufunguliwa mashtaka.



Lakini pengine katika kuonyesha kwamba tukio hilo halikuwa la kwanza na kwamba nyuma yake ulikuwapo mkono wa baadhi ya watu wakubwa, maofisa hao hawakuchukuliwa hatua stahiki na baadhi yao hivi sasa wanaendelea na kazi zao kama kawaida. Takukuru inaposema hakukuwapo ushahidi wa moja kwa moja dhidi ya maofisa hao, inaonyesha bayana kwamba hali kama ndiyo hiyo vita dhidi ya rushwa na ufisadi haitafanikiwa katika nchi yetu.



Sakata hilo linatukumbusha wizi wa mabilioni ya fedha za Epa miaka kadhaa iliyopita, ambapo baadhi ya watu waliokwapua fedha hizo za umma na baadaye kuzirudisha hawakushtakiwa mahakamani. Hivi pia ndivyo ilivyo katika sakata hili la maofisa wa Serikali kukwapua Sh3.5 bilioni kutoka Hazina kwa ajili ya safari hewa za Rais.



Kwa kuwa wamezirudisha, Takukuru inasema wasishtakiwe kwa maelezo kwamba hakuna ushahidi wa moja kwa moja. Hiyo ni nini kama sio mwisho wa vita yetu ndefu dhidi ya rushwa na ufisadi?
http://www.mwananchi.co.tz/uchambuzi/-/1597604/1726024/-/m3oplgz/-/index.html







 
Kwa ufahamu wangu jamaa wanaweza wakawa pia wanayo diplomatic immunity halafu ukijumlisha mambo yanayohusiana na politics its more likely that no one will be taken to court whtsoever..nawasikisha!
 
Kwa ufahamu wangu jamaa wanaweza wakawa pia wanayo diplomatic immunity halafu ukijumlisha mambo yanayohusiana na politics its more likely that no one will be taken to court whtsoever..nawasikisha!

Hiyo immunity inawalinda wanadiplomasia wageni waishio Tanzania and not these tanzanian crooks!
Mkuu hapo ni kulindana tuu na udhaifu wa vyombo vya serikali and nothing else !!

Lakini! Let them beware! Tuna- take note maovu na madudu yote wanayaoyafanya.... na retribution is coming sooner then they would like to believe!

c.c MziziMkavu
 
Last edited by a moderator:
Hiyo immunity inawalinda wanadiplomasia wageni waishio Tanzania and not these tanzanian crooks!
Mkuu hapo ni kulindana tuu na udhaifu wa vyombo vya serikali and nothing else !!

Lakini! Let them beware! Tuna- take note maovu na madudu yote wanayaoyafanya.... na retribution is coming sooner then they would like to believe!

c.c MziziMkavu
Mkuu Misterdennis kila chenye mwanzo hakikosi kuwa na mwisho tungojee uchaguzi unaokuja inshallah ukweli utajulikana.
 
Last edited by a moderator:
Mtu anaiba eti unamshusha cheo!inatia hasira sana
 
Back
Top Bottom