GE2025 Vigogo sita wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamechangia jumla ya Sh.milioni 150 katika harambee ya chama hicho

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
4,274
Reaction score
9,326
Vigogo sita wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamechangia jumla ya Sh.milioni 150 katika harambee ya chama hicho, inayolenga kupata kiasi cha Sh. bilioni 10 za kuwezesha kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Wametoa michango yao leo Agosti 12, 2025, katika harambee inayoendelea ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

Katika harambee hiyo, Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amechangia Sh. milioni 50, Makamu Mwenyekiti CCM, Stephen Wasira Sh. milioni 20, Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango, Sh. milioni 20, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Sh. milioni 20, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla Sh. milioni 20 na Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson Sh. milioni 20, ambapo jumla yake ni Sh. milioni 150.
 
Wezi wa Mali ya umma
 
 
Nyie. Watu muachage utapeli,kwani mmejifunza kwa wale manabii mchongo baada ya kupoteza ushawishi kutoka kwa jamiio ya kitanzania mnnaanza kutafuta ma dj wa miujiza aamaa??aaAlaaa?
 
Kwa jinsi mlivyowaona wakichangia hayo mamilioni ndivyo hivyo hivyo watakwapua na kujilimbikizia zaidi!
Shtukeni!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…