Angalieni ibara ya 15:1 na 2 ya Katiba ya CCM mtapa "clue" ya kwanini fedha za CCM zinauma mno kuliko za Serikali. Kwenye yahoo search for "Kataraiya, mwanakijiji"... utapata jibu pia.
Mzee wangu MK, kwani unaamini kwamba watu hawa wametolewa kwa ubadhirifu?? Come on jamani Malegesi aibe hivyo vimilioni vya nini wakati alikuwa mtu wa karibu na Balali na amepata kule jikoni kwenyewe???
Baada ya aibu ya NEC kutokufanya chochote, wameibua viporo vya news za mwaka jana. Hawa watu walishafukuzwa kitambo.
really..? Kikao cha Kamati Kuu ipi hiyo na kilifanyika lini? maana tusije kuwa tunazungusha habari za mwaka jana mwaka huu.. niko tayari kusahihishwa lakini naamini haya siyo maamuzi mapya..
Hili lilitokea zamani sana. Sijui huyu mleta habari alikuwa kahamia sayari gani hiyo. Nadhani huyu anasafiri kwa technology ya 'ungo,' toka kwenye hiyo sayari ya kusadikika.
Basi ingefaa wafukuzwe uanachama kabisa!
Kwa nini wasifunguliwe mashitaka??? Hawa wanatakiwa kupelekwa segerea. Toka lini mwizi huwa anaombwa kurudisha alichokwiba???Tukiamua kufuata utaratibu huu, basi tusianze kubagua. Wezi wote waliofungwa katika magereza waachiwe huru ili warejeshe walichokwiba. Hii itasaidia kupunguza mlundikano wa wafungwa magerezani