Vigogo wanavyopambana kutaka kuzima ndoto za Sopu

pwilo

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2015
Posts
10,913
Reaction score
13,876
Habari za weekend wadau,

Weekend inaisha vizuri huku mashabiki wa Yanga wakiwa na nyuso za furaha na tabasamu baada ya jana kupata ushindi katika final ya AZAM SPORTS FEDERATION dhidi ya coastal union wana mangushi Wagosi wa Kaya baada ya kushinda kwa mikwaju ya penalty.

Licha ya Yanga kutwaa ubingwa huo ila story kubwa kwa sasa ni kuhusu hatma ya mshambuliaji wa coastal union ambaye jana alikuwa nyota wa mchezo baada ya kufunga hatrick katika mechi hyo kwani team mbali mbali ndani na nje ya Tanzania zimetuma ofa ya kutaka kumsajili mchezaji huyo kutoka coastal union.

Inasemekana vigogo wa AZAM, YANGA na SIMBA wote wamepeleka ofa zao kutaka kumsajili mchezaji huyo huku akiwa na ofa yakufanya trial NORWAY.

Ikumbukwe SOPU alishapitia SIMBA SPORTS CLUB kabla ila kwa takwimu zinavyoonyesha club za kariakoo hazina uvumilivu katika wachezaji vijana hata kama wanaonyesha mwangaza kwani kuna vijana wazuri tu.

Walioachwa kijanja janja na club za kariakoo hivyo nauona mwisho mbaya kwake kama atakubali kuwatumikia wafalme hao wa soka Tanzania ila kwenda AZAM anaweza akawa amefanya maamuzi mazuri na ya manufaa kwa career yake.

Mfano wa wachezaji waliopotea kwa siasa za simba na yanga :–

Yusuph Mhilu, Mateo Antony na Luis Gustavo (YANGA)
Miraji athumani Rashid Juma na David Kameta(SIMBA)
licha ya kuonyesha walikuwa na kitu katika career yao ila waliachwa solemba kwasababu mbali mbali ikiwemo majeraha na kutopata mda mwingi wa kucheza katika team hizo,
Njia sahihi kwa SOPU ni kwenda kucheza nje au kusalia Tanzania kwa wana lamba lamba tofauti na hapo Tanzania itapoteza kipaji kingine kwa siasa za simba na yanga.

SOPU ni hazina kwa taifa TFF mumlinde kwa maslahi ya taifa na mpira wa Tanzania.
 
Akienda Yanga kapotea, Nkane mfano mzuri tu
Mbona Nkane anapata game time na Jana Katia kambani Gori la tatu? Simba ndiyo mortuary ya wachezaji wengi wa ktz refer; Rashid Juma, Miraji Athman, Charles Ilamfya, Jeremiah Kisubi, David Kameta a k a Duchu, Yusuph Mhiru, Gymson Mwanuke, Israh Kwenda nk nk ni wengi mno, Kama Sopu yuko vizuri Basi akuje Jangwani na hakika ata Excel.
 
Yusufu Bakhresa weweeee
 
Ongeza Atupele, Kaheza, Salamba (Makoloz)
 
Akienda Yanga kapotea, Nkane mfano mzuri tu
Nkane kapotea wapi! Mechi ya mwisho na Mtibwa, goli alifunga nani? Mechi ya jana na hao Coastal, goli la 3 alifunga nani?

Yanga ya Profesa Nabi inajali sana vipaji vya wachezaji vijana! Ndiyo maana leo unawaona akina Dickson Job na Kibwana Shomari wakicheza mara nyingi! Akina Mshery nao wanapewa nafasi, hata kama kuna mlinda mlango namba 1!

Hata huyo Sopu angeenda Yanga, angecheza! Akienda simba, kuna mawili! Acheze, au asugue benchi! Akienda Azam, ataishia tu kuota kitambi kama Ibrahim Ajibu! Maana wachezaji wa Azam wengi wanaridhika haraka! Na siyo wachezaji wenye malengo ya kufanya makubwa! Na sababu wanazijua wao wenyewe.

Ushauri wangu; kama atapata ofa Ulaya, aende ili tuongeze wigo wa kuwa na wachezaji wengi wanaocheza soka Ulaya kwenye timu yetu ya Taifa.
 
Mbona Nkane anapata game time na Jana Katia kambani Gori la tatu? Simba ndiyo mortuary ya wachezaji wengi wa ktz refer; Rashid Juma, Miraji Athman, Charles Ilamfya, Jeremiah Kisubi, David Kameta a k a Duchu, Yusuph Mhiru, Gymson Mwanuke, Israh Kwenda nk nk ni wengi mno, Kama Sopu yuko vizuri Basi akuje Jangwani na hakika ata Excel.
Huyo sopu ulimkuza wewe?
 
Huyo sopu ulimkuza wewe?
Na Mhiru ulimkuza wewe, mbona mmemharibia performance yake? Likija suala la usajili habari ya kukuza inawekwa pembeni, maslahi ndiyo kipaumbele.
 
Yanga kumejaa vipaji na makombe hana nafasi Simba wanaua vipaji Azam hawana presha ya makombe bora aende ulaya tu
😂😂😂 sawa mkuu na vile ana vizuizi south bora aende ulaya ila kwa kuwa tyr ameshasaini uto imekuw bora maan uto hawawezi kufika south .......mwisho wao ni Nigeria
 
Aende tu ulaya akafanye trial
Akibakia kwenye
Ligi ya mipasho atapotea tu

Ova
 
Back
Top Bottom