pwilo
JF-Expert Member
- May 27, 2015
- 10,913
- 13,876
Habari za weekend wadau,
Weekend inaisha vizuri huku mashabiki wa Yanga wakiwa na nyuso za furaha na tabasamu baada ya jana kupata ushindi katika final ya AZAM SPORTS FEDERATION dhidi ya coastal union wana mangushi Wagosi wa Kaya baada ya kushinda kwa mikwaju ya penalty.
Licha ya Yanga kutwaa ubingwa huo ila story kubwa kwa sasa ni kuhusu hatma ya mshambuliaji wa coastal union ambaye jana alikuwa nyota wa mchezo baada ya kufunga hatrick katika mechi hyo kwani team mbali mbali ndani na nje ya Tanzania zimetuma ofa ya kutaka kumsajili mchezaji huyo kutoka coastal union.
Inasemekana vigogo wa AZAM, YANGA na SIMBA wote wamepeleka ofa zao kutaka kumsajili mchezaji huyo huku akiwa na ofa yakufanya trial NORWAY.
Ikumbukwe SOPU alishapitia SIMBA SPORTS CLUB kabla ila kwa takwimu zinavyoonyesha club za kariakoo hazina uvumilivu katika wachezaji vijana hata kama wanaonyesha mwangaza kwani kuna vijana wazuri tu.
Walioachwa kijanja janja na club za kariakoo hivyo nauona mwisho mbaya kwake kama atakubali kuwatumikia wafalme hao wa soka Tanzania ila kwenda AZAM anaweza akawa amefanya maamuzi mazuri na ya manufaa kwa career yake.
Mfano wa wachezaji waliopotea kwa siasa za simba na yanga :β
Yusuph Mhilu, Mateo Antony na Luis Gustavo (YANGA)
Miraji athumani Rashid Juma na David Kameta(SIMBA)
licha ya kuonyesha walikuwa na kitu katika career yao ila waliachwa solemba kwasababu mbali mbali ikiwemo majeraha na kutopata mda mwingi wa kucheza katika team hizo,
Njia sahihi kwa SOPU ni kwenda kucheza nje au kusalia Tanzania kwa wana lamba lamba tofauti na hapo Tanzania itapoteza kipaji kingine kwa siasa za simba na yanga.
SOPU ni hazina kwa taifa TFF mumlinde kwa maslahi ya taifa na mpira wa Tanzania.