beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,880
- 6,368
Aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Laurian Bwanakunu pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Lojistiki Byekwaso Tabura watafikishwa Mahakama ya Kisutu kujibu mashtaka yanayowakabili.
Taarifa iliyotolewa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imesema wanakabiliwa na mashtaka ya kuisababishia hasara Serikali, matumizi mabaya ya madaraka pamoja na utakatishaji wa fedha haramu.
Wawili hao ambao walikamatwa Juni 02, 2020 wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani saa tano asubuhi.
Pia soma > TAKUKURU yamnasa aliyekuwa bosi mkuu wa Bohari ya Madawa nchini (MSD)