Vijana 331 wamechaguliwa kujiunga na mafunzo ya Idara ya Uhamiaji

Vijana 331 wamechaguliwa kujiunga na mafunzo ya Idara ya Uhamiaji

Mwachiluwi

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2022
Posts
25,258
Reaction score
48,589
Idara ya Uhamiaji Tanzania imetangaza majina ya vijana 331 waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya idara hiyo kuanzia Machi 1, 2025.

Screenshot 2025-02-06 140359.png
Tangazo la kuitwa kwenye mafunzo hayo limetolewa leo Alhamisi Februari 6, 2025 na Kamishna Jenerali wa idara hiyo.

“Kamishna Jenerali wa Uhamiaji anawatangazia vijana ambao wamechaguliwa kujiunga na Idara ya Uhamiaji kuripoti Chuo cha Uhamiaji cha Raphael Kubaga kilichopo Boma Kichakamiba, Wilaya ya Mkinga - Mkoani Tanga, Jumamosi Machi mosi 2025 kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 8:00 mchana,” imeeleza taarifa hiyo.

Pia, kwa walioomba na kuchaguliwa kupitia Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, wanatakiwa kuripoti Afisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kusini Unguja (Tunguu) Jumatatu Februari 24, 2025 saa 2:00 asubuhi.

Katika taarifa hiyo vijjana waliochaguliwa kujiunga na mafunzo hayo wametakiwa kuripoti wakiwa na vyeti halisi vya elimu na fani mbalimbali.
 

Attachments

Vip mkuu unaona wasumbua vijana
Safar hii wameita watu weng kwenye usaili hivyo nikajua watachukua watu wengi lakin dooh kumbe ndo kwaanza wamejitahid kuchukua watu wachache
 
 
Polisi walinipiga chini dakka za jion na uhamiaji nao wamenipiga chini
 
Back
Top Bottom