Vijana chukueni mchongo wa soya

Hii nchi tuna mito ya kutosha na ardhi za kutosha ila serikali inashindwa kujenga scheme za umwagiliaji kuwasaidia wakulima kupunguza gharama za kununua petroli na dizeli kwa ajili ya kumwagilia mashamba.

Wakulima wengi hawakopesheki na taasisi za fedha..unategemea watalimaje
 
Mkuu wewe unalima? au unahamasisha wengine walime ili uje kuwachuuza.
 
Mkuu wewe unalima? au unahamasisha wengine walime ili uje kuwachuuza.
Mie kuhusu kilimo nilishashindwa najaribu kuwatia moyo watu pengine inaweza kuwa rizki yao
 
Mkuu, ukipata mtendaji(sio wa ofisini) kwenye sekta ya korosho akusimulie hii maneno utachoka maana ni ukweli mchungu. Hakuna juhudi za makusudi kuboresha sekta, siasa nyingi.
Nashukuru kwa unaelewa...
Pamoja sana
 
Ni kweli anza wewe watafata hii dunia nimegundua hutuwez wote kufanya ki2 kimoja..
 
Hii nchi sio rafiki kwa mkulima labda hao wenye mitaji mikubwa. Unalima kwa tabu ukivuna kuna mtu anaitwa dalali anakuja kukupiga kata funua. Wanachezesha bei anakwenda kufaidika yeye unajuta mpaka unawaza bora ungelima msuba.
Naandika kwa uzoefu wangu niliyokutana nayo front line mimi mwenyewe huko shambani.
 
Ukiondoa dalali inakuja sirikali inakwambia mwaka huu tunatabiri kutakuwa na baa la njaa Kwaiyo hakuna nafaka kuuzwa nje ya inji ilitujitosheleze kwa chakula, hapo una gunia zako afu tatu za mahindi ghafla unaanza kuambiwa uuze debe afu Sita 😁😁😁
 
Hii imekaa poa sana samahani mkuu unaweza share kidogo jinsi ya kuyafikia hayo masoko ya nje hasa usafiri na vipari vyake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…