Vijana fanyeni kazi kwa bidii maishani, msiwe wavivu wa kupoteza muda

Vijana fanyeni kazi kwa bidii maishani, msiwe wavivu wa kupoteza muda

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
VCG111385176021.jpg


Tarehe mosi, Juni ni Siku ya Watoto China. Watoto ni maua ya nchi na mustakabali na matumaini ya taifa. Kutoka "Vijana wafanye kazi kwa bidii maishani, wasiwe wavivu wa kupoteza muda" hadi "kustaarabisha roho zao na kuimarisha miili yao", tangu aingie madarakani, rais Xi Jinping wa China mara kwa mara amezungumza na watoto wa shule za msingi na sekodari, kujibu barua ili kuwahimiza wanafunzi wa makabila mbalimbali na kutembelea familia za watu waishio katika maeneo maskini. Ujumbe wa dhati na matumaini makubwa yote yanaonyesha jinsi rais Xi anavyozingatia sana ukuaji mzuri wa watoto kwa pande zote.

Xi Jinping aliposhiriki mazungumzo katika shule ya msingi ya Minzu wilayani Haidian, Beijing mwaka 2014, alinukuu mstari wa shairi “Vijana fanyeni kazi kwa bidii maishani, msiwe wavivu wa kupoteza muda” akihimiza vijana wa kizazi kipya kujitahidi na kuthamini muda. Mstari huu unatoka katika shairi lililotungwa na mshairi wa enzi ya Tang Du Xunhe kwa mpwa wake. Maana yake ni kuwa bidii za utotoni zinanufaisha watu katika maisha yote, na kwamba muda unaenda, watu hawapaswi kuzembea na kuchezea muda. Haya sio tu maneno ya mshairi huyo ya kumtia moyo mpwa wake pekee, bali pia ni maarifa ya kimaisha ya wazee.

Kusoma kwa bidii ndio kipaumbele cha kwanza kwa watoto, lakini kuwa na afya nzuri ni jambo analojali zaidi rais Xi. Mwaka 2020, wakati wa ziara ya ukaguzi katika shule moja ya msingi ya kitongoji katika eneo lililo nyuma kimaendeleo mkoani Shaanxi, Xi aliuliza juu ya hali ya masomo na maisha ya watoto. Alisema, "siku hizi watoto wengi wanavaa miwani, hali ambayo inanitia wasiwasi, pamoja na hali ya afya ya watoto inayopungua, kutokana na mazoezi kidogo ya mwili.

Wachina husema ‘kustaarabisha roho na kuimarisha miili’ hapa kuimarisha miili maana yake ni kujenga miili.” Sentensi hiyo ni kama muhtasari mzuri wa elimu, na kusisitiza maendeleo ya roho na miili ya vijana kwa pamoja. Vijana hodari wanatakiwa kuwa na maendeleo ya pande zote, yaani afya nzuri, utu mzuri, tabia bora ya masomo, na kuwa na uhai mkubwa, ili kuwa na nguzo za kujenga na kustawisha taifa.
 
Back
Top Bottom