Vijana kuisaliti nchi yetu Kenya kwa Shilingi 500/= tu

Vijana kuisaliti nchi yetu Kenya kwa Shilingi 500/= tu

Kingmaja

Member
Joined
Sep 15, 2018
Posts
68
Reaction score
111
Yaibuka Vijana Waliotumika Kupanga Ghasia Za Kenol Waliahidiwa Sh500

Na. Majaliwa Abdulkadli Amran

VIJANA waliotumiwa na wanasiasa wa mirengo ya Tangatanga na Kieleweke mjini Kenol, Kaunti ya Murang’a Jumapili iliyopita walikuwa wameahidiwa kulipwa kati ya Sh500 na Sh1,000, wapelelezi wameambia KINGMAJA MEDIA.

Imeibuka kuwa wengi wa vijana hao si wakazi wa kaunti hiyo, na walitolewa kaunti za Nairobi na Kiambu kuzua vurugu katika makabiliano yaliyowaacha watu wawili wamefariki.

Polisi wamethibitisha kuwa gavana mmoja, wawakilishi wawili wanawake na mbunge mmoja, wote kutoka eneo la Mlima Kenya walifadhili safari za mabasi yaliyowapeleka vijana hao kwenye kuzua ghasia.

Kwenye mpango huo mchafu pia alikuwepo mbunge mmoja kutoka jijini Nairobi aliyewalipia vijana hao gharama zote. Wanasiasa wa upande wa Kieleweke walipanga njama za kuhakikisha kuwa masafara wa Naibu Rais kuelekea Kenol umekwazwa huku wale wa Tangatanga pia wakilipa vijana kupangua njama zote za kumzuia Dkt Ruto.

Kundi moja la kisiasa lililipa vijana kutoka mitaa ya Wetethie na Kiandutu mjini Thika huku kundi pinzani likisafirisha vijana kutoka mitaa ya Mwiki, Githurai, Kasarani, Kayole na hata Kibera.

Hoteli tatu, moja mjini Maragua, nyingine mjini Thika na ya tatu katika eneo la barabara ya Thika zilitumika kuandaa mipango ya vurumai na kushawishi vijana tangu Jumatano.
 
Tatizo sio hao wananchi ni hao wanasiasa.

Wa kuadhibiwa vikali ni hao wanasiasa.

Cha ajabu kwa vile wanasiasa ni rulling class,hua hawaadhibiani hata kidogo,ni members wa brotherhood ya political class.

Even Uhuru can never touch them,they are the same dogs they know each other!
Yeah sure,
 
Njaa! Njaaa!njaaa! Njaaa.=ugomvi. Ushawi. Ukabila. Utumwa. Nk
Njaa ni wewe na ndugu zako waccm.Usisiemu na ujinga ndio inawasumbua sana
 

Attachments

  • Screenshot_20201012-133820_1602499127427.jpg
    Screenshot_20201012-133820_1602499127427.jpg
    37.6 KB · Views: 2
Itakuw pic ya 1980's.sawa nyang'au wa kike.acha uyo mlevi awaburuze na genge lake la kizungu.sisi tunazidi kuwakeraaa

'
Magu oyeeee🙄😂😂. Bandwagons mna lipi la kusema.Just bunch of bums who will never succeed at shit in life
 

Attachments

  • Screenshot_20201012-134241_1602683397845.jpg
    Screenshot_20201012-134241_1602683397845.jpg
    25 KB · Views: 2
Back
Top Bottom