A
Anonymous
Guest
Mgogoro Longido Milioni 131 zapotea .
Zaidi ya Vijana 600 kutoka katika kijiji cha cha Ngereyeni kata ya Tingatinga wilayani Longido wamevyaamia makao makuu ya ofisi na kuharibu mali ya jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori Endumet(EWMA).
Akizungumza na Mwandishi kwa njia ya simu(jina limehifadhiwa) alisema kumekuwa na mvutano baina ya kijiji hicho na uongozi wa jumuiya unaosababishwa na eneo la kilimo.
Kuna eneo ambalo awali ilikuwa chini ya kampuni ya uwindaji ya Kilombero,baada ya kampuni hiyo kuona eneo hilo lipo katika mkondo wa maji walikabidhi kwa jumuiya(EWMA).
Walilitoa kwa jumuiya mwaka 2024 ili liwe sehemu ya hifadhi,lakini wakazi wa kijiji hicho walilivamia na kuanza kufyeka kwa ajili ya shughuli za kilimo.
Anasema jumuiya baada ya kubaini kuna zoezi hilo linaloendelea kinyume na taratibu walitoa onyo lakini bado jamii baada ya kikao kilichoketi jumatano pamoja na viongozi wa jumuiya wapo waliorudi kuendelea na zoezi la uandaaji wa mashamba katika eneo hilo.
Anasimulia kuwa,walivyorudia jambo hilo mamlaka ziliwakamata wahusika lakini mwenyekiti wa jumuiya hiyo aliomba wayamalize katika vikaoo,hivyo vijana hao waliachiwa huru.
Siku walipoachiwa waliratibu uvunjifu wa Amani kwa kuitana kwa kutumia filimbi ya jadi kwa ishara ya kuelekea eneo la jumuiya na kufanya uhalifu.
Anasema eneo lililovyamiwa na wakazi hao kwa lengo la kutaka kuanzisha shughuli za kilimo,jumuiya ilijipanga kufanya sehemu ya kambi ya farasi hata hivyo eneo hilo lina majengo ya thamani na mazingira ni rafiki.
Vijana hao walifika katika ofisi za EWMA wakiwa wamebeba mikuki nakuanza kuharifu mali kwa kuvunja vioo vya majengo,kuharibu pikipiki,nishati ya jua pamoja na kukata miti kwa kutumia silaha za jadi aina ya sime.
Hata hivyo taarifa ya tathimini ya awali ya gharama za mali kutokana na vurugu hizo inaonyesha kuwa ni sililingi milioni 131,493,750 zimepotea kutokana na uharibifu huo.
Je kampuni ya kilombero imezingatia sharia gani kutoa eneo hilo kwa jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori endument?Kuna makubaliano gani ya siri kati ya Endument jumuiya na Kilombero?Endument jumuiya ilipokeaje eneo hilo ambalo halipo katika maeneo yaliyotengwa na vijiji kama sehemu ya hifadhi?nani mchonganishi katika hili?vyombo vya ulinzi na usalama vipo wapi hadi njama hizi zinapangwa? Tunatambua kil kata inao polisi kata kwa nini hili limeshindikana kudhibitwa?
Hata hivyo serikali kupitia wizara ya maliasili na utalii itupie jicho katika jumuiya hiyo imekuwa ikitajwa katika matukio ambayo si salama kwa jamii ikiwemo katiba kuandaliwa bila ushirikishwaji wa wananchi, hata hivyo wananchi walivyoomba kupitia rasimu ya katiba hawakupatiwa,wasiwasi wa vijiji 11 vinavyounda jumuiya hiyo ni kutokana na mambo yanayoendelea katika jumuiya bila utaratibu mzuri.
Migogoro mingi inatokana na kukosekana kwa uwazi na uwajibikaji kwa viongozi kwa wanajumuiya,serikali fuatilieni hili kupata yaliyojifucha.