SoC02 Vijana na mnyororo wa thamani

SoC02 Vijana na mnyororo wa thamani

Stories of Change - 2022 Competition
Joined
Jul 27, 2022
Posts
94
Reaction score
134
Mnyororo wa thamani (Value Chain) ni mfumo mzima wa uzalishaji, usindikaji na uuzaji wa bidhaa haswa za kilimo na ufugaji (agriculture products).

Kama ilivyokuwa zamani tuliwahi kuiishi kauli mbiu ya “Kilimo ni uti wa mgongo” , kauli ambayo haifanyi kazi kabisa kwa baadhi ya vijana. Na hata wale wachache waliofanikiwa kujihusisha katika shughuli hizi wamekuwa wachoyo wa kurithisha maarifa kwa vitendo na badala yake Elimu ya kilimo imebaki tu “Kilimo cha mtandaoni” kama wasemavyo wengi.

Mnyororo wa kurithisha ujuzi na maarifa kuhusu kilimo na ufugaji huanzia kwa wazazi wetu ambao walisombwa na mabadiliko ya utandawazi na kusahau kuturithisha ukulima wenye tija na kutuacha tuendelee kutumia vyakula vilivyopanda ndege na meli miezi kadhaa kutufikia.

Leo natamani vijana waamke kwenye ndoto za kula Matufaa (Apples) yaliyopanda ndege kutoka Afrika ya kusini, tutoke kwenye wimbi la kusubiri vyakula vinavyokuja kwa meli, vyakula vilivyotunzwa kwa kamikali, vyakula vinavyosafiri miezi kadhaa hadi kumfikia mlaji, Naamini hapo tunafahamu fika namna tunavyoharibu afya.

TUFANYEJE KUREJESHA THAMANI YA MKULIMA NA MFUGAJI HUKU TUKITENGENEZA AJIRA?

Ili telete maendeleo endelevu, vija tuna uwezo wa kumrejeshe thamani mkulima na mfugaji kwa kujihusisha na masuala yafuatayo;

1. JENGA MAHUSIANO CHANYA NA MKULIMA/MFUGAJI
Kwa sababu vijana wengi tumeshindwa kuingia shambani wenyewe kulima kutokana na sababu mbalimbali, labda ni mitaji na ukosefu wa uwezo wa kumiliki mashamba yetu ama ukasumba wa kuchukia maisha ya vijijini. Tujaribu sasa kujenga mahusiano chanya na wakulima na wafugaji. Hakuna furaha kubwa kama siku moja mtu ama watu wa mjini wakimtembelea mkulima ama mfugaji mmoja kule kijijini na kumjulisha shauku zao za kufahamu mengi kuhusu shughuli anazozifanya. Naamini tutaacha tabasamu pana kwa mkulima yule maana ataiona thamani yake haswa kwa namna tutakavyojitoa kumfikia alipo. Na hapo huwezi kutoka bila kupewa yale matunda yetu ya asili na mazao kadhaa ya kuwapelekea we mjini kama ushuhuda wa safari yako ya shambani.

2. TENGENEZA UMOJA

Pia tunaweza kutengeneza mazingira ya kufanya kazi kwa kushirikiana. Hakuna maendeleo endelevu bila ushirikiano. Tukikumbuka zamani hata kazi ya kupukusua mahindi ilimalizika kwa haraka pale tulipoifanya kwa umoja wetu. Niliwahi kupitia ripoti moja ya Benki ya Dunia iliyoandikwa mwaka 2020, ripoti hii ilionesha namna viwanda vinavyoweza kuzalisha kwa wingi pale vinaporuhusu ushirikiano. Mfano walioutoa ulikuwa ni wa Kiwanda cha pili cha Bwana Smith, alisema ilibidi waajiri watu ambao walifanya kazi kwa haraka na kugawana majukumu. Mfano kulikuwa na wanaotengeneza vichwa vya pini, kuna waliunga unga nyaya, na kuna waliokamalisha pini sasa. Hapa kila mmoja alifanya kazi iliyoleta tija kwa lengo moja.

Kwa mfano huu, tunaweza kurejesha dhana chanya ya kujitolea na kujenga umoja ambao kila kijana anaweza kuchangia mtaji katika kuanzisha harakati za kujikwamua kiuchumi. Mfano: nina shamba naweza kuitoa ardhi kwa wataalamu wa kulima kwa makubaliano ya kushirikiana katika mazao yetu ya biashara

Tunaweza pia kuwatembelea wakulima na wafugaji ambao wanasafiri umbali mrefu kupeleka mazao yao sokoni, tukanunue mashambani hukohuko, tujenge Upendo na uaminifu kwao, tununue hata kwa malii kauli, Naamini kwa namna tutakavyojihusisha nao tunaweza kabisa kutengeneza taifa lisilo na ubaguzi na kejeli kwa wakulima.

3. MPUNGUZIE ULIPAJI WA KODI

Tunapowanunuza wakulima moja kwa moja mshambani hakika tunawapunguzia mzigo mkubwa wa kodi mbalimbali wanazokutana nazo katika safari za kupeleka mazao yao sokoni. Kwa namna tutakavyompa thamani mkulima tutajitengenezea mazingira ya kuaminiwa na kuungana kithabiti kabisa katika kuyaelekea maendeleo endelevu.

4. RITHISHA MAARIFA YA MNYORORO WA THAMANI

Tuhakikishe sisi vijana tunaisoma haswaaa hii Elimu ya mnyororo wa thamani na kutengeneza madarasa mbalimbali kule vijijini ambayo yatatupa mitaji mikubwa kabisa. Tukamfundishe mkulima huko kwamba sip lazima Kijiji kizima kilime mahindi tu, la hasha, mmoja anaweza kulima mahindi, mwingine akawa mfanyabiashara wa magunia ya kubebea mahindi na vifungashio mbalimbali, mwingine anaweza kutengeneza nembo ambayo ataiweka kwenye kila gonna, mwingine anaweza kufungua duka la pembejeo za kilimo hukohuko karibu na mashamba, mwingine awe anajihusisha na kutoa darasa kwa vitendo kuhusu namna ya kupata mazso yaliyo bora kabisa kulingana na soko.

Kuna namna ambayo tukiamua sisi kama vijana tuna uwezo mkubwa wa kutengeneza jamii yenye upendo, usawa, utu na ushirirkiano ambayo itawezesha urithishaji wa maarifa na kutupeleka kwenye uwanda mpana wa uelewa juu a uthamani wa mnyororo wa thamani. Hii itaturejesha kwenye bustani ya mboga zetu za asili kama vile mgagani, mchunga, tembele, bwete, msusa n.k ambapo kuna wimbi kubwa la watoto wetu hawajui hata majina ya baadhi ya mboga hizi tamu na adimu kwa sasa. Pia tunaweza kuresha miti yetu ya asili yenye matunda na dawa pia, mfano mibuyu ambayo tunaikata kwa Imani potofu huko mijini, mafioksi, matunda yetu matopetope, mastafeli na matunda mazuri yaliyoburudisha tukiwa tunakula tukiwa pamoja katika familia zetu za miaka kadhaa iliyopita.

Mwisho kabisa ila si kwa umuhimu Naamini kwa kumpa mbinu za ukulima na ufugaji bora huyu ndugu yetu tutakuwa tumejitengenezea ajira za kudumu na kurejesha tabasamu usoni kwa mkulima huyu na hakika thamani ya kila mmoja itarejea. Hakika tutaleta maeneleo endelevu katika jamii yetu na vizazi vijavyokwa ujumla wake.

Mimi ninayejifunza kila siku,
Mwl. Demitria T. Gibure.
 
Upvote 33
VIJANA NA MNYORORO WA THAMANI.

Mnyororo wa thamani (Value Chain) ni mfumo mzima wa uzalishaji, usindikaji na uuzaji wa bidhaa haswa za kilimo na ufugaji (agriculture products).

Kama ilivyokuwa zamani tuliwahi kuiishi kauli mbiu ya “Kilimo ni uti wa mgongo” , kauli ambayo haifanyi kazi kabisa kwa baadhi ya vijana. Na hata wale wachache waliofanikiwa kujihusisha katika shughuli hizi wamekuwa wachoyo wa kurithisha maarifa kwa vitendo na badala yake Elimu ya kilimo imebaki tu “Kilimo cha mtandaoni” kama wasemavyo wengi.

Mnyororo wa kurithisha ujuzi na maarifa kuhusu kilimo na ufugaji huanzia kwa wazazi wetu ambao walisombwa na mabadiliko ya utandawazi na kusahau kuturithisha ukulima wenye tija na kutuacha tuendelee kutumia vyakula vilivyopanda ndege na meli miezi kadhaa kutufikia.

Leo natamani vijana waamke kwenye ndoto za kula Matufaa (Apples) yaliyopanda ndege kutoka Afrika ya kusini, tutoke kwenye wimbi la kusubiri vyakula vinavyokuja kwa meli, vyakula vilivyotunzwa kwa kamikali, vyakula vinavyosafiri miezi kadhaa hadi kumfikia mlaji, Naamini hapo tunafahamu fika namna tunavyoharibu afya.

TUFANYEJE KUREJESHA THAMANI YA MKULIMA NA MFUGAJI HUKU TUKITENGENEZA AJIRA?

Ili telete maendeleo endelevu, vija tuna uwezo wa kumrejeshe thamani mkulima na mfugaji kwa kujihusisha na masuala yafuatayo;

1. JENGA MAHUSIANO CHANYA NA MKULIMA/MFUGAJI
Kwa sababu vijana wengi tumeshindwa kuingia shambani wenyewe kulima kutokana na sababu mbalimbali, labda ni mitaji na ukosefu wa uwezo wa kumiliki mashamba yetu ama ukasumba wa kuchukia maisha ya vijijini. Tujaribu sasa kujenga mahusiano chanya na wakulima na wafugaji. Hakuna furaha kubwa kama siku moja mtu ama watu wa mjini wakimtembelea mkulima ama mfugaji mmoja kule kijijini na kumjulisha shauku zao za kufahamu mengi kuhusu shughuli anazozifanya. Naamini tutaacha tabasamu pana kwa mkulima yule maana ataiona thamani yake haswa kwa namna tutakavyojitoa kumfikia alipo. Na hapo huwezi kutoka bila kupewa yale matunda yetu ya asili na mazao kadhaa ya kuwapelekea we mjini kama ushuhuda wa safari yako ya shambani.

2. TENGENEZA UMOJA

Pia tunaweza kutengeneza mazingira ya kufanya kazi kwa kushirikiana. Hakuna maendeleo endelevu bila ushirikiano. Tukikumbuka zamani hata kazi ya kupukusua mahindi ilimalizika kwa haraka pale tulipoifanya kwa umoja wetu. Niliwahi kupitia ripoti moja ya Benki ya Dunia iliyoandikwa mwaka 2020, ripoti hii ilionesha namna viwanda vinavyoweza kuzalisha kwa wingi pale vinaporuhusu ushirikiano. Mfano walioutoa ulikuwa ni wa Kiwanda cha pili cha Bwana Smith, alisema ilibidi waajiri watu ambao walifanya kazi kwa haraka na kugawana majukumu. Mfano kulikuwa na wanaotengeneza vichwa vya pini, kuna waliunga unga nyaya, na kuna waliokamalisha pini sasa. Hapa kila mmoja alifanya kazi iliyoleta tija kwa lengo moja.

Kwa mfano huu, tunaweza kurejesha dhana chanya ya kujitolea na kujenga umoja ambao kila kijana anaweza kuchangia mtaji katika kuanzisha harakati za kujikwamua kiuchumi. Mfano: nina shamba naweza kuitoa ardhi kwa wataalamu wa kulima kwa makubaliano ya kushirikiana katika mazao yetu ya biashara

Tunaweza pia kuwatembelea wakulima na wafugaji ambao wanasafiri umbali mrefu kupeleka mazao yao sokoni, tukanunue mashambani hukohuko, tujenge Upendo na uaminifu kwao, tununue hata kwa malii kauli, Naamini kwa namna tutakavyojihusisha nao tunaweza kabisa kutengeneza taifa lisilo na ubaguzi na kejeli kwa wakulima.

3. MPUNGUZIE ULIPAJI WA KODI

Tunapowanunuza wakulima moja kwa moja mshambani hakika tunawapunguzia mzigo mkubwa wa kodi mbalimbali wanazokutana nazo katika safari za kupeleka mazao yao sokoni. Kwa namna tutakavyompa thamani mkulima tutajitengenezea mazingira ya kuaminiwa na kuungana kithabiti kabisa katika kuyaelekea maendeleo endelevu.

4. RITHISHA MAARIFA YA MNYORORO WA THAMANI

Tuhakikishe sisi vijana tunaisoma haswaaa hii Elimu ya mnyororo wa thamani na kutengeneza madarasa mbalimbali kule vijijini ambayo yatatupa mitaji mikubwa kabisa. Tukamfundishe mkulima huko kwamba sip lazima Kijiji kizima kilime mahindi tu, la hasha, mmoja anaweza kulima mahindi, mwingine akawa mfanyabiashara wa magunia ya kubebea mahindi na vifungashio mbalimbali, mwingine anaweza kutengeneza nembo ambayo ataiweka kwenye kila gonna, mwingine anaweza kufungua duka la pembejeo za kilimo hukohuko karibu na mashamba, mwingine awe anajihusisha na kutoa darasa kwa vitendo kuhusu namna ya kupata mazso yaliyo bora kabisa kulingana na soko.

Mwisho kabisa ila si kwa umuhimu Naamini kwa kumpa mbinu za ukulima na ufugaji bora huyu ndugu yetu tutakuwa tumejitengenezea ajira za kudumu na kurejesha tabasamu usoni kwa mkulima huyu na hakika thamani ya kila mmoja itarejea.

Mimi ninayejifunza kila siku,
Mwl. Demitria T. Gibure.
Hongera sana
 
This is amazing Ms Dimetria. Good job.
 
Back
Top Bottom