Exaud J. Makyao
JF-Expert Member
- Nov 30, 2008
- 1,518
- 24
Hivi kumbe A.Mashariki ina nchi hizi..!Sioni vijana (kati ya miaka 20 - 30) wakipata nafasi muhimu katika siasa za nchi zetu za Afrika.
Kwa kuzimulika nchi za Afrika Mashariki TANZANIA, KENYA na UGANDA,sijui ukweli ukoje hapa wakuu.
Natoa hoja.
vijana ni wavuta bangi....................................
source: mh. wasira
Mkuu PakaJimmy,Vijana wanafaa kutumikia taifa lao kwa kaajili ya nguvu walizo nazo zaidi, lakini si kwenye ngazi za juu za maaamuzi, MAANA HUKOWATAKOROGA.
Ni ukweli uliositirika kwamba maamuzi mengi ya vijana yana mwelekeo wa jazba na uharaka usio na maana!
Ukiamua kuingiza vijana kwenye ngazi za maamuzi, lazima wawe na back-up ya nguvu kabisa ya wazee.
Ukiona Mbunge kijana sana ujue kwamba amechaguliwa na kundi la vijana wenye hasira ya maisha, ambao wanadhani kijana mwenzao atawaelewa hatraka na kuwasaidia.
My take-
Vijana wawe groomed kushika nafasi za uongozi, na si kutoka masomoni au uraiani direct na kuwa viongozi. Mifano ni kama ya akina JK, ambao wamekulia kwenye Siasa!
WABEROYA,Exaud, thanks for bringing this into our attention
To be honest, vijana hawana mpango na siasa in real life, wengi tunaishia kulalamika kuandika
But the same vijana wahamasishaji wazuri kabisa wa michango ya harusi!!. Kijana akimaliza chuo kapata kazi Zain na ka take home kake ka laki sita, CRDB wakimpa mkopo wa gari , utamtaka??
Kuridhika ndio kumetuponza, na katika dunia ya survival of fittest na ubepari achilia mbali ubinafsi, jamaa wanaitumia nafasi hiyo hiyo kutuburuza.
The situation is even worse kwa graduates wetu, they simply hate politics starting form their respective colleges, ukitaka ushahidi uliza uchaguzi kwa mfano wa DARUSO-udsm ni wanafunzi wangapi huwa wanapiga kura?
Miaka ya zamani vijana kwa mfano vyuoni ndio walikuwa mstari wa mbele katika kila kitu ikiwamo kuleta productive challenges kwa serikali
Exaud nadhani inabidi uombe sana mpendwa!
WABEROYA,
Kwa mawazo haya, nasikitika kwanini vijana wamekuwa na image hii.
Hii ni sawa kweli au kuna mahali vijana wameharibiwa?
Kwa maelezo haya,Tumeridhika, hakuna shida Tanzania. Ni nchi ya maziwa na asali! na hakuna wa kufumbua macho haya mpaka upate shida halau ndio Tunailaumu serikali.
debate hamna mashuleni, viongozi hawana inspiration kwa wanafunzi, maprofessor pia hawana mvuto, mtu ku-waza leo awe kama Kikwete si ataugua kichaa, Lakini kuwaza uwe leader kama akina Obama ni rahisi kuliko JK!
Dhana ya zidumu heshima za mwenyekiti nazo zimeliangamiza taifa, viongozi hawana uwezo wa kukaa na ku-debate na wanaowaongoza, kila kitu amri, na maamuzi yasiyo husisha jamii. viongozi kwa kifupi ni watawala. Kwa namna hii huwezi ukampata kijana anayetamani ku-challenge na kuwa challenged ila kutawala. na kutawala ni function ya kuwekwa mahali bila hata idhaa ya watu. au kuwadanyanaya watu kutumia umaskini wao wa fedha.
kuna sababu nyingi I guess, ila kubwa ni kuridhika
BEN, WABEROYA,Mkuu Waborya umenena,
Mtizamo hasi wa jamii pia unachangia vijana wa age kati ya20 hadi 30 kuwa katika siasa.
Pia,vijana wanajua kujiingiza ktk siasa ktk umri mdogo ni hatari na ni kujiharibia maisha
pia,vijana wengi hawajiamini na mara nyingi wanakatishwa tamaa,hili hapa nina experience nalo kabisa
Ila natoa tamko,mimi kiama mim huu mwiko nitauvunja.Bungeni kunahitajika vijana sana...siasa si sehemu ya kwenda wastaafu.
Sioni vijana (kati ya miaka 20 - 30) wakipata nafasi muhimu katika siasa za nchi zetu za Afrika. Nafasi nyingi za juu za kisiasa zimekaliwa na wazee walioshiba miaka.
Sioni vijana (kati ya miaka 20 - 30) wakipata nafasi muhimu katika siasa za nchi zetu za Afrika.
Nafasi nyingi za juu za kisiasa zimekaliwa na wazee walioshiba miaka.
Hii ina maana kwamba vijana hawana uwezo kuongoza siasa za nchi zetu?
Kuna watu hudai kuwa vijana hawana hekima ya kutosha katika kufanya maamuzi makubwa ya kitaifa.
Kwa kuzimulika nchi za Afrika Mashariki TANZANIA, KENYA na UGANDA,sijui ukweli ukoje hapa wakuu.
Natoa hoja.
Vijana wenyewe unaowasema wako wapi???? Hawa wanafiki wanaojifanya kuipinga serikali kwa majina ya bandia kumbe hakuna lolote. Kazi kuloloma tu ooh hiki hakiendi hivi ooh hiki vile, hakuna lolote. Njaa tu inasumbua vijana wa kibongo, hata ukipewa nafasi utakuwa kama hao wengine tu. Nyinyi ni WANAFIKI. Nchi hii imeshauzwa. Vijana mlie tu, labda baba yako awe na yeye matawi ya juu, kama walivyo kina Hussein Mwinyi na Ridhiwani Kikwete vinginevyo nyinyi mbuzi tu!
Mtaishia kuandika andika upuuzi tu humu. Hamfiki kokote. Hamko Makini, Mamluki mnatumiwa tu.
Mabingwa wa kulalamika. Kuanzia sasa Nawapuuza!!!!!!!!
Twajifunza kuwa chachu ya mabadilko hutokana na mgandamizoo katika jamii..Mfano ubaguzi afrika kusini, ukoloni afrika, ubaguzi USA, ukabila Kenya, Mauaji ya Halaiki Rwanda...etc.
Tanzania mgandamizoo wetu ni upi na uko kwa kiasi gani katika kundi lipi na lenye mbinu zipi katika UPAMBANAJI DHIDI YAO????
Vijana wa Tanzania twahitaji mgandamizoo sahihi na kwa hakika tutaamkaa na kukumboa taifa letu toka kwa wanyonyaji Viongozii..
BEN, WABEROYA,
Sasa nini kifanyike?
Tuwaache wazee washike hatamu tu siyo?