Sweveboy_tz
New Member
- Jul 14, 2021
- 2
- 4
Tumekuwa tukilalama kuhusu changamoto ya ajira na kazi inayo wakabili vijana ambao ni kundi kubwa kuliko yote Tanzania. Imethibitishwa kuwa wastani wa umri wa Kijana kwa sasa Tanzania ni miaka 17.7.
Wengi wamekua wakihoji kama tumetanabaisha maana ya hizi takwimu na jinsi gani kama taifa tumejitayarisha kuendana na wimbi hili la vijana.
Wengi pia wamekua wakitoa angalizo la hitaji kubwa la mapinduzi ya mfumo wa elimu yatakayo hakikisha mitaala inatayarisha vijana kwa kuwapa elimu itakayo wawezesha kushiriki kikamilifu na kuwa washindani kwenye soko la ajira la sasa.
Kabla sijaangaza zaidi kwenye hili naomba kutanguliza kwanza msisitizo wa rai ya kuangalia fursa zilizopo kwenye kila changamoto tunayo kabiliana nayo. Ajira hazitoshi NDIO, takwimu zimethibitisha hivi kwa kuainisha kuwa idadi ya ajira imezidiwa na idadi ya vijana wanaoingia rasmi kwenye soko la ajira (wanaofikisha umri wa kujiajiri au kuajiriwa pamoja na wahitimu wa ngazi mbali mbali za elimu).
Hata tukisema tuangalie ajira zisizo rasmi kwenye sekta mashuhuri, maendeleo endelevu yanaendelea kuwa changamoto kwani ajira hizi zinatoa riziki ya mkono kwenda mdomoni tu yaani ‘hand to mouth’ na hivyo kuacha nafasi duni sana za kuzingatia mahitaji mengine ya kibinadamu na kijamii.
Ni kutokana na sababu hizi ndio maana tunaendelea kuwa na mzunguko wa umaskini kwenye jamii na kaya nyingi Tanzania kwani kunakua na muendelezo wa hali duni kutokana na kushindwa kuongeza ungwe ya fursa za kujiendeleza kwenye nyanja mbali mbali za kimaisha.
Hata hivyo Tanzania tumeweza kuona vijana wengi wakipambana na hali zao kwa kutumia fursa hizi hizi zilizo kwenye ajira zilizo rasmi na zisizo rasmi.
Ingawa kumekua na kilio cha uhaba wa fursa, vijana wamejiongeza kwa kutumia ubunifu na uvumbuzi unao wawezesha kutengeneza bidhaa na kutoa huduma mbali mbali kwenye jamii.
Karne ya 21 imekuja na changamoto ya kipekee kwani ni ya ulimwengu mzima inayo julikana kama ‘automation of work’ yaani teknolojia na jinsi ilivyo athiri kazi na ajira za watu. Nafasi nyingi za kazi zimeondolewa kutokana na uwezo wa mashine na teknolojia mbali mbali zilizo vumbuliwa kurahisisha uzalishaji wa bidhaa na huduma kwenye viwanda na makampuni.
Ingawa wengine wanaweza kudai Tanzania hatutakiwi kuwa na wasiwasi bado; ni ukweli usiopingika kuwa kwa dira yetu ya ‘Tanzania ya Viwanda’ na wawekezaji wa kimataifa tunao wapata lazima mashine zitachukua kazi za aina fulani fulani kwani hamna mwekezaji ambaye kama ana uwezo atafumbia macho teknolojia ya kisasa inayoweza kumpa ahueni kwenye gharama za uzalishaji kwa kupunguza gharama za nguvu kazi.
Pamoja na teknolojia kurahisisha uzalishaji na kazi nyingi, tafiti zimeonyesha kuwa hii ‘automation of work’ inakuja na fursa zake pia, kwani mashine haiwezi kuwa binadamu hata siku moja hata ipewe uwezo kiasi gani. Kuna ambavyo ‘robots’ hawawezi kufanya vikiwemo kuwa na utu wa kibinadamu (empathy) ambayo inahitajika kwenye kazi zote.
Kuna nafasi pia za kazi mpya zinazokuja kama fursa kwenye mapinduzi haya ya kiteknolojia zinazo hitaji ufanisi wa binadamu na hulka zake. Ndio maana sasa hivi kampeni za kimataifa sasa zinahamasisha kuhusu ujuzi na maarifa ya karne ya 21 yaani Soft Skills ambazo sasa zinaitwa Power Skills kwani kila kampuni na taasisi zimeziorodhesha kama lazima kuwa navyo ukitaka kuwa mshindani kwenye soko la kazi na ajira.
Ubunifu kwa upana wake unaweza kuwa ndio mkombozi wa wale ambao wako kwenye mfumo rasmi wa elimu na wale walio ishia kuwa mabaki ya mfumo wa elimu Tanzania; ambao bahati mbaya sana kutokana na mfumo na jinsi tulivyoweka mazoea, wanachukua masomo ya ufundi kama mbadala. Cha kujikumbusha ni kwa Taifa linahitaji taaluma na ufundi wa aina mbali mbali ili kuweza kuendelea kiuchumi.
Ambaye ni daktari, lazima afungiwe mabomba ya maji na fundi bomba, na wote wawili yabidi kujisitiri kwa nguo zilizo shonwa na fundi nguo. Ni mfumo iko wa uzalishaji na maendeleo ya jamii. Tunategemeana na hatuwezi kupata maendeleo tunayo yataka kama tusipoenda pamoja na kutoacha mtu nyuma.
Kumekua na ubunifu mbalimbali unaotumiwa na vijana kuzikamata fursa tajwa hapo juu, wengine wakithubutu kuunganisha majukwaa ya kidijitali na vijana wenye ujuzi na maarifa mbali mbali kama soko la kuwanadi na kuwapa ajira.
Cha msingi kama Jamii ni jinsi gani tunawaangalia na kushirikiana nao hawa vijana kwa kutumia huduma zao. Kumbuka hata wale manguli walianza na kazi moja ikawapa uzoefu, vijana wetu wanahitaji kupewa nafasi.
Fursa nyingine zilizopo sasa ambazo vijana wanaweza kuendelea kutumia ubunifu lakini katika ‘urasmi’ ni utamaduni wa kiuchumi yaani ‘Cultural Economy’. Tanzania tumejaliwa na mtaji wa kiutamaduni mkubwa sana ambao umetuwezesha kuwa kati ya nchi za kiafrika zinazo fanya vyema kwenye sekta ya utalii. Sekta hii pia imetajwa kuwa kati ya zile sekta 6 zilizo ainishwa kwenye mpango wa maendeleo ya taifa FYDPII.
Vijana wanao uwezo mkubwa sana wa kurasimisha kazi mbali mbali ambazo tayari zipo kwenye sekta hii ikiwa ni chachu ya kuendeleza uchumi wa kiutamaduni. Kuanzia wachoraji, wabunifu mavazi, sanaa na muziki hadi matamasha; vyote hivi ni fursa za ajira na kazi kwa vijana kama tukiviangalia kwa jicho la vyanzo vya ajira.
Muziki tu umeonyesha jinsi gani unaweza tumika kama chanzo cha ajira rasmi kwa vijana wetu hadi kuwaona kwa mfano wanao nufaika na kulipwa kwa kazi zao kuonyeshwa mtandao wa YOUTUBE, na wale vijana waigizaji tunao waangalia kwenye chanel zilizopo kwenye ving’amuzi vya kimataifa. Uchumi wa kiutamaduni, unaonadi na kuendeleza tunavyo vipenda kwenye utamaduni wetu unaweza kuchangia sana kupunguza kilio cha ajira na kazi kwa vijana.
Ushiriki wa kwenye Michezo pia ukiendelezwa na kupewa ushirikiano na uwekezaji wa kisera na miundo mbinu unaweza kuwa chanzo kingine kikubwa cha ajira na kazi kwa vijana wetu ndani na nje ya nchi. Mtanambe wa vilabu vya Simba na Yanga pekee umeleta jukwaa linaloweza kutumika kwa fursa zake mbali mbali. Tutumie michezo tupate Mbwana Samatta wengine 25,000, tupate Hasheem Thabeet wengine 30,000 watakao tumia michezo kama ajira. Vilabu na mashirikisho mbali mbali ya michezo iache ukiritimba, ubinafsi na rushwa na ijikite zaidi kuendeleza vijana na kutengeneza fursa za kipato na ajira kupitia michezo hii.
Innovation yaani Uvumbuzi sio matumizi ya teknolojia tu, ni namna mpya ya kufanya kitu kwa ufanisi na matokeo makubwa zaidi. Tunaweza kuvumbua vingi sana tukiacha kuangalia kila kitu kwa muktadha uliozoeleka, matabaka na kudharauliana kutokana na kazi zilizopo.
Kilimo cha jembe na hata cha trekta kimeshindwa kuwapata vijana, wengi wanaishia kukimbilia mjini kwasababu ya urahisi na matabaka na manufaiko ya kazi tuliyo jizoesha kama jamii. Kilimo kama kiini cha uchumi wa Tanzania kinashindwaje kuwa chanzo endelevu chenye maslahi mapana kwa vijana kama nguvu kazi ya taifa? Tunakwama wapi?
Ubunifu, uvumbuzi, ujuzi na maarifa vinajengwa na elimu rasmi na isiyo rasmi. Yatosha kusema kwamba imefika wakati tuache lawama ya upande mmoja na kujiangalia kama jamii na nafasi ya kila mmoja wetu kwenye hili swala, ukizingatia sisi ndio wadau wenyewe kwenye mfumo iko. Tuanze ngazi ya chini kabisa kwenye jamii, ngazi ya kaya kabla hatujafika kwenye mfumo na serikali au sekta ya umma na binafsi.
Je, unalea Fundi bomba wa kesho atakaye vumbua mfumo wa kipekee wa bomba utakao wezesha matumizi salama zaidi ya maji? Umemtayarishaje au kumpa ushirikiano gani kuendeleza ujuzi huu?
Je, unalea mchoraji ambaye ana uwezo wa kuwa mashuhuri zaidi ya Vincent Van Gogh? Umetambua kipaji na uwezo wake na unampa ushirikiano gani?
Je unalea mtoto anayeweza kufungua simu au radio na kuiunda upya? Je kama anaweza kuwa na kipaji cha kuunda kifaa kipya kabisa? Umetoa ushirikiano gani kumuendeleza?
Je unalea mtoto anayetoa mapishi ya aina yake huku kila siku akiangalia recipe/njia tofauti na kujaribu viungo ambayo wewe usingetumia na bado akatoa chakula cha kiwango cha kimataifa? Umetambua kipaji chake? Au ndio mapishi sio kazi rasmi? N.B wapishi ni kati ya wafanyakazi wanaongoza kulipwa vizuri kimataifa.
Nihitimishe kwa kusema kwamba elimu, ubunifu ,ujuzi na maarifa kwa vijana ni jukumu letu WOTE kama jamii. Kuanzia mazingira wanayo kulia, hadi fursa mfumo unao watengenezea. Pale tutakapo tambua hili bila shaka tutatambua mchango wa kila mmoja wetu katika kupunguza janga hili la taifa la ajira kwa vijana.

Upvote
7