SoC03 Vijana na ushiriki katika shughuli za mitaa/"nzengo"

Stories of Change - 2023 Competition

Jerry Farms

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2022
Posts
202
Reaction score
167
Nzengo ni nini?
Kwa mujibu wa kamusi ya mtaani! Nzengo ni jumuishi ya eneo /mtaa aghalabu ukihusisha kaya taklibani 50, lenye mpaka wa kiutawala ukiwa na wakazi wa kudumu na wakuhama hama( wapangaji) na wakiwa na katiba, uongozi na tamaduni/ sheria ndogondogo zina zoongoza shughuli za kila siku katika eneo hilo. Shughuli zoote hizi huratibiwa kwa ukaribu na uongozi wa serikali ya mtaa na ofisi ya mkuu wa wilaya katika mkoa husika.

Kadri siku zinavyokwenda taratibu hizi zimekua zikipuuziwa siku hadi siku hivyo kupelekea kwa kiasi kikubwa mmomonyoko wa maadili katika mitaa yetu. Je, n mara ngapi umehudhuria msiba ukaona ni watu wachache wakishiriki! Vikao vya mtaani kwako je nawe ndugu huhudhuria pasi na kukosa ama na wewe ni mmoja wapo wa watu "waliotingwa" na shughuli za utafutaji hivyo huna muda!!!

Watu wengi wameanzisha zoea hili baya la kutojua umuhimu wa kujiunga na vikundi (kuringana na mgawanyo wa Mtaa/Nzengo husika aghalabu kikundi cha wamama na kikundi cha kina baba kila moja likiwa na majukumu ya kuratibu taratibu kubaliwa kufatwa katika mtaa husika kwa jinsi husika. Zifuatazo ni baadhi ya faida ya mwanchi kujiunga katika kundi moja wapo katika uongozi wa mtaa wake.

Uratibu wa shughuli zinazohusisha umma katika mtaa.
Matukio yanayohitaji uhusishwaji wa umma huratibiwa kwa urahisi kama tu katika eneo husika kuna uongozi imara wa mtaa. Mfano matukio kama ya misiba, mikutano na shughuli za kiserikali.

Ulinzi na usalama
Kwa kuwatambua wananchi woote katika nzengo/mtaa ni rahisi kwa uongozi wa mtaa kumtambua kila mmoja mmoja hivyo kuondoa watu wasio na tabia njema katika mtaa wao hivyo matukio kama wizi,udokozi nakadharika kudhibitiwa kwa urahisi. Katika mtaa pakiwa na uongozi imara ni rahisi hata kwa uongozi wa mtaa kuratibu suala la ulinzi shirikishi.

Kutambuana kwa wananchi katika mtaa na kujenga ujamaa.
Katika mikutano ya mitaa, ushiriki wa wananchi huwaleta karibu na hivyo kujenga umoja. Hali hii hurahisisha uendeshaji kwa urahisi na haraka wa matukio yanayohitaji uchangiaji wa nguvu na mali toka kwa mwananchi.
Uwazi na ushirikishwaji wa wananchi katika shughuli za kiserikali.

Mitaa yenye uongozi imara! Wananchi hupata fursa ya kujua na kushiriki katika chaguzi za viongozi wa mtaa, kujadili taarifa za mapato na matumizi ya fedha za miradi mbali mbali katika mtaa na mengine mengi.
Utambuzi wa makundi yenye uhitaji katika mtaa.

Ni kwa kupitia uongozi wa chini, serikali za mitaa na serikali kuu hupata kwa urahisi taarifa za makundi yenye uhitaji katika nzego/mtaa husika.

Pamoja na faida hizi ni kwa nini basi wananchi (vijana kwa wazee) wamekua wagumu kujiunga na uongozi wa mitaa/nzengo katika maeneo yao? Zifuatazo ni baadhi ya sababu zinazopelekea hali hio;
Viingilio vikubwa kujiunga katika vikundi vya kiuongozi katika nzego/mtaa.

Hali hii imeshuhudiwa katika maeneo mengi haswa haswa ya mijini. Vijana na watu wa makamo wamekua wakitoa sababu hii kurasimisha kutojiunga kwao katika uongozi wa mtaa. Wengine hulalama juu ya ada za kila mwezi katika uchangiaji wa mfuko wa mtaa! Shime kwa viongozi katika mitaa kufanya upembuzi na kuja na mipango mikakati ya kuwavuta watu wengi sana kujiunga na uongozi wa mitaa yao.
Kukwepa majukumu.

Katika mitaa shughuli za vijana, watu wa makamo na wazee zimeainishwa. Hivyo baadhi ya watu kwa kuona hilo wanahisi watabanwa pindi wasipotekeleza majukumu yao hivyo kuamua kukaa pembeni.
Kutokutambua umuhimu wa kujiunga katika vikundi vinavyounda mtaa( kundi la kina mama au kina baba katika mtaa).

Kutokua na makazi ya kudumu.
Hili lipo kwa wapangaji, ndugu hawa wamekua wakidai je nikijiunga leo katika uongozi wa mtaa A kesho na keshokutwa nikahamia mtaa B si nitakua nimepoteza michango na stahiki zangu! Elimu zaidi inatakiwa kutolewa kwa kundi hili.

Yafuatayo ni baadhi ya mapendekezo ya jinsi ya kuboresha uongozi wa serikali za mitaa katika ngazi ya chini kabisa ya vikundi vinavyounda nzengo au mtaa katika kata na mtaa.

Kutolewa vipaumbele kwa vijana na makundi maalumu ya watu waliojiunga na wanaoshiriki katika shughuli za mitaa. Mfano katika ajira za muda mfupi serikali kuu iwe inaenda moja kwa moja katika uongozi wa mtaa husika na kuchukua watu toka huko. Hili litapunguza mianya ya watu kuajiliwa kwa kujuana na hivyo kuwavuta wengi kujiunga katika nzengo.

Ada na viingilio kupunguzwa
Baada ya upembuzi yakinifu, mitaa itakayo gundulika kuwa na ada kubwa na masharti magumu kwa wananchi wake ibadiri ( kwa kukubaliana wananchi wenyewe) juu ya vikwazo hivyo.

Wamiliki wa nyumba kurazimishwa kuwasajili wapangaji wao katika ngazi za uongozi wa mitaa. Hii itapunguza matukio yasiyofaa katika eneo husika.

Elimu ya umuhimu wa kujiunga na vikundi katika mtaa.
Hapa ofisi za serikali za mitaa kwa kushirikiana na wajumbe/mabalozi wawezeshwe na kutoa elimu juu ya umuhimu wa jambo hili kwa wananchi wao.

Mabadiliko binafsi
Kila mtu ajenge tamaduni ya kupenda kuwajibika katika shughuli jumuishi za mitaa mfano kushiriki katika vikundi vidogo vidogo vya kiuongozi katika mtaa( vya kina mama,baba na vijana).
 
Upvote 2
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…