Vijana tuache kubweteka, tujiulize biashara yenye mtaji mdogo

Vijana tuache kubweteka, tujiulize biashara yenye mtaji mdogo

Jukwaa limejaa watu wa uelewa wa mambo mbalimbali ngoja waje tuvune maarifa.
 
Tatizo siyo Mtaji, je una Courage ya Kufanya Hizo kazi za Mitaji midogo.. maana Biashara hizo wengi wa Vijana Mkishaziona Mnaona Mnajidhalilisha ,halafu biashara siyo lazima uanzishe wewe zingine zimeshaanzishwa so Join

1. Nenda Kaoshe magari na Pikipiki Maswala ya Kuelewana mtajuana na Boss mnalipanaje kwa Kila Gari unaloosha kama ni Tsh 2000 kwa kila Gari inamaana ukiosha magari 10 una 20 per day

2. Tembea Mtaani Na Bodaboda kama Day worker halafu Then tafuta Mkataba wa Boda unaendesha miezi kadhaaa baadae inakuwa yako

3. Tengeneza Vitafunwa Mfano Vitumbua Then Sambaza Kwenye Vibanda vya Vyakula kwa Bei ya Chini kidogo mfano kama kitumbua ni 300 wewe kawauzie 250...
 
Tatizo siyo Mtaji, je una Courage ya Kufanya Hizo kazi za Mitaji midogo.. maana Biashara hizo wengi wa Vijana Mkishaziona Mnaona Mnajidhalilisha ,halafu biashara siyo lazima uanzishe wewe zingine zimeshaanzishwa so Join

1. Nenda Kaoshe magari na Pikipiki Maswala ya Kuelewana mtajuana na Boss mnalipanaje kwa Kila Gari unaloosha kama ni Tsh 2000 kwa kila Gari inamaana ukiosha magari 10 una 20 per day

2. Tembea Mtaani Na Bodaboda kama Day worker halafu Then tafuta Mkataba wa Boda unaendesha miezi kadhaaa baadae inakuwa yako

3. Tengeneza Vitafunwa Mfano Vitumbua Thai en Sambaza Kwenye Vibanda vya Vyakula kwa Bei ya Chini kidogo mfano kama kitumbua ni 300 wewe kawauzie 250...
safe sana
 
Kwanza kabla ya kutafta biashara jibadilishe kisaikolojia....amua kweli kufanya biashara....biashara ya mtaji mdogo kwangu nnayoweza kkushauri ni kuuza vocha/vifurushi plus kusajili laini

Tembelea matawi ya mitandao hasa voda na tigo wakuunge tigorusha....vodarusha....plus upewe code ya usajili kwa mitandao yote

Tafuta location....angalia sehem ambyo utauza kweli

Weka kila laini ya vifurushi elfu 10...jumla elfu 20

Laini ya mitandao mingne weka buku 10

Chukua laini kwenye mabaranch ya mtandao husika

Andaa meza na mwamvuli anza kazi

Faida ya tigorusha ni 6%(kwa elfu 10 unapata 600)
Vodarusha 8%(kwa elfu 10 unapata 800)

Hapo bdo hela za kwenye vfurush plus ya usajili mwsho wa mwezi
 
Vijana wa sasa tumejawa Umwinyi sana. Una Iphone ya laki 8 unalalama huna mtaji, kutwa kucha vibegi mgongoni, headphone maskion, suruali mlegezo kwenda kutazama wenzenu wanavyofanya manunuzi Mliman City maninaaaaa.
Fanyeni kazi muingize kipato huo utozi mtaishia kufumuliwa marinda.
 
Hii biashara ya kusajili laini,kuuza vifurushi(voda na tigo) na Uwakala(Tigo Pesa na M-pesa) inalipa sana haswa ukituliza akili..kwasasa namiliki mtaji mkubwa kiasi na pia nimenunua pikipiki na kuitoa kwa mkataba wa mwaka mmoja NB:-nimeianza mwaka jana
 
Back
Top Bottom