SoC04 Vijana tuamke kuleta chachu ya maendeleo

SoC04 Vijana tuamke kuleta chachu ya maendeleo

Tanzania Tuitakayo competition threads

luqmtu

New Member
Joined
Jun 25, 2024
Posts
1
Reaction score
0
Vijana ni nguvu kazi katika taifa lolote duniani haswa katika mataifa yaliyoendelea, kama vijana wa eneo fulani au taifa fulani wakijituma vizuri hata sehemu au taifa hilo litapiga hatua.

Kuna umuhimu mkubwa sana kwa vijana wa Tanzania 🇹🇿 kuamka katika usingizi na ndoto mbovu waotazo kwani wao ndio msingi mkubwa wa maendeleo kuelekea miaka 5 mpaka 25 katika taifa letu,vijana engine wamekuwa wakishawishika kujiingiza katika makundi yasiyofaa kama panda road, machine sabini na vikundi vingine viovu.

Vijana tunapaswa tuwajibike, ili kuleta chachu ya maendeleo kwa taifa letu kwa 5 mpaka 25 vijana kama nguvu ya taifa tunawajibu wa kuwajibika ili kuleta maendeleo kwenye nchi yetu, tunapaswa kuwajibika kwenye mambo mbali mbali kama ya kiuchumi, kisiasa na kijamii hii italeta chachu ya maendeleo kwa taifa.

Vijana tunapaswa tujue umuhimu wetu,kuelekea miaka 5 mpaka 25 vijana inabidi tujue tuna umuhimu gani kwa jamii na taifa kwa ujumla kukosekana kwa maarifa ya kujitambua sisi ni kina nani na umuhimu wetu ni upi kwa jamii hujikuta tukiingia kwenye mambo yasiyifaa hali inayopelekea taifa kukosa nguvu kazi na wapambanaji.

Vijana tuwe na malengo, miongoni mwa vitu ambavyo hupelekea kiumbe chochote duniani kufanikiwa ni lengo, lengo litakupa hamasa ya kufanya na kuongeza juhudi katika upambanaji ukiangalia taifa letu vijana wengi hawana malengo mfano wahitimu wa vyuo vikuu hukaa majumbani baada ya kumaliza masomo yao huku wakidai ajira hakuna yote ni kutokana hawakuweka malengo ya mbeleni hii ni kutokana na kukosa mipango ya mbeleni hivyo kuelekea miaka 5 Hadi 25 ya maendeleo vijana tuamke kwa kujiwekea malengo tutapiga hatua.

Vijana tuchangamkie fursa,hili ni jambo la umuhimu sana kuelekea maendeleo ya nchi,vijana tuchaangamkie fursa na tuzitumie tunapozipata vizuri kwani vijana wengi tuna uzembe kwenye kutafuta fursa lakini pia tukipata hushindwa kuzitumia ipasavyo kuelekea mchakato wa miaka 5 hadi 25 ya maendeleo vijana tuamke kwa kutafuta fursa na kuzitumia inavyopaswa hii italeta chachu ya maendeleo kwa taifa.

Vijana tuelimike, hii pia itasaidia kuleta chachu ya maendeleo, sehemu yenye vijana wengi ambao wameelimika na wakatumia vizuri elimu zao huleta manufaa kwa jamii hiyo, vijana wa Tanzania 🇹🇿 inabidi tuelimike na kutumia vizuri maarifa yetu hiyo itapelekea kupata fursa na kuwa kwenye vitengo mbali mbali kama nguvu kazi ya taifa tunao mfano wa vijana walioelimika na wanatumia vizuri elimu zao kama Jokate Mwigero,Shaka Hamdu Shaka na wengine wengi ambao wanatuwakilisha vyema.

Mbali na hayo ya vijana kuamka pia jamii nzima ya Tanzania 🇹🇿 inapaswa kujua maendeleo ni watu na watu hao ni watanzania hivyo basi tunapaswa kufanya mambo mema na mazuri leo yakaleta manufaa kesho kwa vizazi vijavyo tunapaswa tuwe na umoja, amani, mshikamano na upendo ili tuendelee.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom