SoC01 Vijana tupasapaswa kujikita zaidi katika uwajibikaji ili tuweze kuepukana na vishawishi vinavyoturudisha nyuma kimaendeleo

SoC01 Vijana tupasapaswa kujikita zaidi katika uwajibikaji ili tuweze kuepukana na vishawishi vinavyoturudisha nyuma kimaendeleo

Stories of Change - 2021 Competition

ItsMi

Member
Joined
Sep 13, 2021
Posts
66
Reaction score
31
Habari ya kwako ni tumaini langu upo poa kabisa.

Naomba kwa wasaa mwingine tupate kuelimishana sisi kama vijana ambapo tunategemewa kulijenga taifa bora hapo miaka kadhaa ijayo.

Katika kipindi cha ujana watu wamekuwa wakikutana na vishawishi vingi tofauti tofauti ikiwa ni lengo la kutimiza haja za miili yetu na akili zetu vile zinavyowaza.

Katika kipindi cha ujana mwili unakuwa umekamilika katika nyanja zote ambapo akili inakuwa imebadilika pia tofauti na kipindi cha mwanzo sasa katika hali hii vijana walio wengi huanza kujifunza mambo mbalimbali kwa hiari ya mwili hata kwa kuiga wengine kwa kuona kwamba amekuwa mtu mzima sasa ambapo labda anahisi anaweza kufanya lolote huku akisindikizwa na akili yake pamoja na uchochezi wa malezi mabovu, utandawazi, sambamba na usawa wa kimazingira uliopo.

Sasa mara nyingi tumejikuta tukizisikiliza hisia zetu na kuzitimizia haja zake bila ya kutathimini kwamba ni yapi madhara ya kufanya haya nnayoyafanya na badala yake wengi hawawekei maanani katika hilo na matokeo yake wengi wao wanaharibikiwa mapema wakiwa vijana.

Hivyo ikiwa sisi ni vijana tunapaswa kutambua kwamba yatupasa kuwa mfano bora wa kuigwa na jamii kwa kuyaepuka mambo mbalimbali ambayo ni vikwazo katika jamii ikiwa ni pamoja na:

1. Ubakaji, umalayana ukatili wa kijinsia.
2. Wizi, ujambazi na vitendo vya kiuhalifu.
3. Ulevi na matumizi ya madawa ya kulevya.

Ambapo hali hii itasaidia katika kulijenga taifa ambalo ni bora kwa vizazi vijavyo. Pia sisi vijana inapaswa kujitathimini kujua yafuatayo.

1. Mimi ni nani?
2. Nafanya nini?
3. Malengo yangu ni yapi?
4. Nimetoka wapi na ninataka nifike wapi?
5. Kwa malengo yapi?
6. Kwa njia za namna gani ?

Endapo tukifanya hivyo tutaweza kuyafikia malengo kwa maana kujiuliza maswali kama hayo ni njia ya kujitambua na kufanya mambo tunayopaswa kuyafanyia utekelezaji..

Hivyo pia vijana tukiwa tumejitambua tutaweza kutatua kero mbalimbali zinazo athiri mfumo mzuri wa maendeleo ni kama ifuatavyo.

1. Itasaidia kupunguza mimba za utotoni
2. Kupunguza idafi ya maambukizi katika jamii zetu
3. Itasaidia kupunguza watoto wa mitaani
4. Kupunguza ufungishwaji wa ndoa zisizotarajiwa
5. Pia itapunguza mmomonyoko wa maadili na kurudisha nidhamu kayika jamii zetu.

Kwa hakika elimu ikitolewa kwa jamii na ikapokelewa vizuri tutaweza kuikomboa jamii yetu. sisi kama vijana wa taifa hili tutahakikisha hili linawafikia vijana wengi zaidi ili kujifunza na pia kuimarisha ushirikiano na mahusiano mazuri yenye amani baina yetu katika kuhakikisha tunailinda amani ya taifa letu ili kufikia mafanikio na maendeleo ya taifa. kwa sababu penye amani ndipo maendeleo yalipo kwa kuwa vita haijengi bali sikuzote inabomoa.

Ni ombi langu kwa vijana wote kwamba sisi ni vijana na tunalojukumu kubwa na zito kwa taifa hivyo tusiruhusu vishawishi kuja kuharibu ndoto na mipango tuliyojiwekea katika kulijenga taifa la kesho.

Hivyo tunathibitisha kwamba tutakuwa mstari wa mbele kulipigani hili katika kuhakikisha tulifikia lengo.

Asante
 
Upvote 0
Back
Top Bottom