ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 21,643
- 51,642
-Vijana hao hufanya urafiki na wazee kwa nia ya kuiba nywele zao nyeupe
-Vijana hao huchangannya nywele hizo na ‘opium’ inayotengeneza dawa za kulevya na kuvuta dawa hizo zinazowafanya kuonekana wazee
-Wanataka kuwa wazee haraka ili kufaidi kutokana na mgao wa pesa za watu wakongwe kutoka kwa serikali
Wazee walio na nywele nyeupe katika wilaya ya Katakwi nchini Uganda wametahadharishwa baada ya vijana kuwanyoa wazee hao kwa lazima kwa nia ya kupata nywele zao nyeupe.
Inadaiwa kuwa vijana hao ambao wengi wao hawana kazi wamezamia kutumia dawa za kulevya zinazowafanya kuonekana wazee pamoja na kujiwekea nywele za wazee walizoiba ili kuweza kupata pesa kwa watu wakongwe zinazotolewa na serikali ya nchi hiyo.
Vijana nchini Uganda wameripotiwa kuiba nywele nyeupe za wazee ili kutengenza dawa za kulevya zinazowafanya wazeeke kwa nia ya kupata KSh 700 kwa kila mzee zinazotolewa na serikali. Afisa wa mawasiliano katika wilaya ya Katakwi, Oduko, aliwataka wazee kuwa makini na vijana hao ambao ni hatari kwa maisha yao, “Ninawaonya watu wazee kuwa macho na kuwachunguza vijana wanaojifanya marafiki zao kwa kuwa hivi karibuni, huenda watakata vichwa vyeni ili kupata nywele zenu nyeupe,”Oduko alisema.
Kulingana na afisa huyo ambaye pia anahudumu kama afisa mkuu wa kituo cha polisi cha Katakwi Cental, vijana hao huchanganya nywele hizo na ‘opium’ inayotokana na ‘latex’ na ambayo hutumika kutengeneza dawa za kulevya na kuitumia kama dawa ya kulevya.
Oduka alisema kuwa maafisa wa polisi waligundua mbinu hiyo mpya kwenye vikao vya kijamii katika maeneo kadhaa ya wilaya hiyo.
Alisema kuwa vijana walikuwa wakipata nywele hizo kutoka kwa duka za wasusi na wengine walifanya urafiki na wanawake wazee kwa nia ya kupata nywele hizo.
Afisa huyo wa polisi alisema kuwa vijana wao wanatia bidii kwa juhudi hizo ili kupata KSh 700 inayotolewa na serikali kwa watu walio na miaka 65 na zaidi.
“Vijana hao walidai kwa kuwa hakuna nafasi za kazi, ni vyema wawe wazee ili wafaidi kwa pesa hizo za serikali zilizotengwa kwa watu wazee,” Oduko alisema.