ELLY LWITIKO MWASALEMBA
New Member
- Jul 26, 2022
- 2
- 3
VIJANA, USHOGA NA USAGAJI. (HOMOSEXUALITY ADDICTIONS)
Hapo zamani vitendo vya ushoga na usagaji (LGBT) katika jamii za Kiafrika ilikuwa ni aibu na laana kufanya vitendo hivyo kwa kuzingatia misingi ya kitamaduni na imani zetu za kidini. Hali iliyofanya vijana wengi hata wazazi kuogopa kuongelea habari hizi, lakini hivi Leo mijini na vijijini vitendo hivi vimekuwa wazi kabisa na si vya kuogopeka kama ilivyokuwa awali. Hali iliyopelekea hata baadhi ya watu kujitangaza hadharani na kupigania haki za washiriki wa mapenzi ya jinsia moja.
Umoja wa mataifa, mashirika ya haki za binadamu na wanaharakati mbalimbali wameibuka na kulivalia njuga suala hili, LAKINI HII SI ASILI YETU AFRIKA. Vitabu vitakatifu na Imani zetu za dini mbalimbali zinapinga vitendo hivi kuwa vipo kinyume na maagizo ya mwenyezi Mungu.
Visababishi; vinasaba vya mwili, kutokuwa na hofu ya Mungu, kukaa mda mwingi bila shughuli,matumizi ya madawa ya kulevya, ukatili wa kingono, kutazama video za utupu, marafiki, malezi ya wazazi, maendeleo ya sayansi na teknolojia n.k, hivi vyote vimepelekea vijana kuwa waraibu wa mambo hayo.
Madhara yake; kujichukia mwenyewe na kujishusha thamani (matatizo ya kisaikolojia), kuwa mtumwa, kutengwa na jamii unapogundulika, kuchangia mmomonyoko wa maadili na kuihalalisha dhambi, kutumia mda mwingi kwa mambo yasiyo na tija, kusambaa kwa magonjwa mbalimbali na umasikini.
Pia imechangia changamoto nyingi kijamii, kiuchumi na kisiasa katika nchi zetu.
Kijamii; jamii imeshaanza kulichukulia hili jambo kikawaida, Hali inayopelekea vijana wengi waingie katika janga hili. Teknolojia kupitia filamu mfano filamu ya I am Samuel, simu janja na mitandao ya kijamii imekuwa ikichochea zaidi hii hali ya kusambaa na kupelekea kuzalisha kizazi hatari katika Miaka ijayo. Mfano raisi Biden wa Marekani amemteua Karine jean-pierre kuwa msemaji wa wapenzi wa jinsia moja na mtu wa kwanza mweusi katika wadhifa huo.
Kisiasa; baadhi ya viongozi na mashirika ya nchi za magharibi yamekuwa yakiunga mkono jitihada za kupata haki kwa washiriki wa mapenzi ya jinsia moja, mfano: Marekani, UN, HRW na WMA . Pia nchi baadhi za Afrika zimekuwa zikilazimishwa kuunga mkono jitihada hizo hili zipatiwe mikopo na misaada mbalimbali, tarehe 28/9/2015 raisi aliyepita wa Zimbabwe (Robert Mugabe) aliliambia shirika la umoja wa mataifa (UN) “we are not gays”, pia amewahi sema “worse than pigs and dogs” katika kuupinga ushoga.
Kiuchumi; Nchi baadhi zimekuwa zikiwekewa vikwazo vya kiuchumi na nchi za magharibi kwa kutokuunga mkono jitahada hizo, mfano Uganda imekuwa ikilazimishwa kupitishwa mswada wa mapenzi ya jinsia moja, pia Tunisia na Lebanon walisitisha vipimo kwa mashoga baada ya Human right watch (HRW) na WMA kupinga vikali. Hivyo vingine vinaweza kuonekana ni sawa kwa kihaki lakini si sahihi.
Tufanye Nini vijana tulioathirika? ; LAZIMA tufanye maamuzi yenye nidhamu na endelevu ya kuamua kuacha na kutounga mkono kabisa. Pia kumrudia Mungu maana yeye ndiye anatupa neema ya kuushinda uraibu huu, kupata ushauri wa kisaikolojia, kutotengeneza mazingira ya kushiriki kwa namna yoyote, kuchunguza marafiki, kuwa muwazi kwa mtu unaemwamini hili usaidiwe, kuepuka kutokuwa na kazi ya kufanya na kutamani kuona kizazi kinachokaa mbali na changamoto hii. Shetani anafanya tuone dhambi ni kitu Cha kawaida katika fikra zetu.
Serikali ifanye nini? ; Iwe makini katika masharti ya mikopo na misaada mbalimbali inayotoka katika nchi za magharibi hili kujenga jamii bora yenye maadili mema na hofu ya Mungu. Pia serikali itoe msimamo thabiti kuhusu hili jambo hili kulinda kizazi kijacho, mfano serikali ya jamhuri wa muungano wa Tanzania ilijitenga na sakata la aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam P.Makonda la kupinga ushoga hili kulinda mikataba ya kimataifa.
Pia serikali kwa kushirikiana na viongozi mbalimbali wa kidini na mashirika yasiyo ya kiserikali waunde taasisi ambayo itafanya kazi ya kuwashauri, kuwalea na kuwasaidia watu walioathirika na janga hili kama inavyofanyika kwa watu walioathirika na madawa ya kulevya (SOBA HOUSE) kwa njia itakayo kuwa salama zaidi. Pia taasisi hiyo itoe elimu kwa vijana pamoja na wazazi katika umuhimu wa kujilinda na janga hili kwa maendeleo ya kizazi kijacho.
Jamii ifanye nini? ; wazazi, walezi na viongozi wa kidini hawana budi kusimama kidedea kupinga jambo hili na kutoa malezi bora yatakayo wajenga vijana katika mfumo wa maisha wa kiafrika na si kizungu kama tunavyoona kinachotokea kwa wazazi wengi hasa wenye uwezo wa kifedha kwa kuhisi hayo ndiyo malezi sahihi. Wazazi na walezi watengeneze ukaribu, urafiki na vijana hili kujua changamoto zao mbalimbali na si kama alivyosema kiongozi mmoja wa kidini kuwa “Ikiwa mtu anashiriki mapenzi ya jinsia moja na anamtafuta Mungu kwa nia njema, mimi ni nani nimhukumu?”, Hatuhukumu lakini Nia yetu ni kujenga kizazi kilicho salama.
Pia wazazi wasisite kuongea na vijana kuhusu ushoga na usagaji hili kujenga uelewa juu ya janga hili na siyo kama wengi wanavyodhani kuwa kujadili mambo Aya ni kuwapeleka vijana Katika matatizo zaidi.
Vijana ambao hatujaathirika tufanye Nini? ; Ni kuhakikisha vijana wenzetu wote wanaotuzunguka wako salama katika janga hili, na tuwashauri na kuwahudumia kwa upendo na umakini mana wengi wao hawapendi Hali hii na wanashindwa kabisa kuacha. Hivyo maneno mabaya, lawama na laana hazitawasaidia kutoka walipo zaidi ya kuwagandamiza. Kwasababu wapo wengi ambao hawaifurahii Hali hii lakini pia wakitaka kujinasua hawakutani na mazingira yaliyo salama kwa usiri wa maisha Yao. Wanahitaji upendo, neema ya Mungu na matibabu ya kiakili kama wagonjwa wengine hili waweze kujinasua kwenye janga hili.
Pia wapo vijana wanaopenda, hawataki kuacha na wengine wamefanya jambo hili kuwa kama biashara, ambayo ni harari sana kufanya mambo maovu na kuyachukulia kama ni maisha yetu ya kawaida ya kila siku. Tukubali mabadiliko japo yatahitaji nguvu na sadaka za kila kitu chetu.
TUSIMAME KWA PAMOJA KUUONDOA USHOGA NA USAGAJI HILI TUJENGE TANZANIA NA AFRIKA ILIYO NA SALAMA KIMAADILI.
By E.L.M
0767862610.

Attachments
Upvote
3