Kuna fala m'moja kipindi hicho nipo form one, alinipa hii kitu bila kunipa angalizo lolote. Nikaichukua nikaiweka ulimini badala ya nyuma ya lips halafu muda huo huo nikatema ili kujiokoa kumbe ni too late kitu ipo tayari kwenye mfumo wangu kupitia yale mate niliyomeza.
Kosa kubwa nilifanya ni kumeza mate. Mara mbili so dakika zilizofuata kilichonikuta ndio sababu naandika hapa hii komenti.
Nilikichezea kimbunga cha Kuber hadi nikasema kimoyo moyo na alaaniwe aliyetengeneza haya makitu ili watoto wa watu waumie hivi.
Yaani kizungu zungu si kizungu zungu, pressure kupanda sijui, muda mwingine unaona kabisa inchi inapatwa na tetemeko la ardhi ila wewe pekee yako ndio unalisikia kwa nguvu, mixer kuna muda unahisi kuna kundi la nyuki linakufuata ila hauwaoni, mara usikie ving'ora vya gari ya wagonjwa halafu vinapotea ghafla, tena usikie kengele ile ya ringi la gari inalia mtaa wa nyuma. Hapo mwili ni wa baridi ila utasikia Joto la hatari aiseee unavua shati unatamani kubakia na boxer tu.
Ile vita sitakuja kuisahau. Nikakosea nikaenda home baada ya kuona hali inakuwa tete si nikachukua chai kwenye chupa nikaweka na kahawa sasa sijui ili iweje nikiamini itanipa ahuweni. Yaani kichwa chote nakisikia Ziiiiiiiiiiiiiii. Nikanywa chai funda kadhaa. Weee nilitapika chakula chote cha mchana.
Nikaenda kulala kimya chumbani maana sikutaka kuraise maswali mengi endapo wangejua nini kinaendelea. Nikaingia nikaweka miguu ukutani nikalala huku kimoyo moyo nasali rozali na kutubu dhambi zote maana nilikuwa nahisi nikilala hapa naweza nyoosha hii kitu ni zaidi ya sumu.
Dah nashukuru MUNGU nakuja kuamka ni asubuhi mapema siku ya pili. Tokea siku hiyo nikawa nikinusa harufu ya kuber au harufu ya Udi fulani hivi unaofanana na Kuberi nahisi kutapika.
Kuber matako yako.