Vijana wa CHADEMA wana uwezo mdogo sana

CCM wajanja sana ukiwa upinzani wanakushawishi uhame kwa bashasha na visenti,ila wakitimiza lengo unakuwa kama kondom vile hawana time na wewe unabaki chakula tuu kama hivii!
 
Tangu nimejiunga ndani ya CCM, nimepata fursa ya kufanya tafiti na kugundua tofauti kubwa sana kati ya viongozi, wanachama na hasa vijana ndani ya CCM na wale wanaotoka vyama vya upinzani, vikiongozwa na CHADEMA.

Unamaanisha tangu ulivyotoka CHADEMA au ulishajiunga CCM kabla ya kujiunga CHADEMA?

Lakini hali hii inatokana na mfumo wa Chama Cha Mapinduzi ambao umejikita katika malezi na mafunzo kwa vijana wake kupitia jumuiya yake ya vijana (UVCCM) ambayo imejibainisha kuwa ni tanuru la kuoka viongozi wa chama na Serikali.

Hawa viongozi walotufikisha hapa tulipo?????? Are you serious???


Unamaanisha kuongeza maarifa ya kuiba fedha za umma, ujambazi, uuaji na ufisadi au?

lakini pia, Vijana wa UVCCM wana matumaini zaidi kuliko Vijana wa Chadema na wapinzani wengine, leo vijana wa Chadema na Wapinzani wanatamani wangekuwa CCM ili wanufaike na fursa za kupata maarifa na kujengewa uwezo, ndio maana akina Yericko Nyerere, Ben Saanane na wengineo wanafanya kazi za wagombea wa CCM kwa kuwa wamepoteza matumaini na viongozi wao kwenye vyama vyao.

Uwezo mdogo wa vijana wa chadema unajidhihirisha kwenye CV zao, kwani wengi ni mangumbaro wasio na elimu ya kutosha
, lakini pia maneno wanayoandika kila kukicha katika jukwaa hili yanadhihirisha uwezo wao mdogo, thread za akina Henry Kileo, Tumaini Makene etc zinawavua nguo vijana wa Chadema.

Unaweza tuwekea CV yako hapa tukupime?

USHAURI.

Hamna mwenye akili timamu atakubali ushauri wako (hata walioko kwenye chama(CCM) chako!!!!)

Anyway were you serious when writing this????
 
baada ya kusoma coments zote, mimi kama kijana kuna kitu nimejifunza kwa faida yangu
 
kazi ipo MAGAMBA na UGAMBA wao!!!kweli nimekubali kila mtu hujivunia chake..ni kazi kuusimamia ukweli mama!!! utahongwa mpaka msimamo wa maisha yako!!! ndani ya CCM utaendelea kushika mapembe tu!!!
 
Uwezo mdogo wa vijana wa chadema unajidhihirisha kwenye CV zao, kwani wengi ni mangumbaro wasio na elimu ya kutosha,

bonge la krap.

a day after siku ya wamama duniani na kutana na post ya kijuha kama hii kutoka kwa mwanamke.

aibu yako. unaweza kulieleza jukwaa katika hizo unazoita tafiti umeona connection iliyopo kati ya elimu ya kuunga unga na serikali iliyopo madarakani?
 
Kumbe utawala umewaumiza sana vijana mpaka wenye kutawala wanakiri kuwa wamewaumiza sana vijana ambao ndio nguvu ya Taifa
 
Hiyo masters Degree ni ya miezi mingapi? 2008 - 2008!????
Duh! Mambo ya veta hayo


Pasco,

Umeniudhi sana leo....!


Tatizo ni kwamba tu wasahaulifu sana,hivi wewe mwanamke,nyinyi si ndio mliokataa mapendekezo ya wananchi juu ya wabunge Kuwa na elimu ya angalau kidato cha nne!???then unajivua chupi hadharani na kufanywa matusi pasipo kujielewa unaposema umepata elimu bora baada ya kuingia uvccm,hebu twambie huko uvccm umehamia ukiwa na elimu gani,na elimu hiyo uliipata ukiwa chama gani,na je,baada ya kuhamia uvccm ulianza darasa la ngapi,na ulikuwa unasoma kwa mitaala ipi?ni hii hii ya elimu yetu,au kuna mingine inayopatikana huko uvccm??
 
Last edited by a moderator:
Nimesoma sayansi ya Jamii, nilipoamua kujiunga na CCM na kusomea sayansi ya jamii nilijua Tanzania ina watu wa aina yako ambao wanahitaji ukombozi.

Ulisomea sayansi ya jamii na ulifaulu kabisa?
Ina maana CCM wametuharibia elimu kiasi hiki? Nimekugoogle kuona kama utafiti wako umepublish popote sijaona kwa sababu ningeshangaa kama kuna journal ingeweza kuaccept paper yako. Yaani binti ana degree ya sayansi ya jamii halafu uwezo wake ndo huu?
Juliana umenipa sababu nyingine ya kuichukia CCM. Sikuchukii wewe kwa sababu CCM wamekuaminisha kuwa una degree, na wewe bado ni mtoto ukaamini.
 

mkuu kweli umeona mbali sio kama mtoa mada ambavyo hakufikiria hao vijana chanzo cha kuwa hivyo nin?
 
VIJANA wa CHADEMA bado ni wadhaifu sana katika akili na mwili. Kila ninapoandika jambo katika forum hii huwa hawana hoja bali ni matusi tu. Ni tamaduni iliyojengwa ndani ya Chadema, vijana wanatumiwa katika mambo ya hovyo na hawaandaliwi kwa ajili ya kukiokoa chama wakati ambapo kinawahitaji vijana wenye maarifa na uwezo.
 
Dada fanya juhudi, ukuu wa wilaya haunaga muda, unaweza pewa wakati wowote
 
Hivi Zitto ambae ameibua kashfa ya Buzwagi na Escrow na madudu mengine y Serikali ni Kijana wa Chadema..???

Huo ni ufahamu wako au ni ufahamu wa viongozi wako pia..?
Kamuulize Zito wakati anaaibua hayo alikua chama gani?na ni chama gani kilichomlea na kumkuza kisiasa mpaka nawewe ukamjua ukaanza kujpendekeza kwake kabla miguu chemba hajakutwaa
 

Ok naweza nikawa sikubaliani na ulichokibandika hapa; lakini ninapashwa kuheshimu haki yako ya kukibandika; au sio!
Red highlite katika bandiko lako ni kutambua kwamba wewe ni mtafiti; that said nilitegemea sana hapa kwenye bandiko lako kichwa cha habari kiwe supported na takwimu au vielelezo vitikanavyo na comparative study yako hiyo; hakuna! utafiti sio Ngwini (Penguin) per ce; lazima uonyeshe takwimu pia na viambatisho vya mifano halisia ili kuhakikisha huachi nafasi ya msomaji wako kuwa na wasiwasi na utafiti wako kwa sababu na yeye akienda kulinganisha kwenye primary sources ataridhika!?

Hukufanya hivyo sana sana summary yako umepersonalise utafiti wako na kuwapiga washindani wako bellow belt blows!, na mwiso kabisa a sorry political statement! nakunukuu: "Uwezo mdogo wa vijana wa chadema unajidhihirisha kwenye CV zao, kwani wengi ni mangumbaro wasio na elimu ya kutosha, lakini pia maneno wanayoandika kila kukicha katika jukwaa hili yanadhihirisha uwezo wao mdogo, thread za akina Henry Kileo, Tumaini Makene etc zinawavua nguo vijana wa Chadema"

Angalia sana utafiti is a science; unapoanza utafiti ambao conclusion yake ni predetermined; hiyo sio sayansi tena ni RAMLI! and mind you "Psychophancy is a form of metal ill-health!"; lisaidie jukwaa hili kwa tafiti za kisayansi sio ushabiki wa kiitikadi pekee au Ramli.
Unawashutumu wenzako hawana Ilimu ya kutosha! lakini na sisi pembeni tunapata ukakasi kidogo na upeo wa Elimu yako the accuser?! Kumbuka "when you point one finger at your opponent you have three pointing back at you! and one for the sideliners and passersby watching and very curious?! upo hapo; maisha ndivyo yalivyo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 

mfano mama angalia matokea ya form 4 yalipoanza kuwa mabaya,serikali hii ikaona bora ishushe division ndio wataokoa jahazi,kumbe hawakuwa na fikra za mbali,kuwa ndio wanazidi kuuwa taifa la baadae,na niserikali hihii ya ccm, sasa hapo nikuwadanganya watanzania kuwa wanaelimu kumbe mnazidi kuuwa nchi ili watoto wa hao vigogo wa ccm wanaosoma nje ndio waje kututawala kwa kuwa wao ndio wenye elimu bora.
 

Hahaha
 
Kijana kjutumiwa kama dakio ndani ya ccm unaona ndio kugundua fursa na kupewa nafasi,chama kilichopasuka makundi makundi ni vigumu sana kwa kijana mwenye kujitambua kujisifu kuwa yumo ndani ya chama hicho na kuwashangaa walio nje ya chama makundi.Hivi leo kila mwenye akili timamu anatambua bayana kuwa hakuna kitu kinachoitwa ccm tena kuanzia kwenye maadili,utetezi wa wanyonge mpaka kwenye sera.Chama kilichoitwa cha wakulima na wafanyakazi leo viongozi wamekuwa watu wa kukiri hadharani matumizi ya rushwa ndani ya chama ili kupata uongozi halafu kijana unajiona mjanja kuwa ndani ya chama hicho.

Wewe Juliana Shonza na mwenzako Mtela mnajijua na pengine mnajuta ndani ya mioyo yenu kusaliti CHADEMA hasa mkiona jinsi Chama mlichokisaliti kinavyofanikiwa kuunganisha vyama vingine chini ya UKAWA na sasa umoja wao unagawa dozi inayowaacha ccm hoi dhofu lihali mpaka mnapoteana kila mtu anabwatuka kivyake ndani ya chama,kila mmoja anamuhofu mwenzake.

Hebu tueleze ukweli toka uvunguni mwa nafsi yako wewe uko kundi la nani? Je,uko na Lowassa,Membe,Ngeleja,Pinda,Kigwangala,Wassira au kundi lipi? Mpaka sasa ndani ya chama magamba hakuna mwenye ubavu wa kukirudisha chama kuwa kimoja tena,mwenyekiti wenu alisuswa 2010 akapiga kampeni na familia yake unategemea leo atajihusisha kikamilifu?

Porojo pigeni sana ila ukweli unabaki kuwa mmepotea njia na hakuna namna zaidi ya kujirudi,kukiri mlidanganywa na muombe radhi toka mioyoni mwenu muwe sehemu salama vinginevyo subirini aibu ya mchana kweupe nyie walamba nyayo mkiungana mkono na akina Nape na Makonda.
 
Nawaoneeni huruma mnaosubiri kusomeshwa na vyama vyenu,vijana tunaojielewa tumesomeshwa na serikali chuo kikuu kupitia bodi ya mikopo baada ya hapo tunakimbizana na shilling hatimaye tunajilipia wenyewe kujiendeleza zaidi kwa jasho letu,ndio maana hatuna haja ya kujipendekeza kwa mtu tunabase katika reality tunasema lolote bila uoga.tumeondoa dhana ya utegemezi vichwani mwetu.Wito wangu kwa vijana wote wa kitanzania hata biblia na kuran zimesema itafuteni elimu popote ilipo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…