KERO Vijana wa Mkataba wanateseka sana katika Hospitali ya Wilaya Tanganyika Mkoani Katavi

KERO Vijana wa Mkataba wanateseka sana katika Hospitali ya Wilaya Tanganyika Mkoani Katavi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Nikiwa mmoja wa Watumishi wa Hospitali ya Wilaya ya Tanganyika nashauri Mkurugenzi wa Halmashauri awalipe vijana wanaojitolea pesa zao ili kuhudumia taasisi, wanakaa hadi miezi miwili bila posho kidogo, inayohitajika kadri ya miongozo.

Wanaumia sana namna ya kujikimu wanapanga nyumba, kodi tatizo, chakula tumechoka kuwakopesha wasaidie wapate pesa zao inaumiza sana.

Hali hii inapoteza ufanisi wao kufanya kazi wengine kuondoka kabisa hali inapelekea kazi nyingi ukizingatia hospitali haina watumishi wa kutosha.

MKURUGENZI AULIZWA
JamiiForums
ilipomuuliza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, Shaban Juma Juma kuhusu maelezo hayo ya Mdau amesema “Sijaona suala hilo mezani kwangu lakini nitalifuatilia.”

 
Tatizo ni kubwa na ndio ..wanaangukia changamoto ya mahusiano ya bila kutaka ili tu mambo yaende
 
Back
Top Bottom