fakalava
JF-Expert Member
- Jul 16, 2015
- 4,459
- 6,027
Wanabodi,
Ni wazi kabisa kuwa kwa sasa ndani ya CCM mambo siyo swali kutokana na upepo wa Kampeini inayotumia.
Kwa sasa CCM wamekwishajua kuwa itakuwa ngumu sana Magufuli kushinda Urais dhidi ya Lowassa maana wanaona hakuna muujiza wa kuubadilisha upepo, ukiacha Ngamia kupita kwenye tundu la sindano zamu hii hata muujiza wa kumpitisha sungura haupo.
Hii hali imewafanya wakate tamaa kuanzia ile team ya campaign mpaka vijana wa mtandaoni wote wamekata tamaa na kuona kazi wanayoifanya haina maana na haitasaidia chochote.
Pamoja na kwamba anguko la CCM lilitarajiwa lakini si kwa ukubwa tunaouona kwa sasa.
Miongoni mwa sababu zilizochangia kuiporomosha CCM kwa speed ya Kimbunga ni:
1. Kutumia muda mwingi kufanya Kampeini za matusi wakimshambulia mgombea wa UKAWA, huku wakisahau kuzinadi sera zao.
2. Kuteua team ya Kampeini yenye uwezo mdogo, fikiria timu ambayo Kampeini manager ni Bulembo pia humo humo yumo Asampta Mshama, ni dhahiri hii timu haiwezi kuleta ushindi.
3. Hili anguko la CCM Mkapa anachangia pakubwa kwa matusi anayoendelea kuporomosha, kwa matusi aliyoyaporomosha pale Jangwani hakupaswa kupewa nafasi tena kusimama jukwaani, juzi kawaambia wanaume wanaotaka mabadiliko wanataka wabebe mimba kama wanawake.
4. Kitendo cha Magufuli kukiponda chama na kuwaponda Viongozi waliopita kuwa wamekiharibu chama, na yeye akichaguliwa kuwa Rais atafumua mfumo mzima wa chama na mfumo mzima wa Uongozi wa nchi.
Kwa ujumla haya maneno yamewakasirisha na kuwachukiza wengi ndani ya Chama, kwa maana Magufuli anazinadi sera zake binafsi badala ya kuinadi Ilani ya CCM.
Hizi ni sababu chache miongoni mwa sababu nyingi zinazokwenda kuiangusha CCM.
Tukutane 25-Oct 2015, naendelea kukinoa kichinjio changu.