Vijana wa UKUKU na Demokrasia ya Kenya

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Just to make records clear kwa vijana wa UKUKU. Kwa akili zao ndogo wanadhani kutenguliwa kwa matokeo ya uchaguzi ni ushindi kwa Raila. Huu ni ushindi kwa demokrasia na utawala bora ambayo ni falsafa anayoiishi Rais Uhuru Kenyatta kwa vitendo. Rais Kenyatta ni mfano wa kuigwa ktk demokrasia barani Africa. Mara ngapi chaguzi zinafanyika nchi mbalimbali Afrika (ikiwemo Tanzania) na kunakua na "irregularities" nyingi lakini matokeo yanazuiwa kuwa challenged mahakamani?

Hapa kwetu kuchallenge matokeo ya Urais mahakamani ni "dhambi". Matokeo ya Urais hayapaswi kuhojiwa popote. Viongozi wa Afrika wamejigeuza "miungu watu". Kenyatta amevuka kiunzi hicho ambacho viongozi wengi wa Afrika (akiwemo JPM) wamekishindwa.

Kuna watu watasema ni issue ya Katiba. Ofcoz ni matakwa ya Katiba bora ya Kenya. Lakini Katiba bora bila viongozi bora wa kutekeleza ni kazi bure. Viongozi wa Afrika wamezoea kusigina Katiba bila kuhojiwa popote. JPM anasigina Katiba anavyotaka na hakuna anayethubutu kumchallenge. Kwahiyo hata Uhuru angeweza kusigina Katiba akaapishwa kama ilivyo desturi ya "madikteta uchwara" wa Afrika, and nothing could happen.

Lakini Uhuru akasema no. Akaamua kuheshimu Katiba. Uhuru anaamini kuwa Katiba ya Kenya ni kubwa kuliko yeye, anaamini Katiba ya Kenya ni sauti za wakenya. Hapa kwetu kuna mtu anaamini Katiba ya nchi ni kitu cha "hovyohovyo" na hata alipoilizwa Katiba mpya vipi, alisema "yuko busy na kunyoosha nchi kwanza". Uhuru anaamini ktk "independence" ya mihimili mitatu ya dola. Hapa kwetu kuna watu wanaamini mhimili mmoja umechimbiwa chini kuliko mingine.

So kwa ujumla Kenyatta ameonesha "maturity" ya juu sana katika demokrasia na utawala bora. Amefanya hata ambayo wazungu wasingeweza kufanya.

Nampongeza sana Uhuru kwa "maturity" hii kubwa ktk demokrasia. Nakipongeza chama changu Chadema kwa kumuunga mkono muumini wa kweli wa demokrasia kama Uhuru. Najivunia kumuunga mkono Uhuru.

Natabiri ushindi wa kishindo kwa Uhuru Kenyatta katika uchaguzi wa marudio hapo October 31. Naamini hata watu waliomnyima kura awali, sasa hivi wamepata kila sababu ua kumpigia kura na kumuombea kura. Uhuru ameprove ambayo wengi hawakutarajia. Hongera Kenya, hongera demokrasia. Kila la heri Uhuru.!

Credit Malisa GJ
 
Kama Kenyatta na timu take wasingefanya madudu naamini hata shauri lisingefika mahakamani.

Mtu anasababisha mabilioni ya pesa za walipa kodi kupotea kwa marudio ya uchaguzi kwa sababu ya kuchakachua uchaguzi halafu unampongeza!

Huu ni ujinga au upumbavu wa kiwango cha juu!
 
aigwe kwa kuchakachua au vipi mkuu. Angekuwa ni wa kuigwa hayo yaliyotokea wenda yasingekuwepo. hakuna ushindi hapo zaidi ya exposition ya mbinu chafu za ushindi ambazo zinatakiwa kukemewa
Kwa ufupi waafrika wote tuko chini ya vizio vya demokrasia.
mbona hueleweki
 
Bado tunaendelea kung'ang'ania kumuunga mkono alieumbuliwa na mahakama,hiyo katiba ambayo ingeruhusu rais kupingwa mahakamani si ndio iliosiginwa na lowassa akishirikiana na sumaye,sitta!
 
Eti huyu nae ndip great thinker wa chadema

......
 
Wizi ni wizi tu hata tukiupa jina lipi zuri, huwezi kutegemea kuiba ili uwe Rais, tujikite kwenye utendaji kazi kama kigezo cha kuwa rais,si katai asiwe rais bali ashinde kwa halali ili hata nchi zingine za Africa zijifunze, huwezi ukawa president generated by BVR ukanishawishi umekomaa kidemokrasia. Ingawaje nawapongeza Kenya especially mahakama kwa hatua nzuri na uwazi waliofikia, sasa msisema katiba ililetwa na uhuru, kwa Tanzania kikubwa vyama vya upinzani + ccm waungane wote kutaka katiba mpya.
 
Uchaguzi haurudiwi kwa sababu kura ziliibiwa ila kwa kuwa tume haikufuata katiba na sheria za uchaguzi za Kenya. Sasa watu wasio aidha na uelewa au ufahamu wanapotosha sababu za mahakama kufikia maamuzi ya kufuta matokeo hayo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kabisa mkuu hii dhana ya wizi wa kura sijui inatoka wapi maana mahakama imesema tume haikufuata taratibu za kisheria kuwashilisha matokea kutoka majimboni na kwingineko kwenye sehemu husika....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…