SoC04 Vijana Wakitanzania Wapewe Nyumba za Kuanza Maisha

SoC04 Vijana Wakitanzania Wapewe Nyumba za Kuanza Maisha

Tanzania Tuitakayo competition threads

MAISAKI

Member
Joined
Apr 10, 2012
Posts
9
Reaction score
5
Binadamu wanamahitaji makuu matatu - chakula/kinywaji, mavazi na makazi. Nyumba sio anasa, bali ni moja ya mahitaji muhimu yanayochochea amani na utulivu, ukuaji wa kiuchumi pamoja na heshima katika jamii. Moja ya fahari kubwa sana ya kuwa Mtanzania ni pamoja na kumiliki nyumba, yaani kujenga. Kuna msemo mmoja maarufu unasema “kata simu, tupo site” ambao umeenea mtaani na kukubalika.

20240630_235417.jpg

(Nyumba zilizojengwa na Mr Beast, Jamaica)

Watanzania wote wanatamani kumiliki Ardhi, kuanza ujenzi na kuishi kwenye nyumba zao yaani kuepukana na kulipa kodi. Kwa mujibu wa takwimu za FSD Tanzania, moja ya sababu kubwa 3 ambazo watu huwa wanazo wakikopa au kutunza pesa ni kwa ajili ya ujenzi wa nyumba (ya kwanza ni kuwa na ukwasi na ya pili ni kuwekeza).

Katika kipindi cha mwaka 2017 hadi 2021, watanzania wanakopa kwa ajili ya mahitaji mbalimbali, asilimia 3% (2017) na 4% (2021) kwa ajili ya ujenzi au ukarabati wa nyumba. Hii ni ongezeko dogo sana ukilinganisha na matumizi mengine kama gharama za maisha, matibabu na dharura zingine ambapo wastani umekuwa kutoka 23-30%, 18-24% kama zilivyoorodheshwa.

Bajeti ya Tanzania ni Trillion 49.35 ambapo bajeti ya wizara ya Ardhi ni 450.83 bilioni, hii ni sawa na asilimia 0.91 ya bajeti nzima. Mwanzoni, wizara ilipangiwa bilioni 163.17 na kuomba nyongeza ya 172%, yaani 287.66 bilioni. Hii inamaana kuwa wizara hii haitiliwi mkazo kama zingine. Ukiangalia mapato yanayo tokana na wizara pia ni madogo, kwani kwa 2023 lengo ilikuwa wakusanye bilioni 300 ila wamekusanya 136 bilioni (45.3% ya lengo). Chanzo kikubwa cha mapato ni pamoja na kodi ya ardhi, ambapo asilimia kubwa ya ardhi ya Tanzania bara haijapimwa. Hii inasababisha migogoro mingi na kufanya watu wajishauri sana kabla ya kununua Ardhi ili wajenge nyumba.

Upatikanaji wa fedha za kujenga, ambapo zinahitajika nyingi - kwa Watanzania wengi hutumia kujenga taratibu huku wanadunduliza, kuchukua mkopo au kupiga pesa za biashara haramu na kujenga ndani ya muda mfupi. Kwa mujibu wa takwimu za TMRC, March 2024 - mikopo imeongezeka kutoka ukuaji wa 4.65% Desemba 2023 hadi 11.38% March 2024. Shirika la makazi bora (Habitat for Humanity Tanzania) limeeleza kwenye jarida lake zaidi ya 70% ya watanzania hawaguswi na mikopo hii kwani inahudumia wa kipato cha juu & kati tu.


Katika kipindi chote cha serikali ya awamu ya 5, hakuna shirika lolote lililobuni mradi mpya wa makazi ya watu. Yote walikuwa muendelezo wa kazi za serikali zilizopita, taasisi za umma zinazoshikilia pesa za wananchi zilielekezwa zijenge viwanda kwani majengo ni tembo weupe. Hii ilisababisha uhaba mkubwa sana wa nyumba, kwa watumishi wa serikali, binafsi na wananchi kwa ujumla.

Tunahitaji tanzania inayoweza kutoa makazi kwa mtu anayeanza maisha, aweze kulipa kodi kidogo kidogo na mwisho kununua nyumba hiyo. Hii itainua uchumi kwani kipato kile kitapelekwa kwenye uwekezaji badala ya ujenzi wa nyumba ambao unasumbua sana familia. Kipaumbele cha serikali kinapaswa kuwa kupima, kupanga na kurasimisha ardhi ya Tanzania kwani watapata mapato, pia wataepusha migogoro.

Tukiangalia nchi za Afrika zilizopiga hatua kubwa kipindi cha nyumba kama Libya, serikali ilikuwa inatoa nyumba kwa wananchi wake. Kuongezea ni kwamba miundombinu za barabara na usafiri inabidi iboreshwe ili watu waweze kufika kwenye makazi yao kwa wakati na bila kuharibiwa magari yao. Takwimu zilizopatikana mwaka 2010 na utafiti wa Chama cha Viwanda Tanzania, zinasema kuwa Tanzania inapoteza 20% ya mapato yake kwa foleni za barabarani na ajali. Kwa sasa idadi hiyo inakadiriwa kuwa mara 1.5 yake kwani idadi ya raia imeongezeka.

Tanzania tunayoitaka ni ile itakayoweka mbele haki za wazawa wa asili, ambao wamekuwa wakiishi katika makazi hayo kwa muda mrefu kiasi kwamba mila na tamaduni zao zinaingiliana naArdhi ile. Hatukatai maendeleo lazima yaje, lakini yapaswa kutumia majadiliano na sio silaha katika kufikia muafaka wa matumizi ya ardhi na maendeleo ya makazi.

Swali kubwa ambalo sisi raia, na vingozi wetu tunapaswa kujiuliza ni kwamba Maendeleo yanafuata watu au watu wanafuata maendeleo? Dira ya taifa ya 2050 lazima ikubali kwamba maendeleo yanapaswa yachagizwe na serikali, yaani barabara, maji, maji taka, mtandao, upimaji wa viwanja unaanza; halafu watu wanasogea kuweka makazi na si vinginevyo ili kuepusha mkanganyiko na migogoro mingi. Naitamani Tanzania ambayo hakuna kijana anayeanza kuingiza kipato, awaze kujenga na kununua gari kwanza. Serikali inatakiwa kuwa na mfumo mzuri wa upatikanaji wa huduma hizi ili kipato kiende kwenye kuwekeza, kutunza na kutumia kwenye mahitaji mengine. Inawezekana! Tanzania ambayo vijana kuanzia 30 watakabidhiwa nyumba za kuanzia maisha.

Haya ni mambo 10 serikali inatakiwa kufanya na kuweka katika mipango yake ya Dira 2050.

1. Sera ya Nyumba na Makazi

2. Mkopo wa Kiwanja ambao utakuwa kwenye Tozo ya kila muamala unaofanywa kwenye simu, bank ya raia

3. Wawezeshe bank ikopeshe nyumba kwa riba ndogo zaidi, na wadau wengi zaidi wafungue microfinance ya nyumba. Hii inawezekana kupitia TMRC

4. PPP yaani serikali na mashirika binafsi kushirikiana kufanya miradi ya nyumba nafuu, nyumba za wahitaji maalum & nyumba za wanaofanyiwa ukatili (domestic violence shelter homes, affordable homes & special needs home)

5. RERA & EAB iundwe kupitia muswada ambao umekuwa ukisubirishwa & kufanyiwa maboresho tangu 2017. RERA ni Real Estate Regulatory Authority & EAB ni Estate Agency Board. Muswada hiyo unaweza kuiona hapa
View: https://t.me/hamiahapa/146?single

6. Matumizi ya Technolojia kwenye miradi ya nyumba za serikali ili kusaidia Rent-to-Own, Mortgage & Rent. Mfano mifumo ya access control kwamba mtu akilipa anaweza kuingia, asipolipa mlango unajilock. Analipia nyumba kama kifurushi cha dish 😀. Pia teknolojia za smart homes zitasaidia kutunza nishati, maji & kusaidia wataalam wa ujenzi kujenga nyumba zinazokidhi mahitaji ya watu.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom