Wapo vijana wengi mitaani wenye elimu nzuri tu na uadilifu kuliko hata waalimu. wako mitaani hawana kazi ya kufanya kwa sababu Serikali yao haiwatumii. Zipo kazi nyingi tuu kama vile za NIDA kuwapatia watanzania vitambulisho hadi leo hakuna kitambulisho' Zoezi la SENSA vijana hawa wangetafutwa wakapewa semina wanaweza kufanya hii kazi vizuri sana hata kuingiza data kwenye Kompyuta. Lakini hakuna wa kuwasemea japo wanajulikna wapo. Waalimu tayari wana Ajira yao. Kwa nini kuwapa kazi nyingine wakati wanatakiwa wawe kazini. Yaani serikali inaona bora shule zifungwe waalimu wapate kazi hii ili wasigome. Poleni vijana wa Tanzania.