Vijana waliozaliwa kuanzia Miaka ya 90 ndiyo watakomboa hili taifa

Vijana waliozaliwa kuanzia Miaka ya 90 ndiyo watakomboa hili taifa

BIG THINKER

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2018
Posts
680
Reaction score
1,436
Hiki ndicho ninachokiona Mimi na ukikaa peke yako ukatafakari hili BANDIKO utakubaliana na Mimi Hawa vijana wametuzid sana sisi tuliozaliwa Mika ya 89 kurudi nyuma wengi wetu vichwa vyetu havina kitu zaid ya kuwa machawa kama akina mwijaku, baba levo na doto magari Hawa wote wamezaliwa Miaka ya 89 kurudi nyuma.

Angalia watoto wa 90's sasa wanavyotusua Kila Kona hawa jamaa wakikaa wanafiti kwenye mziki vijana wa 90's ndiyo wameleta mabadiliko mfano diamond mpatinum chib de, hamonize nk

Hata kwenye UTAFUTAJI nimeshuhudia vijana wengi wa 90's wanaingia mjini Hawana kitu ila baada ya muda wanakuwa na chawa wa Miaka ya 80's sisemi hakuna wa 80's wasiotusua wapo sema ni wachache wengi Wana mali za kurithi.

Tukija kwenye siasa hii nchi imeongozwa na sisi wa Miaka ya 80's kurudi nyuma na hakuna makubwa tuliyofanya zaid ya kupigana vikumbo na kusagiana kunguni hatuna mwelekeo wa maana hata katiba mpya imetushinda tunabaki tunalalamika tu, ila nawaamin vijana waliozaliwa Miaka ya 90's lolote wanaweza kufanya na hao ndiyo wataibadilisha hii nchi siyo sisi.

Hata hili sakata la MUUNGANO sisi wazee tunaoujua na kuukumbatua MUUNGANO siku tukitoka Duniani Hawa vijana wakakalia viti MUUNGANO kwa heri make ukiongea nao wengi hoja za MUUNGANO hawakubaliani nazo.

Vijana mliozaliwa Miaka ya 90 hadi Sasa ndiyo tegemeo pekee la hii nchi na ndiyo watatuletea katiba mpya sisi wengine acha tuendelee kuufyata.

Haya vijana uwanja ni wenu
 
Mimi nimezaliwa 90 s

Kwaandiko lako basi naona kila kizazi huona chenzie ni bora.

Tangu nimezaliwa nimekiona kizazi cha mwisho cha kisiasa mwaka 2010 kizazi cha kina joshua nasari ambao bila shaka ni 80's tangu hapo wanao pambania taifa hili hi hao hao akina Slaa, Mbowe, Zitto, Sugu, Mpina, Jussa n.k

Hakuna jipya kwa sisi mitoto ya 90. Hawa wa 2000 ndo wamekuwa vilaza hatari kadri tunavyozidi kwenda mbele ndo tunatengeneza taifa la wajinga tu. Ajisemee mama mmoja mkazi wa lagos ni mwanachama wa ACT hili taifa atakae kuja kulikomboa hajazaliwa bado ama yupo shuleni.
 
Kama kijana wa 90's naunga mkono hoja
#nitakuwa wa kwanza kuukataa Muungano
#Nitaidai katiba kwa gharama zote
#Nina uchungu na Tanganyika yangu,mizee wakati wenu umepitia tulichokiona kwenu mikataba ya kimangungo na ufisadi,na limuungano bovu
 
Sema hzi kamali ndiyo zinatuharibia vijana wetu, kucha kutwa wanabeti, huu ni kama mtego watawala wameuweka kwa hiki kizazi japo Kuna na wazee wa 80 Bado wanashinda wakibeti
 
Hahaha wakati kizazi hicho kishapotezwa
Kizaz hicho chote wanataka kukata mauno,kuwa waimba mziki,kizaz hicho wamejiwekeza sana kwenye burdan,umbea nk
Kizaz cha 90 kishapotezwaaa

Ova
Na maroli model wao ni kina mwijaku, juma lukole na baba level
 
mimi ndio huyo mwenye hekima sikuwa nijue leo unanifanya nijione mwamba but all in all sina kitu mamaq
 
Hicho kizazi cha miaka ya 90s maana yake Unazungumzia kizazi cha vijana ambacho kwa sasa kiko busy kubet, kukesha hapa JF kwenye nyuzi za kula tunda kimasihara, kusaka connection, kutafuna mirungi na pombe kwa kwenda mbele, kupost mapicha ya ovyo instagram, kubishana mambo ya simba na Yanga, kutafuta watu wa kulea, tuma kwa namba hii nk.
Hivi hicho kizazi kinaweza kukomboa taifa? Mmh! Sijui.

Kifupi hicho ndio kizazi cha kwanza cha ovyo kupita maelezo, kukifuatiwa na vizazi vingine vilivyofuata.
 
Kizazi cha dhahabu
images (15).jpeg

Sio hawa
IMG-20230628-WA0022.jpg
 
yani hao ndio watachukua machawa na mafisadi hatari.. we ingia tu kwenye serikali za vyuoni ndio utawajua..wanafisadi hadi hela za kutengenezea vimbweta
 
Back
Top Bottom