Vijana wanaumwa maradhi gani?

Vijana wanaumwa maradhi gani?

ipogolo

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2011
Posts
6,280
Reaction score
5,979
Wanabodi,habari za Jumatatu! Tukiwa tumeianza wiki kuu kwa ajili ya hitimisho la kipindi cha Kwaresma, jana Jumapili( Matawi) nilipigwa na butwaa. Nikiwa mmoja wa waumini niliyehudhuria ibada hiyo, niliona waumini wengi vijana wakiwa wameketi wakati wa kipindi cha Injili.

Kwa desturi Injili husomwa na kasisi waumini wakiwa wamesimama. Injili ya Jumapili hii ya matawi ilikuwa ndefu kidogo( DKK 30). Vijana wengi walikuwa wameketi hoi taabani.
Watu wazima umri kati ya miaka 45 kuendelea mbele walikuwa ngangari wamesimama wakifuatilia Injili.

Je, Vijana Afya zinagomba? Hawapendi kusimama?

Namwaga ubwabwa.
 
Kama ni kinyume na matakwa ya Kanisa wewe kama muumini ambaye unajiona umetukukuka ulichukua hatua gani?
 
Hapo si ni dar ? ,kama ni dar ndio kawaida yao,,kama ni mkoani basi katoka dar

All in all,mkuu vijana sikuiz vijana sisi wavivu
 
Tatizo kubwa ni kwamba vijana wanafanya shughul ngumu zinazo wa-oversize
 
Kama ni kinyume na matakwa ya Kanisa wewe kama muumini ambaye unajiona umetukukuka ulichukua hatua gani?
Kusimama wakati injili ikisomwa ni takwa la kikanisa.
Watu wenye umri mkubwa wangekaa ningedhani ni sababu ya umri wao.
Vijana kushindwa kusimama dkk 30 ni dalili ya nini?
 
Hapo si ni dar ? ,kama ni dar ndio kawaida yao,,kama ni mkoani basi katoka dar

All in all,mkuu vijana sikuiz vijana sisi wavivu
Ni kweli Dar na kimenishangaza. Sisi Iringa sioni hayo! Vijana wa Dar kama wanaume wa Dar.
 
mkuu mawazo yako yalikua kutizama vijana kuliko kuckiliza somo
Haihitaji akili sana. Ukiwa umekaa viti vya nyuma utaona mbele pasi na shaka.
Macho yalitazama lakini masikio yalisikiliza.
 
tatizo ni idara ya liturujia ya kanisa katoliki ijipanue iwafundishe waalimu wa dini na homilia zizingatie liturujia ili waumini wakumbushwe kila mara.mtu anamshika mkono askofu hajui kazi yake ni kuibusu pete.tulipokuwa kijijini jimbo la moshi miaka ya sitini ukimuona padri popote njiani kwa kuwa walikuwa wanavaa kanzu na msalaba mkubwa unapiga magoti naye anafahamu kuwa ana jukumu la kuwabariki.jambo ambalo limetuwia shetani ni kuwa hao mapadri hata kanzu mitaani hawataki kuvaa.nampongeza sana Ruwaichi wa mwanza.
 
Back
Top Bottom