Wanabodi,habari za Jumatatu! Tukiwa tumeianza wiki kuu kwa ajili ya hitimisho la kipindi cha Kwaresma, jana Jumapili( Matawi) nilipigwa na butwaa. Nikiwa mmoja wa waumini niliyehudhuria ibada hiyo, niliona waumini wengi vijana wakiwa wameketi wakati wa kipindi cha Injili.
Kwa desturi Injili husomwa na kasisi waumini wakiwa wamesimama. Injili ya Jumapili hii ya matawi ilikuwa ndefu kidogo( DKK 30). Vijana wengi walikuwa wameketi hoi taabani.
Watu wazima umri kati ya miaka 45 kuendelea mbele walikuwa ngangari wamesimama wakifuatilia Injili.
Je, Vijana Afya zinagomba? Hawapendi kusimama?
Namwaga ubwabwa.