Vijana wanya viroba msikubali kutumika kisiasa! Katiba imewatambua, tumieni nafasi leo siyo kesho

Vijana wanya viroba msikubali kutumika kisiasa! Katiba imewatambua, tumieni nafasi leo siyo kesho

nyimbag

Member
Joined
Feb 28, 2015
Posts
41
Reaction score
17
VIJANA WANYA VIROBA :mvutaji:MSIKUBALI KUTUMIKA KISIASA!
KATIBA IMEWATAMBUA, TUMIENI NAFASI LEO SIYO KESHO
Katika taifa lolote vijana ni nguzo kuu ya kuleta maendeleo katika jamii husika. Ushiriki wa vijana katika harakati zote za kijamii, kiuchumi na kisiasa ni nguzo muhimu katika ujenzi wa taifa imara la kesho. Tunapowaandaa vijana kwa namna yoyote tunaandaa watu ambao wataweza kuchukua kijiti na kutuongoza wakati tutakapokuwa tumechoka na hatuna uwezo wa kuendesha mambo yetu tena.
Ili taifa lolote liwe imara halina budi kutengeneza mazingira mazuri kwa vijana ambao hatimaye watachukua nafasi za kuliongoza taifa husika. Jambo la muhimu ni vijana kujenga utayari wa kuweza kuutumia ujana wao katika mtazamo chanya na kushiriki katika harakati za kulisaidia taifa.
"Ibara ya 54 (1) Kila kijana ana haki na wajibu wa kushiriki kikamilifu ktk shughuli za maendeleo ya Jamhuri ya Muungano pamoja na jamii kwa ujumla, na kwa mantiki hiyo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano na jamii zitahakikisha kuwa vijana wanawekewa mazingira mazuri ya kuwa raia wema na kupatiwa fursa za kushiriki kikamilifu katika nyanja za kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.
Ibara ya 54 (2) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (1), Bune litatunga sheria itakayosimamia, pamoja na mambo mengine, uanzishwaji, muundo, majukumu na uendeshaji wa Baraza la Vijana la Taifa "
Ni wazi kuwa mchango wa kundi la vijana katika maendeleo na mustakabali wa nchi yoyote ni muhimu sana. Tangu kupata uhuru, Tanzania vijana wengi walijengwa katika misingi ya uzalendo na kuaminishwa katika misingi ambayo inalenga matumizi mazuri ya nguvu za vijana katika taifa la Tanzania.
Mwanafilosifia wa Kifaransa Joseph Joubert akiwazungumzia vijana anasema kuwa ukitaka kujua jambo lolote basi waulize vijana kwasababu wanajua kila kitu. “Ask the young. They know everything”

Lakini mwanafilosofia mwingine, Aristotle Mgiriki huyu yeye anamlinganisha kijana kama kiungo muhimu na cha kudumu katika ujenzi wa Taifa,ambapo anasema „The young are permanently in a state resembling intoxication”.

Hata hivyo, mabadiliko ya kisiasa na kiteknolojia yamebadilisha namna mambo yanavyoenda. Sasa tofauti na zamani, kumekuwa na tofauti kubwa ya kimtazamo. Ni rahisi kubaini kizazi cha sasa kinavyowaza kwa kupitia mitando ya kijamii.

Namna watu wanavyoshiriki katika kuchangia mijadala mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii inatathminisha maono na mawazo waliyonayo vijana katika jamii. Tofauti na zamani, vijana wa sasa wanaonyesha kwa kiasi fulani kutojua wajibu wao katika jamii.

Pamoja na wanasaikolojia na wanazuoni mbalimbali kuutambua umuhimu huo wa vijana. Bado vijana wa maeneo mengi duniani, hususani Afrika wamejikuta wakiingia kwenye changamoto ya kutumiwa na watu wenye nia na dhamira tofauti tofauti. Wakati mwingine vijana hutumiwa kushiriki mambo ya hatari kwa ustawi wao binafsi na wa nchi kwa ujumla.

Umuhimu huu wa vijana kwa mujibu wa wanafilosofia hawa unakuwa kazi bure, kwasababu katika nchi za Afrika nguvu ya vijana walio wengi imeanza kutumiwa na magenge ya wachache na wenye malengo yenye viashiria vya hatari.

Katika nchi nyingi ikiwemo Tanzania vijana wamekuwa wakitumika kutekeleza matakwa ya kisiasa. Wamekuwa wakitangulizwa mbele kunapotokea maandamano au masuala yoyote magumu katika jamii. Ni wazi kuwa hakuna ubaya wa vijana kushiriki kwenye harakati za kisiasa ubaya unakuja pale mtu anaposhiriki katika jambo ambalo halifahamu kwa kina namna atakavyonufaika nalo na wala hajui athari za jambo hilo katika jamii.

Baadhi ya watu wazima ambao wamezaliwa kuanzia miaka 80 kurudi nyuma wanalalamikia uwajibikaji wa vijana wa sasa katika suala zima la ushiriki katika harakati za ujenzi wa Taifa. Wanaona vijana wa sasa kama watu ambao hawajitoi kushiriki katika mambo mazuri ya kuliendeleza taifa la Tanzania.

Kama Taifa tumeshindwa kutumia mianya chanya iliyoletwa na teknolojia ya leo na badala yake tumeendelea kukumbatia pande hasi za teknolojia.

Imekuwa ni jambo la kawaida sana ukipita kwenye kurasa za mitandao ya kijamii ikiwemo ile ya ‘facebook’ na ‘twitter’ kuona watu wakijadili mambo ya kichochezi ambayo kwa hali na mali yanaonesha ni kwa jinsi gani taifa linapoteza mwelekeo.

Ifike wakati sasa pamoja na hamasa za kisiasa, kiuchumi na kijamii zilizopo, tuangalie namna ya kuweka maslahi ya Taifa mbele na kamwe vijana tusikubal kutumika kwenye kueneza chuki na kufanya vitu ambavyo ni kinyume na ubinaadamu ikiwemo kupigana, kuchemeana nyumba au jambo lenye kuashiria matendo yaliyo kinyume na Sheria kwa binadamu wenzetu.
 
duh hatari wanakuny.a viroba?

Msamehe bwani! nafikiri hilo ni kosa la kiuandishi tu, To me I think the writer intended to write "Wanywa viroba". Msamehe bure. Na mhimize atumie muda wake kusoma Katiba Inayopendekezwa ambayo sasa ipo mitaani ili wananchi waisome na wapate ufahamu ili muda muafaka na sahihi ukifika wakapige kura.
 
Duh hii Katiba kweli ni hatari. Imewatambua hadi wanywa viroba!

Hao wanywa viroba nazo waliitwa na Sitta kutoa maoni yake pale Sitta alipojitwikwa dhamana ya kukusanya maoni badala ya Tume ya Warioba?
 
duh hatari wanakuny.a viroba?

Mkuu, hayo ndio Madhara ya kutekeleza kila anachotumwa. Yeye amefanya haraka kukumbilia haraka humu JF kutekeleza agizo la bosi wake, amekimbia haraka kama mtoto huku akiimba ili asisahau alichotumwa.
 
Mkuu, hayo ndio Madhara ya kutekeleza kila anachotumwa. Yeye amefanya haraka kukumbilia haraka humu JF kutekeleza agizo la bosi wake, amekimbia haraka kama mtoto huku akiimba ili asisahau alichotumwa.

Kiongozi kumbe hata ww umewaona wachumia tumbo, wanakurupuka tu!
 
Msamehe bwani! nafikiri hilo ni kosa la kiuandishi tu, To me I think the writer intended to write "Wanywa viroba". Msamehe bure. Na mhimize atumie muda wake kusoma Katiba Inayopendekezwa ambayo sasa ipo mitaani ili wananchi waisome na wapate ufahamu ili muda muafaka na sahihi ukifika wakapige kura.

Ni kweli kabisa mda ukifika wapige kura ya hapana!
 
Ni kweli kabisa mda ukifika wapige kura ya hapana!

Hayo ni mawazo yako, usipende kuwalisha watu maneno yako ili wafuate maamuzi yako. hapa tuelimishane na tuangalie vifungu mbalimbali kuliko kurudia rudia maneno yako unayopenda wewe kuyasikia na hupendi kusikia ya watu wengine. Hatutasonga mbele zaidi ya kurudia hayo hayo.
 
Hayo ni mawazo yako , usipende kuwalisha watu maneno yako ili wafuate maamuzi yako. hapa tuelimishane na tuangalie vifungu mbalimbali kuliko kurudia rudia maneno yako unayopenda wewe kuyasikia na hupendi kusikia ya watu wengine. Hatutasonga mbele zaidi ya kurudia hayo hayo.

mawazo yangu ndio na nina haki ya kuyatoa.
 
Kiongozi kumbe hata ww umewaona wachumia tumbo, wanakurupuka tu!

Kila mtu ni mchumia tumbo hapa duniani ukitaka kulijua hilo kaa nyumbani na uwe jobless utelewa,tumbo ndio linakufanya ufanye kazi ndio maana imeandikwa ASIYEFANYAKAZI NA ASILE! wee mwenyewe ni mchumia tumbo tu! Mie nimemuelewa labda uelewa wangu na wenu uwe tofauti!Tanzania inao vijana kibao ambao wanajihusisha katika utumiaji wa vinywaji vikali na madawa ambayo yanaathiri nguvu kazi ya taifa, mara nyingi hawa huweza kurubuniwa kwa malengo fulani, Katiba pendekezwa imetoa wigo mpana kwa vijana hao kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo yao na taifa na kuwaondoa katika mazingira yasiyofaa Ibara ya 54 inaeleza yote hayo!
 
Back
Top Bottom