Pre GE2025 Vijana wasichague viongozi kwa mihemko ya kivyama au chuki, bali kwa uwajibikaji na sera bora zinazotimizika

Pre GE2025 Vijana wasichague viongozi kwa mihemko ya kivyama au chuki, bali kwa uwajibikaji na sera bora zinazotimizika

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

kagram

Member
Joined
May 1, 2024
Posts
5
Reaction score
3
Kumekuwa na mashindano mengi ya mpira hasa mpira wa miguu kwenye majimbo na kata mbali mbali nchini.

Kwa jicho la kawaida ni jambo zuri lakini kama ukijiuliza ni kwanini ije kipindi hichi na sio miaka miwili au tatu iliyopita tena ikija na ahadi nyingi na fedha nyingi basi utagundua ni siasa imejaa na viongozi wanajiweka karibu na vijana ambao ndio wengi kwa idadi hapa nchini ili waweze kupata kura zao.

Maoni yangu au wito wangu kwa vijana wasiache kushiriki hiyo michezo washiriki na kama kuna fedha wachukue wasichezee fursa ila wawatathimini hao viongozi kwa ahadi zao walizozitoa uchaguzi uliopita je wamezitimiza? Na wasichague viongozi kwa mihemuko ya kivyama au chuki kwa chama fulani ila wachague kwa kigezo cha uwajibikaji sera bora na ahadi zinazotimizika.
 
Kuna mtu bado anaamini uchaguzi ndio unaotoa viongozi? Kwa taarifa yako tu ni kuwa ccm sio chama cha kizazi hiki, ndio maana inalazimisha kupora chaguzi ili wakae madarakani kwa shuruti. Matokeo yake watu wamepuuza hizo chaguzi, maana kushiriki kwenye chaguzi ambazo kura haziheshimiwi, hayo ni matumizi mabaya ya raslimali muda.

Machafuko ama mapinduzi ya kijeshi pekee ndio yatarejesha heshima ya box la kura, na mabadiliko ya kweli.
 
Back
Top Bottom