MWANAHARAMU
JF-Expert Member
- Dec 12, 2021
- 4,041
- 10,699
Tanzania ni nchi inayofuata Mfumo wa Ubaba.
Yaani baba ndio kichwa Cha familia, jina la baba la ukoo ndio hurithi mtoto.
Yaani kwa Tanzania sio tu watoto urithi Mali Bali pia hurithi ubini pamoja na kabila na huna jinsi utakavyo weza kubadili.
Jamii humtambua mtu kutoka ubabani.
Huu ndio utambulisho wetu,
Mtoto atarithi kabila toka kwa babaye
Yaani Mallya, Mushi, Njau tunajua ni mchaga haijalishi mamaye ni nani.
Halikadhalika Mwakyusa, Mwakapesa, Mwakasitu, Mwakimeme tutambua ni Mnyakyusa.
Kule pwani tunatarajia majina kama akina Pazi, Nyumba, Ngwale,Mbwela, kibanda au Kikwete tunajua huyu atakuwa Mkwere, Mzaramo, Mndengereko, Mnyagwata au Mngindo.
Tatizo Kuna kundi kubwa la watoto ambao huzaliwa bila kujua baba zao, baba zao kuwakana, kutotambuliwa toka Koo za baba zao huwa wanawekwa kundi gani?
Maana upande wa kikeni namaanisha ule upande wa mama yake huwa hawaesabu kama upande wake yaani wanajua ni ndugu yao ila hujulikana kama Mgeni.
Kiafrika mtoto wa Mwanaume ni mrithi halali wa Mali za baba yake, Tambo za ukoo wake na sifa za kabila lake atake au asitake.
Kiafrika mwanamke hayupo kwenye Kutoa ubini ila uhesabiwa ameolewa hivyo yupo kwenye Koo ya Mwanaume.
Athari kubwa huwa zinakuwa kwa mtoto aliyezaliwa huku atambuliwi na upande wake stahiki au haujui.
Mfano: John alikuwa na miaka 25 akiwa amelelewa na mama yake bila kumjua baba yake hivyo kupelekea kukataliwa, upande wa kikeni kuwa sio mmoja wa wanaukoo ila pia hawezi jiita upande wa kiumeni.
Akawa anashindwa kujitambulisha kwa kujiamini, kitu kilichompelekea kupata athari za kisaikolojia.
Anashindwa kujua atazikwa wapi?
Atapewa heshima na familia yake?
Ukoo wa upande wa mama yake watamkubali kuzikwa kwenye eneo la makabuli yao?
Historia yake itakuwaje?
Uzao wakwe utawekwa kundi gani?
Kiukweli sehemu ya identity yake ilishaporwa?
Tanzania ina makabila 128, na karibia watu Milioni 60 hujinasibisha na haya makabila ila kwa mtu asiyemjua mzazi wake hupata kigugumizi kusema kabila lake.
Kukubali yeye ni mbegu iliyopotea hakubali, ila kujitambulisha ni anatokana na jamii fulani haiwezekani.
Hili kundi uishi chini ya kivuli Cha:
(1)Kukosa kujiamini
(2)Kudhaniwa kuwa sio raia
(3)Kusengenywa kuwa ni watoto haramu
(4)Kuonekana wamevamia Koo
(5) Uoga
(6)Kukosa utambulisho
(7)Kukosa majina ya Koo au familia
(8) kutokuwa sehemu ya kabila lolote
(9) Kuharibikiwa kwa tabia
(10) Matumizi ya mihadarati
(11) Kujikana
(12) kuleta madhara kwenye jamii hasa roho ya ukatili.
(13) Kujiua
(14) Kumdharau mama yake
(15) Kuhusishwa na tendon la zinaa
Jamii inajifanya imevaa miwani, hili kundi hushika madaraka, wasomi au majirani zetu.
Hawa watu huteseka kimya kimya kutokana na identity crisis, hivyo wengi h
uishi kwa kuishia hapa duniani maana ni aibu iliyo hai.
Lakini ukiangalia trend ya Sasa, ni kama kuwa single mama ni jambo linalopewa sifa na heshima na jamii.
Kudanga ni sifa ya wanawake wajanja na walio elimika ilihali wakija pata ujauzito uteseka maisha yao yote.
Wengi hudhani kundi hili la watoto huwa na vipaji maalumu kitu ambacho sio kweli.
Hili ni kundi linalohisi kubaguliwa, kudhihakiwa, kudharauliwa hadi kunynnyaswa toka siku ya kwanza wangali duniani kwa kuitwa watoto haramu,
wengi huingia katika vitendo visivyofaa kwenye jamii hivyo kutokuwa na sifa njema.
Hivyo wachache walioamua kutokubaliana na hali halisi na kuamua kupigana kukombowa maisha yao.
Kumbuka huyu hana Urithi Wala matumaini toka kwa baba Wala mama.
Naomba nifafanue kidogo Grace Lalago alipata mtoto wa kiume toka kusikojulikana na baba mtoto kuamua kukana mimba.
hivyo mimba na baadae mtoto kulelewa upande wa Mwanamke yaani kwa wajomba maana hakuwana jinsi.
Grace Lalago miaka mitano(5) baadae to alipata mume na kuolewa na Mumewe alijulikana kama bwana Magembe.
Baada ya miaka kumi bwana Magembe ambaye ni msukuma kwa asili, alipata watoto wake watatu(03) Toka kwa Grace.
Ambao ukoo wao ni Magembe na walikubalika huko Usukumani, Mali zote za Bwana Magembe siku Moja zitarithiwa na hao watoto.
Yule mtoto wa Grace Lalago alikuwa hana tumaini jingine nje ya shule, hivyo alilazimika kusoma kwa bidii na maarifa ili aweze kuexcell kwenye masomo na siku Moja awe mtu muhimu kwenye Taifa hili.
Ukisoma kisa hiki usisahau kusoma kisa Cha Diamond pamoja na mafanikio yake yote ila bado ana identity crisis.
Ndio mara ajiite Nyange au ajiite Abdul.
Kisa kingine ni Q chilla na historia yake.
Unapokuwa binti kumbuka unawajibu si tu wa kuchagua mchumba bali wa kuwachagulia watoto wao baba mzuri na historia ya maisha yao.
Kujifanya umjini mwingi hakuna kheri ila shida kabla ya uzee wako.
Kuna kisa kingine ambacho siwezi kuwaacha bila ya kuwahadisia,
kuhusu Mama mmoja aliye pigwa mapanga mpaka kifo chake kisa watoto wake kutaka kujua asili yao yaani baba yao, maana kule Usukumani walikuwa wanatukanwa na wananzengo kuwa wao wamebaka kabila na Warudi kwao.

Upvote
3