Vijiji vya Jimbo la Musoma Vijijini Vyaendelea Kusambaziwa Maji ya Bomba Kutoka Ziwa Victoria

Vijiji vya Jimbo la Musoma Vijijini Vyaendelea Kusambaziwa Maji ya Bomba Kutoka Ziwa Victoria

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

VIJIJI VYA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI VYAENDELEA KUSAMBAZIWA MAJI YA BOMBA KUTOKA ZIWA VICTORIA

Wiki hii imekuwa ya furaha tele kwa vijiji vya Mabuimerafuru (Kata ya Musanja) na Chumwi (Kata ya Nyamrandirira) kupata maji ya bomba ya kutoka Ziwa Victoria.

Tenki la ujazo wa lita 300,000 limejengwa Kijijini Mabuimerafuru. Maji ya tenki hili yatatumiwa na vijiji vya Kata nne (4), yaani Mabuimerafuru (Kata ya Musanja), Chumwi (Kata Nyamrandirira), Murangi, Lyasembe (Kata ya Murangi) na Masinono (Kata ya Bugwema)

Tafadhali, kutoka kwenye CLIP/VIDEO iliyoambatanishwa hapa, sikiliza shukrani nyingi zilizotolewa kwa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

DC wa Wilaya yetu, Dkt Khalfany Haule, ametoa ushauri na maelekezo mazuri ya utumiaji na utunzaji wa miundombinu ya maji ya bomba kwa wananchi wa Musoma Vijijini.

Vijiji vyote 68 vya Jimbo letu vina miradi ya usambaziwaji wa maji ya bomba, na miradi hiyo iko kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6
Musoma

Tarehe:
Jumapili, 16.6.2024
 
Hivi ule mradi wa maji wa kutoka MGANGO - KIABAKARI ulikwishaisha na wanachi kuanza kutumia maji maji?
 
Back
Top Bottom