Vijiji vya Ujamaa vilivyokufa ni vipi?


Keil,

Leo umeamsha munkari wangu.

Nitamuomba samahani Mzee Mwanakijiji kwa kutoka nje ya mada kidogo, kusogoa na Keil.

For the past 6 weeks I have been having a self debate about role of Party (TANU-CCM) and Government of Tanzania in solidifying poverty in Tanzania.

Mfano swali moja ambalo najaribu kuliundia hoja na hata kuanzisha thread ni kuhoji mfumo wa mapato ya serikali ya Tanzania.

Ukiangalia majedwali ya BOT hata bajeti, unakuta Serikali inaongea kwa HERUFI kubwa kuhusu mauzo ya mazao kama pato la Taifa. Lakini swali langu ni hili, ni kwa kiwango gani kipato hicho kwa uhalisi kinaenda kwa aliyevuja jasho? nikiwa na maana Mkulima?

Mpaka leo hii Mkulima wa Tanzania anapokea kama mapato si zaidi ya 15%-20% ya bei ya mazao yake. Kuna Serikali za vijiji, vyama vya ushirika, bodi za mauzo, wizara mama na serikali kuu ambazo kila moja inanyofoa shilingi zake kutoka bei ya Korosho.

Jiulizeni kama Mkulima angekuwa na uwezo kamili wa kujitafutia soko na kuuza anakotaka leo hii watu wa Vijijini wangekuwa wapi kimaendeleo?

Sasa hapa nitamjibu Zakumi na swali lake kuuliza tuonyeshe Mizania za Vijiji (balance Sheet).

Ikiwa Serikali inanyakua faida yote ya mazao na mkulima akija kupewa pesa yake kila mara he is breaking even (uwiano wa gharama za yeye kuzalisha na mapato ni sawa bila kuwa na faida ya kutosha au ziada), jitihada zake kusonga mbele zinabakia pale pale, ungetegemeaje yeye ajenge nyumba ya bati, achangie dawati au kuungana na kujenga hospitali?

Hivyo pamoja na kuwa tulipiga vita Unyonyaji, tuliruhusu unyonyaji wa Dola kupitia Chama cha Kisiasa na Serikali kuwa mmiliki na mnufaika mkuu wa mapato kwa kisingizo cha kujenga nchi (si kujenga Taifa, those are two different things)!

Ndio maana ukiwasoma CHADEMA na sera yao ya Majimbo wanadai kuwa kila wilaya itarejeshewa kwa kiwango kikubwa fedha za makusanyo ya kodi na mauzo ili wilaya zijiendeleze.

Nitajitahidi kufungua mada maalumu, kuchangua Serikali ya Tanzania na mfumo wake wa mapato hapo baadaye.
 

Don't evade the point! The point is: Umeudanganya Umma! Apologize to the public!
 
Butiama hakikuwa kijiji cha ujamaa?If so then sera yote haikuwa sahihi...you start from home
 
Keil,

Naomba usome hii habari kutoka Raia Mwema. Angalia ni jinsi gani watu wanatoka jasho halafu wanawekewa vikwazo kunufaika kisa Serikali na wakala wake hawana uwezo! Let them find market and dictate the prices!

 


President Julius Nyerere urged Tanzanians to reject capitalist exploitation, and build a society based on African communalism. Ntimbanjayo Millinga with a few others and hardly any funding put these views into practice and built an extraordinary rural society based on equity between women and men, young and old. By 1969, 17 ujamaa villages had formed the Ruvuma Development Association (RDA). But the governing party was so hostile to grassroots power that, against Nyerere’s will, they closed it down. Tragically, Millinga died in 2008. But the RDA he led is a beacon in our struggle today.






Najaribu kuipitia hii phase over and over.
 
Butiama hakikuwa kijiji cha ujamaa?If so then sera yote haikuwa sahihi...you start from home

Butiama kilikuwa kijiji cha ujamaa na kilikuwa mbele sana kwenye utekelezaji wa sera hii. Kilimiliki mali nyingi kijamaa ikiwemo karakana ya kisasa kabisa ya zana za kilimo, malori ya kusomba mazao na mbolea, mashamba makubwa tu ya kijamaa, walijenga community centre nzuri sana,....Kilichoua miradi ya vijiji hivi ni uhasibu mdogo sana wa miradi hii, ufisadi na uongozi hafifu mno. Vijiji vyenyewe bado vipo na ukienda pale Butiama utaona baadhi ya alama za ujamaa.Kilichonishangaza mimi ni jinsi mashirika ya UMMA yalivyokufa tena yakiongozwa na yale yaliyokuwa yanamilikiwa na TANU/CCM kama SUKITA, MECCO,....
 

Mimi nimewahi kufika Butiama,na zijaona haya....vitu impressive pale ni vile vya Mwalimu na familia yake...sasa kama watu waliweza kuuwa kijiji cha muasisi mwenyewe then there were more than problems in the policy....
 
Vijiji vya ujamaa bado viko mkoa wa Kilimanjaro katika wilaya za Same na Mwanga, kule kando ya ziwa Jipe, vijiji kama Kigongo nk ni vya ujamaa. Maeneo ya lower Moshi kuna vijiji kama Mvuleni, Newland vyote vya ujamaa na vipo hadi leo.
 
Vijiji vya ujamaa bado viko mkoa wa Kilimanjaro katika wilaya za Same na Mwanga, kule kando ya ziwa Jipe, vijiji kama Kigongo nk ni vya ujamaa. Maeneo ya lower Moshi kuna vijiji kama Mvuleni, Newland vyote vya ujamaa na vipo hadi leo.

Vipo kwa majina au vina operate kama VvU?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…